#COVID19 Leo ni siku ya Afya ya Akili, Je Watanzania tutumie chanjo ya Corona kama kipimo cha utimamu wetu?. Wapinga chanjo, sio wazima! Je ni vichaa?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,597
Wanabodi,

Leo October, 10 kila mwaka ni siku ya Afya ya Akili, kuna ule utafiti, ulioonyesha kuwa kwenye kila Watanzania 4, mmoja ana tatizo la Afya ya akili.

Matokeo ya utafiti huo, umerudiwa leo asubuhi kwenye TBC na daktari mmoja Mtaalamu wa Afya ya akili kwenye mahojiano ya kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa live kila asubuhi, leo kikijikita kwenye kuizungumzia siku ya Afya ya akili duniani.

Ili uweze kulielewa bandiko hili kikamilifu, anza na kusoma hoja za gazeti hili.

20211010_093038.jpg

kisha nenda bandiko hili
Kuwa kichaa sio mpaka kuokota makopo!. Je, Tanzania tuna vichaa wengi kuliko tunavyojidhania?!.

Hivyo tunavyoendelea kuiadhimisha, ni vyema kujiuliza jee wewe ni mmoja kati ya wale wanne, ukijikuta ni mmoja wao, unaweza kujitibu kwa kujitambua tuu na kama ni serious, nenda kwa wataalamu, ila wale wenye serious critical problem, huu ni ugonjwa tuu kama ugonjwa mwingine wowote na watu wenye matatizo haya wanahitaji matibabu kama wagonjwa wengine wowote.

Kiukweli kabisa katika Jamii yetu tuna vichaa wengi kuliko tunavyojitambua. Wengi wanadhani kipimo cha kwanza kabisa cha kumjua mtu amechanganyiwa ni kuongea peke yake, hiyo ni stage ya mwisho ya ugonjwa, kiukweli kuna vichaa vichaa wengi, wanaongea vizuri tuu kama ni wazima, ila hayo wanayoongea ndio huwabainisha kuwa sio wazima!.

Miongoni mwao kuna wanasiasa, na hata viongozi wengi tuu, wakiwemo baadhi ya viongozi wetu wa dini, mtu mwenye akili timamu ukiwasikiliza kwa makini utabaini kuwa hata baadhi ya viongozi wetu wa dini, haswa hizi dini za kisasa za uchochoroni, baadhi yao sio wazima, ni vichaa kabisa, japo wana vaa very smart na kuzikusanya sana sadaka!.

Jee mnaonaje tukitumia kipimo rahisi zaidi cha kisasa cha kujipima Afya yako ya akili, ni kutumia kipimo cha chanjo ya Corona. Jiulize jee wewe unaikubali chanjo ya Corona?, ukijikuta unaikubali, then wewe ujihesabu Afya yako ya akili iko vizuri, uko sawa, hivyo kama hujachanja, nenda kachanje. Ukijikuta wewe sio kwamba huikubali na bado hujachanja kwasababu unataka kwanza kujiridhisha kuwa hii chanjo ni salama, hivyo wewe bado ni undecided, then anza kujiuliza, kama wewe ni mzima, au laa ila wale wote wanaopinga chanjo inawezekana kabisa, hawa sio wazima, ni wagonjwa wa akili, ni vichaa ila tuu hawaokoti makopo?, hivyo badala ya kuwashutumu na kuwasimanga, tunahitaji kuwasaidia ili akili zao zirudi, wote tukachanje kulinusuru taifa.

Nakutakia Jumapili njema, na siku njema ya Afya ya akili.
P
 
Wapinga #COVID na chanjo wote wenye hoja za kudandia dandia bila misingi/maelezo ya kitafiti ni vichaa!

NB: Idadi ya vichaa ni kubwa sana. Na tusiwalaumu! Mifumo yetu na viongozi wetu ndo chanzo!
 
Wapinga chanjo wote ni vichaa
Mimi naona nyinyi mliokubali kuchanjwa ndiyo hamna akili! Kwa sababu lengo la hiyo chanjo hata halieleweki ni nini!!

Eti unaweza kuchanjwa, na bado ukapata tena hiyo Corona! Mbona kwenye chanjo nyingine hatuambiwi upuuzi kama huu?

Siku wakija na chanjo ya uhakika kwa 100%, nitachanja. Ila kwa sasa, wacha tuendelee kupigana chenga za mwili.
 
