Uchaguzi 2020 Linapokuja suala la kuiondoa CCM madarakani, wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ni kikwazo

Arusha tunajua mnasupport watu wenu as wabunge wengi ni kutoka huko.

Mwanza watakuja kuwasikiliza as Wasukuma ni wastaarabu,watakuja kuona show ya bure then kura watampigia Magufuli,lake zone hamtoboi.

Magufuli anapendwa huko hatari.
Huku Mwanza Chadema hawezi kutoboa hata kidogo.
 
Kila mtu ukweli wa kile anachoamini huwa moyoni mwake. Na matendo huongea kwa sauti kubwa kuliko maneno. Watanzania wengi wanampenda JPM, wanapenda anachofanya ndo maana walimpigia kura miaka mitano ilopita na hata sasa watampigia tena.
 
Hawa wa DSM wanataka sana HOJA, uwaeleze mambo kwa hoja siyo uwatake wafanye mambo kwa MIHEMUKO. Wa Dar-es-Salaam wana mambo mengi ya kulinganisha hasa inapokuja kwenye masuala ya elimu, miundombinu, mahospitali na mambo mengine mengi ya maendeleo.


Wengi, nje ya jiji la Dar-es-Salaam labda wana kosa uwezo wa kudadavua mambo na hoja za wanaharakati, wapinga maendeleo na vibaraka wao. Kwa mantiki hiyo kuwafanya washabikie kila neno toka kwa wapinzani, ingawa SI KWELI WAKATI WOTE! Ona wananchi na Watanzania katika nchi yote watoavyo hoja za kupinga kauli za akina Lissu, Zitto na wengine kuhusu maendeleo tunayoyaona hapa nchini.


Kila mtu anajua umuhimu wa miundombinu ya reli, barabara, flyovers, ndege, bandari, usafiri wa majini, vivuko n.k. katika ujenzi wa uchumi kuwa HIVYO NI VITENDEA KAZI katika kuharakisha na kuchangamsha biashara (za nje na za ndani), kuharakisha utoaji wa huduma muafaka na mambo mengine kama hayo ambayo wewe na mimi tukiyachangamkia tutanufaika KIUCHUMI, tofauti na dhana na madai potofu kuwa "hayo ni maendeleo ya vitu"! Hawa wachumi wa leo wana mambo ya AJABU SANA, SIJUI VIPI?
 
Watanzania kipindi hiki wanachagua maendeleo, wamechoka na blah blah. Kuulaumu leo Mkoa wa Dar es Salaam ni kukosa fadhila kisiasa.

2015 Jiji la Dar es Salaam liliongoza kwa kuwapa wabunge 6 (Mtulia, Mdee, Kubenea, Mnyika, Waitara na Mtolea) na madiwani lukuki..lakini kipi cha ajabu walichofanya? Sawa labda hawa kupewa ishirikiano na Serikali..vipi ukaribu wao kwa Wananchi waliowachagua? Aibu tupu...

Kiukweli katika kipindi ambacho hatutaki blah blah na michezo ni kipindi hiki. Upinzani umevuruga wenyewe na hauna sifa tena jiji la Dar es Salaam..!
 
Aisee, CHADEMA ndio walikuwa kundi la wanufaika wa wizi uliokuwa ukiumiza nchi huko nyuma? CCM ndio wazalendo wa kweli? Safari hii Watanzania lazima wapate kizunguzungu!
 
Upinzani Nchi hii naona bado sana, kama vyama zaid ya 10 (vya upinzani)vinapingana vyenyewe kuitaka Dola sisi wananchi tufanyeji, Upinzani utashika Dola pale tu utakapokua na sera mbadala na pia utakapokuwa na dhamira ya dhati yakuacha tamaa ya madaraka na kuamua kuungana dhidi ya Chama Tawala ili kuwaletea WANANCHI maendeleo ambayo wanahisi bado hayajafikiwa.
 
