#COVID19 Leo ni siku ya Afya ya Akili, Je Watanzania tutumie chanjo ya Corona kama kipimo cha utimamu wetu?. Wapinga chanjo, sio wazima! Je ni vichaa?

Hata chanjo dhidi ya PEPOPUNDA nayo imetengenezwa huko kwa waitwao "mabeberu" 🤣🤣

Wakijikata tu na kutoka kidonda hukimbilia HOSPITALI kuiulizia SINDANO YA "Tetenasi".....
 
Chanjo ya Ukimwi ikibisha hodi hutochanga?
Chanjo ya kuongeza nguvu za ngono ikifika hutochanja!?
Ndg; wewe ni kichaa!
Hivyo vyote havina tija yoyote ile kwangu. Nguvu ninazo, na pia najitahidi kucheza viwanja salama.

Labda itokee chanjo ya kuongeza miaka ya kuishi hapa duniani! Hapo nitachanja. Maana natamani niishi miaka mingi ili nije kula matunda ya kazi zangu nizifanyazo sasa.
 
Zile za surua na pepopunda ingekuwa unazipata Sasa, nazo ungezikataa, je Ile ya homa ya manjano na Ile ya in au zile za matende , upi mtazamo wako kuhusiana nazo.
Sasa hizo chanjo ukisha chanjwa, unapatwa na hayo magonjwa? Je kwenye jamii yetu kwa sasa unayasikia hayo magonjwa kuwaathiri watoto na watu wazima?

Mimi sikatai kuchanjwa! Ila napenda kuja kuchanjwa chanjo ya ukweli, badala ya hizi takataka zenu mnazopewa na Mabeberu kwa masaharti ya kupata misaada mnayo itumia kupigia ufisadi.
 
Inashtusha.....

Iko hivi.....

Mmoja wa rafiki zangu ni DAKTARI WA BINADAMU....mwenye elimu kubwa tu....kubwa tu kutoka " the most prestigious University".....alinishangaza aliponiambia kuwa HATOCHOMA hiyo chanjo DHIDI YA UVIKO kwa kuwa "dhehebu la dini yake" linapinga hiyo CHANJO....

Nilimwangalia na kubadilisha MADA ili nisijifedheheshe nafsi yangu....

Hebu tizama....ikiwa MTAALAMU WA AFYA....tena kabobea...anatoa maneno hayo.....daah IT IS HAVOC.....😪😪

UKICHAA NI MPANA SANA KATIKA JAMII ZETU
 
kwa wanasiasa na viongozi vichaa ni wale WOTE waliokuwa wanasema chanjo haifai kipindi Dr. Magufuli akiwa hai, lakini baada ya kuwa ameuliwa wanasema chanjo inafaa.

kwa wananchi vichaa ni wale wote waliochanja.
 
Unamkuta mtu anaipinga CHANJO dhidi ya CORONA kwa kigezo kuwa zinatoka ULAYA kwa mabeberu....huku kila siku akimeza TEMBE DHIDI YA VIRUSI VYA UKIMWI....sasa sijui hizo tembe zinatengenezwa Lushoto Tanga?!!! 🤣
Mimi napinga chanjo ya Corona kwa ufanisi wake mdogo! Haina maana kupoteza muda wangu kuchanja chanjo ambayo haitanisaidia kunikinga na hayo maradhi kwa 100%!

Huku ni kupotezeana tu muda. Bora niendelee na huu utaratibu wangu wa kuchukua tahadhari.
 
Mimi napinga chanjo ya Corona kwa ufanisi wake mdogo! Haina maana kupoteza muda wangu kuchanja chanjo ambayo haitanisaidia kunikinga na hayo maradhi kwa 100%!

Huku ni kupotezeana tu muda. Bora niendelee na huu utaratibu wangu wa kuchukua tahadhari.
Iko hivi mkuu.....

Kwa hiyo pamoja na kupewa chanjo mathalani dhidi ya TETANUS ndiyo usichukue tena tahadhari?!! 😲😲

Watoto wadogo huwa wanachanjwa chanjo dhidi ya KIFUA KIKUU....je huwa hawaugui huo ugonjwa?!!!
 
Iko hivi mkuu.....

Kwa hiyo pamoja na kupewa chanjo mathalani dhidi ya TETANUS ndiyo usichukue tena tahadhari?!! 😲😲

Watoto wadogo huwa wanachanjwa chanjo dhidi ya KIFUA KIKUU....je huwa hawaugui huo ugonjwa?!!!
Tetenasi ya wapi bhana! Sisi wenzako mbona ni mara nyingi tumekatwa na chupa, vyuma chakavu, kuchomwa na misumari kwa bahati mbaya, nk.

