DOKEZO PreGE2025 Lissu aondolewa Keko. Anapelekwa wapi?

DOKEZO PreGE2025 Lissu aondolewa Keko. Anapelekwa wapi?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Kimsingi nchi yetu ilichelewa sana kumpata mtu aina ya Tundu Lissu, ambaye ni jasiri, mpambania haki na pia mzalendo kwa nchi yake! Huku akiwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa ndani na nje ya nchi.
Kabisa mkuu walikuepo wengi sema muda ulikua hauja fika. Sema wamepotezwa wengi pia huyu alijua muda upi na mahala gani akifika anaweza kuonesha alichonacho kwa ukubwa huu. Angekua mtu wa chini wangesha muua siku nyingi
 
Wapo wapi akina idd Amini Dada, Mabutu, bokasa, sadam Hussein magu na wenzao? Uchawaccm wako usikufanye kujitoa fahamu kuharalisha vitendo vyenu haramu vya kishetani
Soda's Power hamna uwezo wa kufanya lolote , endeleeni kulialia mitandaoni.
 
Madai ya mh rais kuchafuliwa na swala hili hayana msingi wowote.
Lisu ni mmoja wa maelfu ya watuhumiwa wa uhalifu walioko huko magerezani ambao uwepo wao magerezani hauna athari ya aina yoyote kwa heshima ya mheshimiwa rais.
Lisu sio mtuhumiwa pekee ambaye yupo gerezani.
Huko gerezani yupo na wenzake wengi tu kwahiyo mwacheni apambane na hali yake hadi siku ya kutoka atakuwa ana adabu kidogo kama ilivyokuwa kwa freeman Mbowe alivyokaa gerezani miezi kadhaa akatoka akiwa na adabu kiasi.
jitahidi kutofautisha ujinga na upumbafu
 
w980-p16x9-2025-04-12T172014Z_1141611647_RC2WUDAKB3LX_RTRMADP_3_TANZANIA-POLITICS.jpg

Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu amehamishwa gereza la Keko alikokuwa akishikiliwa, huku mahali alikohamishiwa pakiwa hapajulikani.

Msemaji wa Jeshi la Magereza, Elizabeth Mbezi alipoulizwa kuhusu taarifa hizo alisema bado hajazipata.
halipoulizwa kama kuhamisha watuhumiwa na wafungwa ni siri, amesema, "Inategemea na makosa, yapo makosa wanahamishwa kwa siri na yapo makosa hawahamishwi kwa siri." Alipoulizwa kuhusu tuhuma za Lissu, alisema, "Ngoja nifuatilie kwanza."

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa ,Mawasiliano na Uenezi, Brenda Rupia leo Ijumaa, Aprili 18, 2025, imesema viongozi wa Chadema akiwamo Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Wakili Ali Ibrahim Juma, Mawakili, wanafamilia na wanachama kwa nyakati tofauti, wamefika katika Gereza la Keko kumwona Lissu, lakini hawakufanikiwa kumwona.

“Juhudi zao za kumuona Mhe. Lissu hazikufanikiwa baada ya kuelezwa kuwa hayupo katika gereza hilo, cha kusikitisha, hawakupewa maelezo yoyote rasmi juu ya alipopelekwa.”

Chama hicho kimelitaka Jeshi la Magereza, mamlaka husika na vyombo vya Dola kutoa taarifa wazi na za haraka kwa umma kuhusu mahali alipopelekwa Lissu.

“Iwapo bado anashikiliwa katika Gereza la Keko, ni haki ya familia, viongozi na wanachama kumuona - ni haki ya msingi ya kibinadamu na kikatiba,” amesema Brenda.
 
Madai ya mh rais kuchafuliwa na swala hili hayana msingi wowote.
Lisu ni mmoja wa maelfu ya watuhumiwa wa uhalifu walioko huko magerezani ambao uwepo wao magerezani hauna athari ya aina yoyote kwa heshima ya mheshimiwa rais.
Lisu sio mtuhumiwa pekee ambaye yupo gerezani.
Huko gerezani yupo na wenzake wengi tu kwahiyo mwacheni apambane na hali yake hadi siku ya kutoka atakuwa ana adabu kidogo kama ilivyokuwa kwa freeman Mbowe alivyokaa gerezani miezi kadhaa akatoka akiwa na adabu kiasi.
Inaonekana hujui how politics is na namna Nchi zinavyoendeshwa.

Nenda kasome Ushauri aliopewa Mwl Nyerere kabla hajang'atuka madarakani Mwaka 1985 na Benki ya Dunia na Jamii ya Kimataifa

Kama unadhani huko gerezani wapo wengi wanaostahili kuwa detained kwanini anayeimbwa ni huyo Lissu

Kuna watu tangu Nchi yetu ianze mfumo wa Vyama vingi wapo huko Upinzani kwaajili ya Check and balance ndiyo hao akina Mbowe na Lissu
 
Back
Top Bottom