- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakati Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kikitangaza kufanya Maandamano ya amani leo Jijini Dar Es salaam chini ya Mwenyekiti wake Freeman Mbowe, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda amechapisha mtandaoni mwake akisema anazo taarifa kuwa Mwenyekiti Mbowe yupo Arusha na hivyo kumualika ofisini kwake Jijini Arusha.
Makonda ameandika "Kaka yangu Mbowe kumbe umeingia Arusha na hausemi. Karibu Ofisini basi ukiamua Kutoka"
Ikumbukwe kuwa saa chache zilizopita, nyumba ya Freeman Mbowe iliyopo Mikocheni ilizingirwa na Jeshi La Polisi huku mkewe Dr Lilian Mtei akiripotiwa kuzuia kutoka nyumbani kwake.
Source: Jambo TV
Makonda ameandika "Kaka yangu Mbowe kumbe umeingia Arusha na hausemi. Karibu Ofisini basi ukiamua Kutoka"
Ikumbukwe kuwa saa chache zilizopita, nyumba ya Freeman Mbowe iliyopo Mikocheni ilizingirwa na Jeshi La Polisi huku mkewe Dr Lilian Mtei akiripotiwa kuzuia kutoka nyumbani kwake.
- Tunachokijua
- Freeman Mbowe ni mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambaye amekuwa mwenyekiti wa chama hicho kwa muda wa miaka 20 sasa.
Septemba 11 2024, CHADEMA kupitia mwenyekiti wake, Mbowe alitangaza kuwepo kwa maandamo 23, Septemba 2024, ili kushinikiza kuchukuliwa kwa hatua dhidi vitendo vya utekaji na mauaji nchini ya watu mbalimbali ambapo baadhi ya viongozi wa CHADEMA wamepotea huku mmoja, Mzee Kibao akitekwa kwenye basi na baadaye kukutwa akiwa kafariki dunia, ambapo CHADEMA walisisitiza kuw iwapo wliyosema yasipotimizwa 23, Septemba 2024 wataandmana.
Mapema 23, Septemba 2024, imeripotiwa baadhi ya wanahabari taarifa (Tazama hapa na hapa) kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amechapisha kwenye mtandao wa kijamii akidai Mbowe ameingia Arusha na hivyo kumkaribisha ofisini kwake.
Pia JaamiiCheck imepita kwenye akaunti ya Paul Makonda ya Instagram na kukuta chapisho hilo kama linavyoonekna hapo chini.
Je, ukweli ni upi?
JamiiCheck imefatilia tarif hiyo na kubaini kuwa haina ukweli kwani vyanzo vyetu vya kuaminika vimetueleza kuwa mbowe yupo Dar Es Salaam na si Arusha kama taarifa hiyo inavyodai.
Aidha, Mbowe ameonekana Magomeni akiwa amefika ili kuongoza maandamano ambapo baadaye imeripotiwa kakamatwa na Polisi akiwa Magomeni Dar Es Salaam, jambo ambalo linathibitisha kuwa taarifa ya Mbowe kuingi Arusha Si ya kweli.
Tazama Video Mbowe akiwa Magomeni, Dar Es Salaam, Septemba 23, 2024