Kwenu wakulima wa Tikiti: Je hii hesabu ni sahihi kwamba eka 1 unapata milioni 8 net profit?

Ramon Abbas

JF-Expert Member
May 4, 2021
1,964
3,900
Nimekutana na hii post huko mitandaoni, sijawahi kulima tikiti wala kupiga hesabu za idadi ya miche kwa ekari moja.

Naomba tufahamishane kama kilichoandikwa na huyu ndugu yetu ni sahihi ama lah kuhusu upatikanaje wa faida ya tikiti kwa eka 1.

FB_IMG_1634362025066.jpg
 
nakuheshim sana mkuu kuna mahala udhanisaidia, hebu tujikite zaidi kwenye mada maana hapa hatuna shamba
Mkuu sidhani kama nimekwambia vibaya labda umelichukulia vibaya...
Ukiingia shamba utapata jibu kamili wa maswali yako.

Nimewahi kulima matikiti Simiyu,kilimo cha kumwagilia.
Nililima mara ya kwanza,kijana akaniangusha sikupata kabisaa(stori ndefu)
Nikalima mara ya pili ilikua ni pembeni ya mto,sijui mvua ilinyesha wapi ,mto ulijaa maji mpaka ukatema miche yote ikasombwa..

Bado sikukata tamaa

Nikaenda kulima msowelo morogoro,Japo changamoto ni nyingi ila nilipatapata kwa kiasi chake changamoto kubwa ikaja kwenye soko...
 
Utamu wa Ngoma ingia uicheze mwenyewe, Usisubiri kusimuliwa. Mtu kama una milioni zako mbili fanya kile kitu unachotamani kukifanya kutoka Moyoni mwako hicho ndicho. Siyo kusikiliza story za kufanikiwa ghafla haipo hiyo.Milele yote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usijaribu kuingia na hiyo mentality na huo uhakika wa mil 8 utaumia na kuchukia watu.....

Uzuri kuna rafiki angu alilima tikiti nikiwa nae bega kwa bega.....ni hiyohiyo heka 1 tena alilima kwa kumwagilia Dodoma pale.....

Kwanza aliset shamba vizuri sana na kufunga mipira ile ya maji vizuri (mipira ile inafanya drop irrigation kama sijakosea), akazungushia uzio vizuri sana na kuhakikisha supply ya maji ni ya kutosha tena yanatoka bombani na anamatank yake makubwa 10 na muda wote yanejaa maji......

mbegu zikapandwa vizuri, baada ya kupanda mbegu, ikaja shida ya kunguru kufukua mbegu, tukatafuta ile mikanda ya zamani tukatoa ile kama ramani ya ndani sauti yake inafukuza wanyama au ndege ikifunga......

limeisha hilo mbegu zikaanza kutoa majani vizuri kabisa....panzi wakaja wakawa wanajificha chini ya majani wanakula focal point za muhimu za majani.....tukaanza ona majani yanasinyaa, hapo tuliishapiga dawa ya kwanza ila tukapiga dawa nyingine kidogo ikasaidia.....

Mbegu zikaota matikiti yakaanza ota vizuri tu, shida ikaja matikiti mengi yakadumaa hivi, hadi yanakomaa yakawa madogo sana..... Wiki 2 kabla ya kuvuna, wakaibuka wezi wanaiba hadi 4 kwa siku, tukatoa uangalizi yakavunwa yakiwa machache sana hayazidi 500 .....

Mwisho wateja wakawa hamna, ikabidi watu wakopeshwe na majirani wakopeshwe vizuri zaidi .....wadeni wasiozidi 50 ndio walilipia......biashara ikawa imeleta hasara

Huyo jamaa amesema (ukaamua kuuza) hamna mtu anaamua kuuza bei fulani bali dalali ndio anakuamulia bei, maana masokoni bila madalali mzigo wako utakuharibikia.....

Hivyo hiyo hesabu haina uhalisia kabisa nimeshuhudia.
 
Inawezekana lakini kulithibitisha hilo,hakikisha shamba lako lina miundo mbinu ya umwagiliaji na si kutegemea mvua;pia mbolea,dawa za kuua wadudu,pamoja na ulinzi wa kutosha. Tumia hela kupata hela
 
Usijaribu kuingia na hiyo mentality na huo uhakika wa mil 8 utaumia na kuchukia watu.....

Uzuri kuna rafiki angu alilima tikiti nikiwa nae bega kwa bega.....ni hiyohiyo heka 1 tena alilima kwa kumwagilia Dodoma pale.....

Kwanza aliset shamba vizuri sana na kufunga mipira ile ya maji vizuri (mipira ile inafanya drop irrigation kama sijakosea), akazungushia uzio vizuri sana na kuhakikisha supply ya maji ni ya kutosha tena yanatoka bombani na anamatank yake makubwa 10 na muda wote yanejaa maji......

mbegu zikapandwa vizuri, baada ya kupanda mbegu, ikaja shida ya kunguru kufukua mbegu, tukatafuta ile mikanda ya zamani tukatoa ile kama ramani ya ndani sauti yake inafukuza wanyama au ndege ikifunga......

limeisha hilo mbegu zikaanza kutoa majani vizuri kabisa....panzi wakaja wakawa wanajificha chini ya majani wanakula focal point za muhimu za majani.....tukaanza ona majani yanasinyaa, hapo tuliishapiga dawa ya kwanza ila tukapiga dawa nyingine kidogo ikasaidia.....

Mbegu zikaota matikiti yakaanza ota vizuri tu, shida ikaja matikiti mengi yakadumaa hivi, hadi yanakomaa yakawa madogo sana..... Wiki 2 kabla ya kuvuna, wakaibuka wezi wanaiba hadi 4 kwa siku, tukatoa uangalizi yakavunwa yakiwa machache sana hayazidi 500 .....

Mwisho wateja wakawa hamna, ikabidi watu wakopeshwe na majirani wakopeshwe vizuri zaidi .....wadeni wasiozidi 50 ndio walilipia......biashara ikawa imeleta hasara

Huyo jamaa amesema (ukaamua kuuza) hamna mtu anaamua kuuza bei fulani bali dalali ndio anakuamulia bei, maana masokoni bila madalali mzigo wako utakuharibikia.....

Hivyo hiyo hesabu haina uhalisia kabisa nimeshuhudia.
Aisee kilimo ni kazi ngumu! Kinahitaji kujifunza sana na kupata uzoefu!
 
Mkuu huyo uliyemscreenshot siyo MKULIMA bali ni Motivational Speaker.

Ukihitaji UKWELI /majibu /ushauri basi mtafute mkulima.

Haina maana kumuomba fundi simu ushauri wa biashara ya Madini... utafeli kwa kupata taarifa zisizo sahihi!
 
Back
Top Bottom