Uchaguzi 2020 Linapokuja suala la kuiondoa CCM madarakani, wakazi wa Jiji la Dar es Salaam ni kikwazo

CreativityCode

Senior Member
Aug 8, 2020
158
653
Leo nimeona niliamkie jiji Dar es Salaam.

Linapokuja suala la kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi majiji makuu ya nchi huwa ni kitovu kwa sababu huwa yana wakazi wengi walioelimika na kupata exposure ya kutosha tofauti na miji mingine katika nchi husika.

Hali ni tofauti nchini Tanzania kwani majiji ambayo yanaonekana ni kitovu cha mabadiliko ni majiji yenye hadhi ya pili na siyo jiji kuu la Dar es Salaam.

Amsha amsha inayofanywa na wakazi wa majiji ya Arusha, Mbeya, Mwanza na hata miji midogo kama Kahama na Shinyanga licha ya kuwa na idadi ndogo ya watu ukilinganisha na Jiji la Dar es Salaam is way too far.

Pia ni ajabu ya karne Jiji kama la Dar es Salaam kuendelea kuwa na wabunge wa Chama kilichozeeka kama CCM achilia mbali kuwepo na wakazi ambao bado kwao CCM ni kimbilio. Dar mnakwama wapi?

Mfano mdogo wa hivi karibuni ni ukweli ulio wazi idadi ya wakazi wa Dar es Salaam waliojitokeza kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA haikuridhisha. Sasa tazama Arusha ilivyompokea Tundu Lissu kwenye kampeni jana.

Hata linapokuja suala la haki kwa watetezi wenu wa haki, mfano kupigwa risasi Tundu Lissu, kupotea kwa akina Ben Saanane, Azori Gwanda, kupigwa na kudhalilishwa kwa akina Halima Mdee na Jeshi la Magereza, tulitarajia mjitokeze kwa wingi kupinga uonevu wa aina hii. Lakini uoga umewazidi.

DAR ES SALAAM AMKA UONGOZE MAPAMBANO, ACHA UOGA.

DAR ES SALAAM UNAHITAJI MAISHA BORA NA UHURU KULIKO ILIVYO SASA UNAONEKANA KAMA ZIZI LA NG'OMBE, UCHAFU KILA MAHALI, MITARO MICHAFU, UKOSEFU WA MAJI SAFI NA SALAMA, MIPANGO MIJI YA HOVYO KULIKO MAJIJI YOTE DUNIANI. AU UMERIDHIKA NA VIDARAJA VYA UBUNGO NA MFUGALE? DAR TEMBEA UONE NDIPO UTAJUA HUJUI NA WATAWALA WANAKUHADAA.

YOTE HAYO NI HAKI YAKO MAANA UNALIPA KODI KULIKO MIJI YOTE NCHINI TANZANIA

Siku njema
 
Wale wanatumia akili kufikiri.

Lisu alisema mikataba ya madini haiwezekani tutaiweka nchi pabaya JPM ingawa sio mwanasheria akaona hapana akajitoa kwa nguvu zote na moyo wote kuitetea Tz dhidi ya mabeberu na akashinda.

Lissu mpaka leo hapendi jinsi Tz tulivyoamua kupambana na CORONA kivyetu vyetu kila siku analia tufate amri za wazungu!

JAMANI KWA MWENYE AKILI TIMAMU YEYOTE JE HUYU MTU NI WAKUPEWA MIHURI YA NCHI?

MAGUFULI4LIFE.
 
Umesema vizuri kwamba wana Dar wana exposure kubwa ukilinganisha na majiji na miji mingine Tanzania.

Hivyo wanajua kuchambua mchele na pumba sasa kama wapinzani hawana hoja bali ni pumba tuu unategemea nini? Unafikiri wana Dar ni wafuata upepo kama wewe.

Kamjulishe Lissu kuwa sisi mwaka huu piga ua garakaza tuko na Rais Magufuli full stop.
 
Dar, kila Lugha zipo, kila kabila zipo, mkusanyiko huo unasababisha kuwa ndilo jiji lenye wasomi wengi

Ukitambua Hilo, basi ni dhahili pia ujue! Hakuna kanda ya kubebwa na jiji la Dar! Hapa ni sera zinazogusa na zilizo na mizania yenye mwelekeo usio tia Shaka hata kidogo ndio zitawashawishi Wana Dar es salam

Unataka eti utuaminishe kwamba Leo hii Tanzania inaeweza kuwa na mfumo wa bima za afya kama Obamacare!!! Wamarekani wenyewe umewashinda halafu wewe Kwa akili yako eti Tanzania inawezekana

Halafu muelewe pia kwamba, Muda wa kumpigania mtu Eti ashike madaraka ulishagapitwa Wakati, hasa katika Taifa la wastarabu Tanzania

Ni Sera nzuri zinazogusa ndio tunashindanisha! Na pia itafika muda ambapo wagombea hawatahitaji kutupozea muda wetu wa kazi kwenda kuwasikiliza wakimwaga mipasho badala ya kumwaga Sera, ni muda ufike wa wagombea kunadi Sera zao kwenye luninga sio kutumia pesa nyiiingi za Kampeni za kutukanana tu la maana hakuna!

