Uchaguzi 2020 Linapokuja suala la kuiondoa CCM madarakani, wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ni kikwazo

Leo nimeona niliamkie jiji Dar es Salaam.

Linapokuja suala la kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi majiji makuu ya nchi huwa ni kitovu kwa sababu huwa yana wakazi wengi walioelimika na kupata exposure ya kutosha tofauti na miji mingine katika nchi husika.

Hali ni tofauti nchini Tanzania kwani majiji ambayo yanaonekana ni kitovu cha mabadiliko ni majiji yenye hadhi ya pili na siyo jiji kuu la Dar es Salaam.

Amsha amsha inayofanywa na wakazi wa majiji ya Arusha, Mbeya, Mwanza na hata miji midogo kama Kahama na Shinyanga licha ya kuwa na idadi ndogo ya watu ukilinganisha na Jiji la Dar es Salaam is way too far.

Pia ni ajabu ya karne Jiji kama la Dar es Salaam kuendelea kuwa na wabunge wa Chama kilichozeeka kama CCM achilia mbali kuwepo na wakazi ambao bado kwao CCM ni kimbilio. Dar mnakwama wapi?

Mfano mdogo wa hivi karibuni ni ukweli ulio wazi idadi ya wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA haikuridhisha. Sasa tazama Arusha ilivyompokea Tundu Lissu kwenye kampeni jana.

Hata linapokuja suala la haki kwa watetezi wenu wa haki, mfano kupigwa risasi Tundu Lissu, kupotea kwa akina Ben Saanane, Azori Gwanda, kupigwa na kudhalilishwa kwa akina Halima Mdee na Jeshi la Magereza, tulitarajia mjitokeze kwa wingi kupinga uonevu wa aina hii. Lakini uoga umewazidi.

DAR ES SALAAM AMKA UONGOZE MAPAMBANO, ACHA UOGA.

DAR ES SALAAM UNAHITAJI MAISHA BORA NA UHURU KULIKO ILIVYO SASA UNAONEKANA KAMA ZIZI LA NG'OMBE, UCHAFU KILA MAHALI, MITARO MICHAFU, UKOSEFU WA MAJI SAFI NA SALAMA, MIPANGO MIJI YA HOVYO KULIKO MAJIJI YOTE DUNIANI. AU UMERIDHIKA NA VIDARAJA VYA UBUNGO NA MFUGALE? DAR TEMBEA UONE NDIPO UTAJUA HUJUI NA WATAWALA WANAKUHADAA.

YOTE HAYO NI HAKI YAKO MAANA UNALIPA KODI KULIKO MIJI YOTE NCHINI TANZANIA

Siku njema


Dar es salaam ni Rahisi kuishika.

Ukishamshika Mkono Shekhe mkuu wakoa wa Dsm.
Ukamshika mkono Malasusa.
Ukamshika Mkono Pengo.
Ukamshika Mkono Gwajima.
Ukamshika mkono Mzee wa upuku, unakua umeshamaliza jiji lote na huna la ziada hapo.

Hao ndio viongozi wa dini wanaoruhusiwa kupiga kampeni kwenye nyumba za Ibada.
 
Back
Top Bottom