Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..

Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..

Ukifika hadi bia ya nne hujaongea hata sentensi 5 za kingereza inabidi ukaombe chenchi yako urudi nyumbani tu
 
Sema no "pombe" 2018
no-drinking.gif

Naunga mkono hoja.
 
Bia ya saba
[emoji481] [emoji481] [emoji481] [emoji481] [emoji481] [emoji481] [emoji481]
Maandalizi ya kupakiwa kwenye toroli
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]aseee JF raha sana
 
bia ya 7 hata yule ambaye hajasoma MEMKWA hujikuta akiongea kiingereza tena kwa kujiamini sana utadhani katoka kwa malkia elizabeth
[emoji15][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]memkwa
 
Kwa wanywaji wazuri wa bia,

chupa ya kwanza [emoji481] huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo… Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

chupa ya pili [emoji481][emoji481] kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi….

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Bia ya tatu [emoji481][emoji481][emoji481] huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana…. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza…..

Bia ya nne [emoji481][emoji481][emoji481][emoji481] huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia….. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano [emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481] ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu……na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali’

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita [emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481] na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Wajumbe wenzangu wa kikao naomba karibuni bier ya 7 na kuendelea
Art of creation [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hahahaha we jamaa hatari sana,huu ni ukweli mtupu,vipi kuhusu wazee wa nyagi?
kama nikachupa kale kadogo ukikamaliza tu unahsi uso ni mzito na unataman kila mda kujifuta futa unahc kama ganzi. usoni na huambatana na mambo yote aliyo nayo aliyekunywa bia tao kichupa chapili kikiisha unaona kujiamini nakutaman kujionyesha na hapo ndio simu inatumika kupigia watu na aliye karibu kumualika cha tatu maranying huambatana na mambo ambayo kesho ukiyakumbuka lazima ujisie vibaya
 
Hii comment yako huwa nawauliza sana wanaodai namalizia pesa baa kwamba za kwao wanamalizia wapi?

Anyway nifafanulie avatar yako maana naona watu wanapeana kwa miguu
Mkuu hiyo Avatar iangalie vizuri utaielewa.kuna mtu anazungukwa hapo.
 
Kwa wanywaji wazuri wa bia,

Mkuu mie nina mtazamo tofauti kuhusu unywaji bia baa, kadiri unapozidi kunywa

[emoji481]
Unaaangalia wahudumu wa baa, na kushangaa kwa nini hii baa ina wahudumu wazee kiasi hiki na uniform ambazo haziwapendezi kabisa
[emoji481][emoji481]
Unaanza kuona kwamba kumbe zile uniform zao sio mbaya kama ulivyofikiria mwanzoni
[emoji481][emoji481][emoji481]
Unaanza kuona kwamba actually kuna baadhi ya wahudumu uniform zao zinawapendeza sana!
[emoji481][emoji481][emoji481][emoji481]
Unaanza kuhisi kwamba ile shift ya wahudumu wa baa uliyoikuta ulipoingia baa imeondoka imeingia shift nyingine ambayo wahudumu ni wazuri sana kulinganisha na shift ya kwanza
[emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481]
Unashangaa kwamba baadhi ya wahudumu wa hii baa ni warembo kweli na unashangaa kwa nini hii baa inaleta wahudumu warembo pale saa za kufunga baa zinapokaribia!
[emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481]
Unagundua kuna mhudumu mmoja wa baa ambaye ni tofauti kabisa na wengine na ni mrembo kuliko au Miss Tanzania!
[emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481]
Unafanya uamuzi kwamba huyu mhudumu wa baa aliye mrembo kuliko Miss Tanzania ambaye hakuwapo ulipoingia hii baa lazima uondoke naye kwa udi na uvumba, hata akidai pesa nyingi kiasi gani!

..........kesho yake asubuhi............

unaamka na unapomwona mhudumu wa baa uliyeondoka naye usiku amelala pembeni yako unapiga yowe kwa nguvu nooooooooooooooo!!!
 
Ulichosahau mkuu ni kwamba mtu akishalewa huwa anaongea ukweli tu yaani anaweza kutoa mpk siri zake [emoji2][emoji23][emoji23]
In wine there is wisdom, in beer there is freedoms , in water there is bacteria.....BENJAMIN FRANKLIN
 
Sijawahi kunywa bia hivyo sijui lolote kwenye hili, nimesoma nabaki nacheka tu
Anza Leo hujachelewa ni chupa zinazokufanya kujua kuongea kiingereza vizuri tofauti ni mwanzo. Lakini ni kwa muda tu chaji ikiisha ubora wa lugha hupungua
 
Yan bia 6 me ndo naanzaga kushtukaa nkifika ya 9 napoa kabisaa ya 12 natafutaa kitanda na siwez kuongea. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sinaga mafujo wala kubishana sababu kupiga kelele kunazidisha kulewaa
 
Watu kama wewe wameshanipa ushauri sana wa kupiga vyombo ila msimamo ni hapana vinywaji laini vinatosha
Kama hujawahi tumia sikushauri kujaribu maana utajutaa sijajua umri wako ila kuanzia ukubwan pombe ni hatari. Me nakumbuka nmeanza darasa 3 rasm ile unatoka na mzazi anakutilia kichelee kwenye glass [emoji23][emoji23]
 
vp kuhusu sie tunaokunywa konyagi,valuer,magic moment..embu tupe mchanganuo[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3]
Nkiwa nimeshibaa vyema maji shazi labda tuwe nakasafar karefu kwenye ka private k vant kubwa inakataa chap natafuta na kadogo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom