Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..

Ladha ya bia ya 1 hadi ya 6..

Pombe bwana hivi jaman mi kuna siku hua nalewa mpaka inabaki mb3 yaan hizo mb 3 ni za kukufikisha hom na ukifika tu kesho hukumbuki hata ulifikaje hom bt ndio umefika na milango unakuta umefunga bt hukumbuki umerudije hahahah
Najiulizaga sana maana unakuta mtu yupo nzwiii yaani chakarliii lakini nyumbani anafika
 
Kuna jamaa yangu yeye akifikisha bia ya tano na kuendelea anakumbuka ndugu zake waliokufa,hicho kilio atakachoangusha hapo ni hatari,baa nzima macho kodo kwetu lol.
 
Haa haa haaa
Mimi nikifika bia ya 3 hua nakua na mawazo na mipango mikubwa sana ya kimaisha.

Ila nikifika ya 7 hua naanza kuwaza papuchi tu.
Ha ha ha ha ha we jamaa hatari,bia ya 7 inakimbila kichwa cha chini.
 
Jaman bia ipewe heshima ake .....
Nikinywaga safari ikifik ya 3 nikijishika usoni naona sura kama sio yangu ....
Sema bia inanifanyaga niongee kiingeleza kizurii sana kiasi kwamba hata IQ yangu inaongezeka ahahaha
Sura nzito na kama ganzi inaanza ukipiga zaidi unaanza ona bia kama soda tamu mnoo
 
Serengeti light aka henken mayai yabarid me nikieka mdomon mara mbil kameishaa ilaa nikatamu kako Kama kameungua unguu hvii unaeza jikuta umekausha cret sema kukojoa kilaa saaa
Kwhyo Haileweshi Hadi Kuzima
 
Kwa wanywaji wazuri wa bia,

chupa ya kwanza [emoji481] huwa haileti hisia yoyote. Mnywaji humaliza chupa hiyo bila kuona matokeo yoyote zaidi ya kupoza koo… Na mara nyingi huwa mkimya, pengine huwa anasoma gazeti lake au kwa siku hizi anawasiliana na ndugu na jamaa kupitia simu yake.

chupa ya pili [emoji481][emoji481] kimsingi ndipo mazungumzo ya awali na wanywaji jirani huanza na haya huwa mazungumzo ya busara, yakihusu muelekeo wa ligi mbalimbali, siasa, idadi za ajali na kadhalika na wakati huu hata takwimu hutolewa zilizo sahihi….

Mtu anaweza kukutajia wachezaji wote wa ligi daraja la tatu la huko Ujerumani bila kukosea, hata idadi ya wachezaji wa Yanga bila kukosea.. Ila wakati huu kama unaanzisha mashindano ya kucheua ni wakati mzuri kwani bia ya pili huongeza hisia za kucheua.

Bia ya tatu [emoji481][emoji481][emoji481] huanza kumfanya mnywaji aanze kusikia furaha na pia huu huwa wakati ambapo karanga na korosho huliwa sana…. Pamoja na mazungumzo kuhusu mpira na siasa, ghafla mazungumzo kuhusu michepuko huanza kujitokeza…..

Bia ya nne [emoji481][emoji481][emoji481][emoji481] huanza kusababisha masikio yaanze kupoteza nguvu za kusikia kwani utaona mnywaji ghafla amepandisha sauti, na ukijumlisha na kuwa baa zetu huwa na muziki una kelele utadhani waliopo wote wana matatizo ya kusikia….. bia hii humsaidia kuongea kwa nguvu kushindana na kelele za muziki.

Bia ya tano [emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481] ni hatari kidogo kwani ukiinuka kwenda chooni mara nyingi unarudi hujafunga zipu……na kipindi hiki ni kibaya kwa wanywaji wa kike maana unaweza kumkuta akienda chooni akijiangalia kwenye kioo anaanza kulia peke yake na kulalamika; ‘Mi sipendwi mpaka leo sijaolewa’ au ‘ Mume wangu sijui yukoje hanijali’

Japokuwa lazima isemwe ukweli ukifikisha bia hii, maisha ni raha sana unaweza ukaanzisha shoo ya kukata mauno katikati ya baa na kudai wewe ni mkali kuliko Shilole.

Kuanzia bia ya sita [emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481][emoji481] na kuendelea, chochote utakachosema au kufanya ni wazi kesho yake asubuhi utajilaumu sana.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Wajumbe wenzangu wa kikao naomba karibuni bier ya 7 na kuendelea
Uzoefu unaongea,hatari sana.........!
 
HIVI WADAU CASTLE LITE,NDOVU NA SERENGETI ZINALEWESHA KWELI ? MIE NISHAZOEA NGUMU KUMEZA LAGER
Miye n mnywaji wa konyagi!yaani nkinywa castle lite 9 ndio naiskia/nai-feel kwa kweli.hizo bia ni nyepesi mno!zanijaza tumbo tuh!na hivi mlaji ovyo ovyo!bia siwezi!
 
Hahaaaa.., hivi ni ya ngapi vile now.., hata sikumbuki.., mtanikumbusha kukikuchaaa!!
 
Back
Top Bottom