Tumeishia kuweka tu mafuta ya taa au spirit, na maisha yanaendelea. Usiishi kwa kuriri mkuu. Hii chanjo ya Corona mmeingizwa chaka na Mabeberu, ili biashara za makampuni yao zipige hela.
 
Upo sahihi kabisa! Covid ni sayansi! Chanjo ni sayansi! Lakini utakuta kila mtu anajifanya kujua wakati asprini tu hajui kuigawa wala kuitengeneza!

Yaani watu wanazungumzia suala muhimu la chanjo kama wanavyozungumzia timu zao za Ulaya wasizozijua vizuri!
Watu wa hivyo kama siyo vichaa basi ni wendawazimu!!
Utawala wa awamu ya 5 uliendesha propaganda hasi dhidi ya chanjo ambayo mpaka Leo bado ipo vichwani mwa raia.
 
Mkuu ahsante kwa bandiko zuri la kufikirisha, kizuri zaidi umeeleza jinsi ambavyo mtu anawezakuwa na matatizo ya afya ya akili (kichaa) na asiokote makopo, akawa anaonekana mtanashati na bado isimuondoe kwenye kundi la vichaa.

Lakini napingana na wewe kwa kutumia hoja ya chanjo kama kigezo cha ukichaa na afya bora ya akili.

Ni sawa na kusema kati ya hizi timu mbili Simba na Yanga, ukiwa Yanga au Simba afya ya akili yako ina mushkeli.

Au kutumia dini ( madhehebu) kwamva ukiwa mkristo au muislam akili ina tatizo.

Ukitumia kigezo cha chanjo inakua umejibana kwenye eneo dogo sana lusilotosheleza kuhitimisha uzima au upungufu wa afya ya akili.

Hapo tutazalisha swali lingine, mtu anaweza kuwa na ukichaa kwenye suala la chanjo pekee na akawa genious mambo mengine?

Huo ukichaa una maeneo au afya ya akili inapokua mbovu inasthiri maamuzi na mambo yote anayofanya mtu?

Mwingine anaweza kyamua kigezo cha ajira kwamba ni ukichaa, kwamva kutokuajiriwa inaonyesha matumizi ya akili na kuajiriwa ni ukichaa.

Hali kadhalika mwingine ataenda mvali zaidi kwamba kujenga au kutokujenga inafanya wahusika kuwa kwenye kundi la ukichaa au akili yenye afya.

Ni hadi pale utakapomsikiliza kila mmoja atoe sababu zake kwanini yeye anapendelea kuajiriwa au kutokuajiriwa, maelezo yake yatafanya uone kama yana mantiki au la.

Kwa muktadha wa bandiko lako, mtu mwenye tatizo la akili akienda kuchanjwa anaodoka kwenye hilo kundi kisha amechanjwa?

Kuna mtu ukimuuliza kati ya kuishi na kufa bora nini, atakwambia kwa hali yake angetamani afe jana, ukipata kumsikiliza unaweza kujikuta unaenda kumnunulua sumu kwamba yuko sahihi.

Binafsi nakubali watu wengi sana wana matatizo ya akili sema madhara ndio yanatofautiana kiwango.

Ukiongeza na haya mambo ya tozo, utafiti ukirudiwa unaweza kukuta wenye shida ya akili wameongezeka.

Kutumia kigezo cha chanjo ya corona kupima afya ya akili inaweza isitoe picha halisi ya tatizo.
 
Hivyo vyote havina tija yoyote ile kwangu. Nguvu ninazo, na pia najitahidi kucheza viwanja salama.

Labda itokee chanjo ya kuongeza miaka ya kuishi hapa duniani! Hapo nitachanja. Maana natamani niishi miaka mingi ili nije kula matunda ya kazi zangu nizifanyazo sasa.
Duuh; naona umedhihirisha kuwa wewe ni kichaa!
Ili uishi miaka mingi unahitaji immunity. Na kazi ya chanjo ni kuboost immunity yako dhidi ya vimelea vya maradhi!
 
Ni sawa na kusema kati ya hizi timu mbili Simba na Yanga, ukiwa Yanga au Simba afya ya akili yako ina mushkeli.

Au kutumia dini ( madhehebu) kwamva ukiwa mkristo au muislam akili ina tatizo.
Mkuu hiyo mifano uliyoitoa ni viashiria vikubwa sana ya ukichaa. Mitaani huku wengi ni vichaa kisa dini. Wengine ni vichaa kisa Simba, Yanga na zile timu zao za Ulaya wasizozijua vizuri!
Tafuta kwanza maana ya ukichaa utakubaliana na mimi!
 
Back
Top Bottom