Dar waga nawashanga sana wamekalia simba na yanga ujinga mtupu timu hata ukizijumlisha zote upati timi moja wote awajui kucheza mpira dar pia chips mayai zinawardusha nyuma unakuta mwanaume mziga anakula chips na mayai na demu wake wote ni chips unategemea nini
 
Sio kweli kuwa Dar haipendi mabadiliko:
(1) Huwezi kupima uungwaji mkono kwa kuangalia wingi wa watu wanaokuja kwenye kampeni viwanjani kwa sababu:
(a) Watu wengi, kama sio wote wa Dar wanapata taarifa nyingi na kwa wakati kupitia simu zao (twitter, IG, Facebook, whatsap, n.k) kwa hiyo hawana haja ya kwenda viwanjani kujua wagombea wanaahidi nini. Mimi mfano kila siku jioni naenda Youtube na JF na Twitter na naweza kuona na kusoma habari nizitakazo za wagombea.
(b) Watu wengi wa Dar wana shughuli na miangaiko mingi inayowafanya warudi majumbani hoi. HIvyo muda na nguvu za kusimama viwangami hawana

Vilevile watu wengi wa Dar ni wasomi na wakishasikiliza wagombea mara moja wanakuwa wameshaelewa na hawaitaji usawishi zaidi kuwabadilisha. Wanasubiri tu siku ya uchaguzi wampigie kura mtu wao.

Kwa hiyo watu kuwa wachache kwenye kampeni ya Lissu au JPM isitupumbaze. Wana Dar wengi wameshafanya maamuzi wanasubiri 28-October wachague Uhuru, Haki, na Maendeleo yao.
 
Wale wanatumia akili kufikiri.

Lisu alisema mikataba ya madini haiwezekani tutaiweka nchi pabaya JPM ingawa sio mwanasheria akaona hapana akajitoa kwa nguvu zote na moyo wote kuitetea Tz dhidi ya mabeberu na akashinda.

Lissu mpaka leo hapendi jinsi Tz tulivyoamua kupambana na CORONA kivyetu vyetu kila siku analia tufate amri za wazungu!

JAMANI KWA MWENYE AKILI TIMAMU YEYOTE JE HUYU MTU NI WAKUPEWA MIHURI YA NCHI?

MAGUFULI4LIFE.
Pamoja na hiyo mikataba ya madini, mtanzania wa kawaida anafaidika na nini?
Je, hata maji ya bure anapata?
Au umeme wa bei nafuu?
Acheni undezi wazee
 
Pia ni ajabu ya karne Jiji kama la Dar es Salaam kuendelea kuwa na wabunge wa Chama kilichozeeka kama CCM achilia mbali kuwepo na wakazi ambao bado kwao CCM ni kimbilio. Dar mnakwama wapi?
Huna shukran wewe
2015 chadema ukawa waliteka manispaa zote kasoro ilala na wakabeba halmashauri ya jiji
Wapinzani kwa Sasa mmechokwa watu wameamua wafanye Mambo mengine,nendeni huko mikoani Dar tumewachoka
 
Umesema vizuri kwamba wana Dar wana exposure kubwa ukilinganisha na majiji na miji mingine Tanzania.

Hivyo wanajua kuchambua mchele na pumba sasa kama wapinzani hawana hoja bali ni pumba tuu unategemea nini? Unafikiri wana Dar ni wafuata upepo kama wewe.

Kamjulishe Lissu kuwa sisi mwaka huu piga ua garakaza tuko na Rais Magufuli full stop.
Jibu Konki
 
Hapa nimefanya kazi ya kutoa Like kwa kila aliyekuwa na mtazamo chanya kuhusu CCM ya Magufuli.

Jamani JPM ni deal wadau acheni mihemuko msije badae kujiona wajinga.

Kiukweli kumsapoti kwangu Lowasa 2015 siku hizi nikitulia huwa nahisi usaliti fulani
 
Back
Top Bottom