Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,575
- 13,261
Tundu Lissu amejibu tuhuma zilitolewa dhidi yake kwamba anayoyasema kuhusu Rais Samia na mtoto wake Abdul kutoa pesa ili kuvuruga uchaguzi ndani ya CHADEMA.
Majibu hayo yamekuja baada ya member wa JamiiForums.com kuandika andiko likiwa na madai hayo
Pia soma: Inadaiwa hasira za Lissu zinatokana na kunyimwa gari na Rais Samia
Lissu amejibu baada ya kutafutwa na JamiiForums, ambapo amesema:
"Mimi sijawahi kuomba favour yoyote, narudia, yoyote, iwe ya gari au kitu kingine chochote kutoka kwa Rais Samia.
"Kitu pekee ambacho nimekidai kwake ni haki zangu za:
(a) Kupatiwa passport nyingine baada ya mwanzo kuibiwa;
(b) Kulipwa kiinua mgongo kwa muda niliofanya kazi ya Ubunge,
(c) Kulipwa stahiki za matibabu yangu baada ya shambulio la Sept 2017.
"Katika madai hayo, (a) na (b) yalitekelezwa kabla ya mimi kurudi nchini mapema mwaka jana, na nilisema hivyo hadharani. Madai ya fidia ya matibabu hayajalipwa hadi hivi sasa na nimesema hivyo hadharani mara nyingi.
"Tuhuma za rushwa hazina uhusiano wowote na kuvunjika kwa maridhiano. Mimi binafsi nimeanza kuzungumzia hadharani juu ya kukwama kwa maridhiano mapema kabisa ya mwaka jana.
"Nimezungumzia rushwa za Abduli na mama yake wiki mbili zilizopita. Wanaoamini kuna uhusiano wowote kati ya masuala haya hawajatumia vichwa vyao sawa sawa.
"Kuhusu ushahidi wa rushwa za Abduli na mama yake, ijapokuwa rushwa huwa haitolewi risiti, kuna ushahidi wa kutosha wa uwepo wa rushwa na mwenye macho haambiwi tazama!"
=====
Pia soma:
- Tundu Lissu atahadharisha uchaguzi ndani ya chama kuingiliwa na fedha za Rais Samia na mwanae Abdul