Sasa wewe unalaumu tujitokeze kuja kusikiliza mipasho na matusi yanatusaidia nini Sisi Dar!

Pambaneni na Hali yenu"
 
Sio wakazi wa Dar bali wakazi wa Dar wenye asili ya Dar.

Mashabiki wa CCM hapo Dar ni zile familia unakuta binti kafikisha miaka 40 kamleta na bwana ake hapo nyumbani wamezaa watoto 6 wanaishi hapo-hapo na baba mkwe yupo anachekelea wanavyogongana vitambi kugombea foleni ya kuingia chooni.
 
Ni kwa sababu Dar es Salaam ina mchanganyiko wa watu halafu wagombea ubunge wa Chadema wote asili yao kaskazini.
 
Chuki dhidi ya chama tawala ilitokana na madhaifu ya serikali huko nyuma sio kila jiji lazima lisichague chama tawala kwa sasa mambo yamebadilka,imebaki imani tu ya mtu juu ya chama fulani kwamba hiki ni chama changu,kuhusu dar huko nyuma huo mji ulikuwa na kero nyingi ndio maana wapinzani walipata nafasi na unatakiwa uelewe kero nyingi za majiji ni huduma za jamii Maji, umeme, barabara na afya sasa magufuri ametatua karibia asilimia 70% ndio maana wanamuunga mkono, barabara zinajengwa, foleni zinapunguzwa,s tand zinajengwa, huduma za afya za kibingwa zinapatikana, umeme 24hrs, maji hakuna mgao na unaunganishiwa kwa mkopo watu wa dar wana sababu gani ya kuchagua upinzani hiyo miji kama Arusha ni mihemuko, Mbeya, Moshi, mwanza, Tarime, na Iringa ni mazoea ya upinzani lakini si kweli kwamba kila mji Lazima uchague upinzani.
 
Tunavijua vizuri vyama vya upinzani Dar hatuwezi kuwa mtaji wa kutengeneza ruzuku za chama cha familia fulani

Tuliibeba NCCR mageuzi ya mrema na mabere marando baadae wakatuangusha

Tukaibeba CUF wakatuangusha

Tukawabeba CHADEMA lakini mkatuangusha 2020 kwa tamaa za Lisu na Mbowe

Sasa hivi tuacheni tupumzike na siasa upinzani wa uongo

Alafu sasa hivi Dar ni mkoa kama mikoa mingine ya Tanzania tuacheni tupumue

Nimeshapigwa sana mabomu ya machozi kwa ajili ya CUF na NCCR mageuzo kumbe tulikuwa tunafanywa mtaji

Watu wa Dar sasa hivi hatutaki fujo tunasubiri reli ya mwendo kaise ishe tuanze kuemda mikoani kutembe jioni tunarudi Dar kulala
 
Mi naona wamwkidhi matarajiio kwa kiwango kikubwa sana.

Kuanzia kumpokea Tundu lissu, mikutano ya ufunguzi ilikua bambam.

Bado naamini mabadiliko makubwa mwaka huu yataamuliwa na Dar
 
Hii ni hoja mujarabu. Kuna kuna tatizo kubwa la uhamasishaji Chadema Kanda ya Pwani au Mashariki. Kama kuna timu za kampeni hapa jijini basi ni wazi kabisa inafanya kazi chini ya kiwango. Hawafanyi amsha amsha kuelekea mikutano mikubwa. Hakuna matangazo ya kutosha kwa vipaza sauti (haijulikani kwa wakazi wengi kuwa kuna mkutano wa mgombea uraisi).

Hakuna mapikipiki ya amsha amsha. Hakuna amsha amsha kwenye social media kuwavuta wakazi wa jijini wahudhurie. Ukiona nyomi A_town ujue wakina Godbless wamefanya kazi nzuri. Ukiona nyomi Mwanza ujue kuwa Pambalu anafanya amsha amsha vizuri. Ukiona Yanga wamejaa pale uwanja wa Mkapa ujue uhamasishaji ulikidhi viwango.
 
Ni ngumu kwa upinzani kutoboa Dar kuna mambo mengi sana ya msingi ya kimaendeleo ambayo yamefanyika na yanaendelea kufanyika, CCM imerudisha imani kwa wana DSM, siku hizi wana CCM hawazomewe kama zamani, na Dar ndio kitovu cha maarifa kwa Tanzania, watu wake wanajielewa sana.
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom