Late Sedekia kumbe alichukuliwa kimzimu

Late Sedekia kumbe alichukuliwa kimzimu

Haya bwana, atuelekeze namna ya kumrudisha tena kama amemuona alipo. Lakini Mwakasege sio Mchungaji. Longolongo za watu hizo na yaonyesha wapinga Kristo wamejaa mitaani.


Hata yeye mwenyewe huwa anasema ivyo mbele ya kadamnasi, na huwa anasema kabisa yeye anamchungaji wake na huwa anaenda ibadani kabisa.
Yeye huwa anajiita mwalimu, na si mchungaji.
 
Hata mimi nimeckiliza hicho kipindi hakusema muimbaji wake wala hakusema kasafiri naye alisema huyo mchungaji alitakiwa kumtoa muimbaji wa injili lakini hakusema maswala ya kusafiri
 
Hahah!!!

Sasa mmenye ina maana na hao jamaa wa RFA wataenda kuzimu kufuatilia kama kweli huyo muimbaji yupo huko?

Au labda niambie mbinu mujarabu wanaoitumia kujiridhisha.

Ha Ha Ha Ha Jamaa alisema kwa aliua wazazi wake wote na ndugu zake na kumbakisha m1 tu,kuna vitu vya uhalisia uwa wanafatilia lakini vya kuzimu sidhani,wana-investigate hivi tangible.
 
MWALIMU MWAKASEGE ATOA USHUHUDA JUU YA KIFO CHA FANUELI SEDEKIA

Mwalimu Christopher Mwakasege
ametoa ushuhuda huo katika semina
inayoendelea sasa katika viwanja vya
Furahisha jijini Mwanza Semina hiyo
yenye somo linaloitwa namna
ambavyo Roho Mtakatifu awezavyo
kukusaidia ili upokee kile
unachokiomba imeanza tar
19-07-2011 na inatazamiwa kuisha tar
23-07-2011.
Alisema Roho mtakatifu akwambiavyo
omba hiyo haina MJADALA ni kuingia
kwenye maombi mpaka upate
unachokiomba kwa kuwa gharama ya
kuingia kwenye maombi ili kupata
ulichotakiwa kukipata ni ndogo kuliko
gharama ya kukosa kile ulichoambiwa
ukipate katika Maombi hayo.
Roho mtakatifu anapokupa mzigo wa
kuombea jambo anakupa na muda
ukizembea muda huo ukipita
kinakuwa ni kiporo, na kiporo
kinaweza kikalika na kipo ambacho
hakiliki. .
“Tulipoenda Israel na Fanuel Sedekia
kisha akaanza kuumwa madaktari
waliniambia ubongo wake kwa asilimia
tisini haufanyi kazi. Lakini walishangaa
kwa nini kila mara niko pale Hospitali
wakasema kwa nini usikae tu Hotelini
kisha ukawa unapiga simu kuulizia hali
ya Mgonjwa? Wao hawakujua kwa nini
naenda pale kwa kuwa suala la kupiga
simu tu sio tatizo ningeweza kurudi
Arusha kisha nikawa napiga simu.
Suala hapa ni kuwa nilikuwa naenda
kila mara kwa ajili ya kumfanyia
maombi, nilikuwa nakaa kandokando
ya Bahari ya Galilaya nafanya maombi
juu ya Sedikia kwa masaa sita nikitoka
hapo nasikia upako wa ajabu sana
kIsha napanda Taxi kuelekea Hospitali.
Nikifika Hospitali madactari na watu wa
ICU walikuwa washanifahamu hivyo
naenda moja kwa moja kwenye
chumba cha nguo nabadili nguo kIsha
naingia ICU alikolazwa.
Nikifika nambana Mungu kwa maswali
Mengi namuuliza Sedekia, hivi
unaongea nini na Yesu muda wote huo
si urudi? na kisha namuuliza Yesu, hivi
Yesu si unafahamu kuwa Sedekia
anamke ukimchukua mkewe
atamuachia nani? Kisha baada ya
maneno hayo naweka mkono juu
yake. Nilipokuwa nikiweka mkono juu
yake ghafla upako wote unakuwa
kama umenyonywa.
Baada ya hapo narudi hotelini naanza
tena kumuuliza Mungu hivi Mungu
kama basi husikii maombi yangu sikia
maombi ya watanzania kwa kuwa saa
hiyo nilijua watanzania wengi
wanamuombea Sedekia.
Inafikia wakati nakata tamaa lakini
ndani yangu najisemea Mwakasege
haiwezekani jitie moyo kisha nabadili
aina ya maombi, kwa kuwa nilikuwa na
nguo zake pamoja na passport yake
nikawa naviweka kati kisha nikawa
naanza maombi ya Yeriko, nikawa niko
hotelini usiku nazunguka nguo zake
na paspot yake huku nikifanya
maombi.
Taratibu Mungu akaanza kuniambia
kuwa sedekia harudi, Kipidi hicho mimi
na familia yangu tulikuwa tumepanga
kwenda kupumzika nchini Uingereza
wakati wa skukuu ya Chrismass, na
booking mpaka ya Hotel tulikuwa
tumeshafanya, na watoto wote wako
nyumbani wakijiuliza tunaendaje
kupumzika wakati Sedekia anaumwa?
Chrismass ikapita na mwaka mpya pia
kisha Sedekia akafariki.
Baada ya kifo hicho sikuchoka nkarudi
tena kwa Mungu nikamuuliza kwa nini
Mungu umeamua kumchukua Sedekia
mikononi mwangu? Mungu alinijibu
vitu ambavyo siwezi kuvisema hapa.
Kila siku mimi ni mgeni katika maombi
namhitaji ROHO anifundishe kwa upya
kwa kuwa sijui vita gani ninakwenda
kupambana nayo, Mungu anabaki
kuwa Mungu kwa kuwa hufanya
atakavyo”


Source:Hosanna Inc: Mwl Christopher Mwakasege atoa shuhuda juu ya kifo Fanuel Sedekia
 
Ngoja niendelee kufuatilia mazishi ya Mandela live najifunza vitu.
 
