kwa Wazo alilotoa muheshimiwa Yona ni la kuzingatiwa sana, isje ikwa kama wimbo wa Remmy mAMBO KWA SOKSI, ambao ulipigwa marufuku zama zile na kwa sasa kinachozungumziwa ni mambo kwa soksi kwa asilimia 100.
Muheshimiwa ana wazo la msingi na mimi namuunga mkono katika hili, na tena si kuwekewa alama tu na hata wale ambao wanavirusi vya ukimwi wanaoenda nchi za nje ni vema wakajulikana katika nchi waendazo ili kudhibiti maambukizo ya ukimwi,
Tatizo watu wanaambukiza virusi kwa makusudi na kwa kudhamiria, nakumbuka kauli waliyoitoa waathirika kipindi kile kuishinikiza serikali iwape chakula walitishia 'kuambukiza virusi kwa makusudi' na pia wametishia pia 'kuacha kutumia dawa za kupunguza makali ya virus', hii ni hatari zaidi kuliko kuwekewa alama.
kinachoniogofya zaidi ni hivi vitisho vyao, kwani mtu awazavyo ndivyo alivyo', wanawaza kuua raia wengine wasio na hatia, wanawaza kuua watu wengi zaidi kwa kusababisha 'resistance' ya dawa.
Nawaunga mkono India, dunia imekuwa ndogo sana, mnakumbuka mfano wa yule gay 'mhudumu wa kwenye ndege' alivyowaambukiza watu kadhaa (new type carpos sarcoma)?