Maoni yangu yakizingatia hoja za wanaopinga chanjo, ilhali wamesha chanja chanjo zaidi ya kumi tangu utoto wao.
Upo sahihi kabisa! Covid ni sayansi! Chanjo ni sayansi! Lakini utakuta kila mtu anajifanya kujua wakati asprini tu hajui kuigawa wala kuitengeneza!

Yaani watu wanazungumzia suala muhimu la chanjo kama wanavyozungumzia timu zao za Ulaya wasizozijua vizuri!
Watu wa hivyo kama siyo vichaa basi ni wendawazimu!!
 
Jana nilikuwa nimekaa kijiwe kimoja cha kahawa sasa akapita rafiki yangu huku amesima na kupaza sauti na kuniuliza ikiwa nimeshachanjwa....nikamjibu kuwa tayari kwa sauti kubwa pia...kile kijiwe wanakaa watu wazima wengi tu wenye heshima zao....baada ya hapo MADA ikaanza.....🤣

Wazee wale wakaanza KUNISHAMBULIA kwa maneno....wakaenda mbali kuishambulia Serikali na wakuu wake kuwa WANATUMIKIA MASLAHI YA MABEBERU Khaaa 😲😲😲Nilishangazwa sana na hoja zao ......

Nilichomaizi ni kuwa BAADHI YA WATANZANIA tuna hulka ya kutopenda kujishughulisha kuutafuta ukweli kutoka VYANZO MBALIMBALI ...Sasa sijajua ni kutokana na UKOSEFU WA ELIMU?!! USHABIKI TU?!!!

Na je ushabiki uliopitiliza si "ukichaa"?!!!🤣🤣

Wataalamu wa afya wanasema UKICHAA una vitu viwili.... DELUSIONS+HALLUCINATIONS.....

"Delusions" mfano wake ni ule mtu kujiona/kujihisi wa maana na mkubwa sana kuliko uhalisia uliopo.....🤣🤣

CHANJO NI BORA KULIKO TIBA

#SiempreJMT
 
Upo sahihi kabisa! Covid ni sayansi! Chanjo ni sayansi! Lakini utakuta kila mtu anajifanya kujua wakati asprini tu hajui kuigawa wala kuitengeneza!
Yaani watu wanazungumzia suala muhimu la chanjo kama wanavyozungumzia timu zao za Ulaya wasizozijua vizuri!
Watu wa hivyo kama siyo vichaa basi ni wendawazimu!!
🤣🤣😍
 
Mimi naona nyinyi mliokubali kuchanjwa ndiyo hamna akili! Kwa sababu lengo la hiyo chanjo hata halieleweki ni nini!!

Eti unaweza kuchanjwa, na bado ukapata tena hiyo Corona! Mbona kwenye chanjo nyingine hatuambiwi upuuzi kama huu?

Siku wakija na chanjo ya uhakika kwa 100%, nitachanja. Ila kwa sasa, wacha tuendelee kupigana chenga za mwili.
Zile za surua na pepopunda ingekuwa unazipata Sasa, nazo ungezikataa, je Ile ya homa ya manjano na Ile ya in au zile za matende , upi mtazamo wako kuhusiana nazo.
 
Mimi naona nyinyi mliokubali kuchanjwa ndiyo hamna akili! Kwa sababu lengo la hiyo chanjo hata halieleweki ni nini!!

Eti unaweza kuchanjwa, na bado ukapata tena hiyo Corona! Mbona kwenye chanjo nyingine hatuambiwi upuuzi kama huu?

Siku wakija na chanjo ya uhakika kwa 100%, nitachanja. Ila kwa sasa, wacha tuendelee kupigana chenga za mwili.
Chanjo ya Ukimwi ikibisha hodi hutochanja?
Chanjo ya kuongeza nguvu za ngono ikifika hutochanja!?
Mbona sadaka mnatoa kwa waganga na makuhani wenu bila hata kuelewa ni za nini, kwa nini?
Ndg; wewe ni kichaa!
 
Unamkuta mtu anaipinga CHANJO dhidi ya CORONA kwa kigezo kuwa zinatoka ULAYA kwa mabeberu....huku kila siku akimeza TEMBE DHIDI YA VIRUSI VYA UKIMWI....sasa sijui hizo tembe zinatengenezwa Lushoto Tanga?!!! 🤣
 
Wazee wale wakaanza KUNISHAMBULIA kwa maneno....wakaenda mbali kuishambulia Serikali na wakuu wake kuwa WANATUMIKIA MASLAHI YA MABEBERU Khaaa 😲😲😲Nilishangazwa sana na hoja zao ......
Deep inside unajua aliyeleta hii kadhia ni nani!
 
Back
Top Bottom