Tangu lini Mwakasege ni Mchungaji? Hajawahi kuwa mchungaji wala kuusomea japo alishauliwa akasema yeye wito wake ni Mwalimu.,Kwa waumin wakiluther tunaelewa hilo ili mtu awe mchungaji lazima akasome.

Omba radhi Mkuu kwa kupotosha watu.
1.Mwakasege ni mwalimu na sio mchungaji
2.Kipindi hicho cha rfa hajatajwa sedekia

Ni dhambi kubwa sana kuwahusisha watumish wa Mungu kwenye laana kama hii tena pasipo na uthibitisho.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Acheni kumsema vibaya mtumishi wa Mungu. Huyo aliyeko redioni abanwe alete vielelezo. Ikiwezekana apewe video kamera kabisa akatuletee uthibitisho na ushahidi juu
 
Tangu lini Mwakasege ni Mchungaji? Hajawahi kuwa mchungaji wala kuusomea japo alishauliwa akasema yeye wito wake ni Mwalimu.,Kwa waumin wakiluther tunaelewa hilo ili mtu awe mchungaji lazima akasome.

Omba radhi Mkuu kwa kupotosha watu.
1.Mwakasege ni mwalimu na sio mchungaji
2.Kipindi hicho cha rfa hajatajwa sedekia

Ni dhambi kubwa sana kuwahusisha watumish wa Mungu kwenye laana kama hii tena pasipo na uthibitisho.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Watanzania tunapenda bla bla sana,namba ya simu ipo ya jamaa mpigie ukate mzizi wa fitina,muimbaji gani wa injili aliyefia nje ya nchi akiwa pamoja na mchungaji wake? Hayo maelezo sijayatoa mimi,kayatoa jamaa aliyekuwa anahojiwa,mpigie jamaa katoa namba ya simu!
 
Acheni kumsema vibaya mtumishi wa Mungu. Huyo aliyeko redioni abanwe alete vielelezo. Ikiwezekana apewe video kamera kabisa akatuletee uthibitisho na ushahidi juu

We ndio umeongea ukweli jamaa abanwe aeleze ukweli halisi.
 
Hata mimi nimeckiliza hicho kipindi hakusema muimbaji wake wala hakusema kasafiri naye alisema huyo mchungaji alitakiwa kumtoa muimbaji wa injili lakini hakusema maswala ya kusafiri

Kipindi kipo recorded kasema mchungaji alimtoa muimbaji injili na walisafiri,kama kuna mtu kakirekodi akiweke usikilize vizuri,mie ni mfatiliaji sana wa kipindi hiki,vipo hadi vingine nimerekodi.
 
RFA hawafai, kunakipindi jamaa alitoa simulizi kuwa mke wake wa zamani alikuwa jini! Kumbe uongo mke alikuwa anaishi Igoma akaenda kukanusha kwenye radio free africa. Hizo ni story kama za akina Shigongo. Watanzania yapuuzeni hayo ni uongo mtupu.
 
Acheni kumsema vibaya mtumishi wa Mungu. Huyo aliyeko redioni abanwe alete vielelezo. Ikiwezekana apewe video kamera kabisa akatuletee uthibitisho na ushahidi juu
Mtumishi wa mungu wapi bhana? Huyo ni mfuasi wa Shetani tu, watumishi wa mungu walisha pitaga zamani nazama zao hazipo tena. Ukimuona mtu anajiita mtumishi wa mungu jua anamtumikia Lussifer huyo.
 
Duh! Kumbe hawa wachungaji (sio wachunga mifugo) niwatu hatari sana, inabidi waepukwe.
 
Mkubwa hii sio siasa,nakumbuka kwamba late sedekia alifariki nje ya nchi akiwa na mchungaji(((Mwakasege source JF members))),nakama wewe ni mfuatiliaji wa kipindi cha sintosahau cha RFA story zake ni za kweli maana wana-investigate kwanza then wakishajidhihirishia ukweli ndio wanakuhoji,na jamaa amesema kabisa mchungaji alimtoa muimbaji wake na alichokifanya ni kutumia mbinu ya kusafiri nae!! Mwakasege vipi tena mbona hvyo?

kaka unaamin kua kipindi cha sitosahau kinakua invesigated,na nan?wap hyo inafanyika kaka,sitoshau n historia ya mtu binafsi ya huko nyuma hata miaka 70 iliyopta sasa nan anainvestigate historia ya mtu pale RFA?HZO STORY ZOTE NI ZA KUTUNGA KM ZA SHGONGO,KWA MFANO KM UNAKUMBUKA MIAKA KM 4 AU 5 ILIYOPTA KUNA JAMAA ALIKUA AKITOA STORY YA UCHAWI HUKO SHY ENEO LINAITWA GAMBOSHI,KUA ALIENDA HUKO AKAKUTANA NA UCHAWI,NA MAMBO KM HAYO,HYO STORY NI YA KUTUNGA NA ALIITOA BRO WANGU WALA HUKO SHY HAPAJUI,NI STORY ZA KIZAMANI SANA TULIZOKUA TUNAHADITHIWA NA BIBI YEYE AKAIMODERNISE NA KUISEMA RFA,NA HADI SASA NAISH NAE HUYO MCHAWI FEKI WA GAMBOSH,USIAMIN KILA KINACHOSEMWA KWENYE RADIO.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom