Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 52,858
- 131,520
Kipofu wa kiume ni ruksa kuswali pamoja na wanawake?Na hapo ndipo mzizi ulipo mkuu, kuona na kupata mfadhaiko, kutoka kwenye dhana nzima ya kufanya ibada na Mungu wako.
Kipofu wa kiume ni ruksa kuswali pamoja na wanawake?Na hapo ndipo mzizi ulipo mkuu, kuona na kupata mfadhaiko, kutoka kwenye dhana nzima ya kufanya ibada na Mungu wako.
hapo sasa umenielewa kabisaUyahudi na Uislamu unafanana kwa kiasi kikubwa(japo sielewi kwa nini Waarabu na Wayahudi huwa wanatwangana muda wote), hata hivyo Ukristo uko mbali sana na Uyahudi pamoja na Uislamu japo zote ni Abrahamic religions.
Tukianza na,
1. Uungu- Sehemu kubwa ya Ukristo wanaamini mungu wa nafsi tatu ambapo kwa Waislamu na Wayahudi wanaona ni upotovu.
2. Yesu Kristo- Ukristo umejengwa juu ya msingi wa kifo na kufufuka kwa Yesu Kristo, Waislamu wanasema Yesu hajafa na Wayahudi wanasema Masihi Kristo hajaja kabisa
3. Vyakula- Wakristo tofauti na Wasabato hawana Sheria za vyakula,
4.Ibada-Wakristo hawana Sheria za mwilini kuhusu Ibada kama za kutawadha, kusujudu n.k kama ilivyo kwa Waislamu na Wayahudi
5.Ndoa- Ukristo hauruhusu ndoa za mitaala
Nasikitikita kukwambia kuwa maandiko haya hapa chini ni agano la kale.. 😀 😀 😀 😀 😀Hakuna sheria za Kikristu zilivyo hivyo. Hapo itakuwa umesoma vitabu vya historia vilivyojaa Mila ,tamaduni na sheria za kiyahudi za again la kale. Hapa ndio watu wengi Huwa wanakwama . Maelekezo sahihi soma agano la kale kwani Yesu alikuwa kutenganisha mambo ya kitamaduni yaliyokuwepo kwenye agano la kale na ndio maana wayahudi walimuua kwa sababu aliwakosoa kwenye masheria kama haya. Agano kipya ndio mpango.mzima hata kitimoto na bia lakini tunashushia saaafi maana alikosoa zile Mila za walawi za kutoka kula mdudu na lutakasa vyakula vyote
Mno bwasheeKama unajifunika kwa hijab, niqab au burka ina maanisha sio rahisi umbile la mwili wako wako kuonekana kwa hiyo hata matamanio ya wanaume yanapungua na inakuwa rahisi kujichanganya bila kuamsha hisia, japo ajabu pia ni kwamba kuna watu kama min -me anasema wanaovaa hivyo ndio huwa anawatamani zaidi!
Kustarehesha siyo heshima?Mwanamke katika Uislam ni kijakazi na chombo cha starehe hana heshima yoyote
Aloo🙌Katika dini zote dini ya kiislam ndio dini nzuri , bila kujalisha wanayoyasema ni pumba , ila ndio dini inayo mfaa mwanaume wenye akili timamu.
Unabisha ? Bisha kwa hojaAloo🙌
Nimezaliwa huko hiyo dini imejaa vitisho ubinafsi na ukandamizaji hasa kwa jinsia keUnabisha ? Bisha kwa hoja
Ukandamizaji upi ?Nimezaliwa huko hiyo dini imejaa vitisho ubinafsi na ukandamizaji hasa kwa jinsia ke
Huko mwanamke ni kama chombo fulani sitaki kusema sana mambo ya dini za watu ila hapana aiseeUkandamizaji upi ?
Sio kweli kuna wanawake wajanja tu ni waislam unataka kusema wewe ni mjanja zaidi yao ?Huko mwanamke ni kama chombo fulani sitaki kusema sana mambo ya dini za watu ila hapana aisee
Tabia za hovyo na za kishenzi za familia yako,usifanye kua ndio ikawa kua ndio tabia za watu wote wa dini hiyo,usihukumu dini yote kwa tabia za familia yako,Nimezaliwa huko hiyo dini imejaa vitisho ubinafsi na ukandamizaji hasa kwa jinsia ke
Yoda umepata majibu yako sasaMkuu swala hilo linaitwa Ikhtilat kwa lugha ya kiarabu..
sasa nini faida yake:
1. Kulinda Unyenyekevu (Khushui')
Unajua swala ya kiislamu inavyofanyika kuna kugusana baina ya vidole vya miguu na kuna kulinganisha mabega na zaidi kuna rukuu na sigda inayomtaka muumini kuinama na kuinuka na kuinamisha kichwa chini jambo ambalo kama utaswali na mwanamke pembeni linaweza kuondoa utulivu kwa kuamka matamanio na kukuondoa kwenye swala (unajua tena wenzetu wameumbwa na magnnetism)
2. Kuepuka Vishawishi (Fitna)
Uislamu unasisitiza kuzuia mazingira yanayoweza kuleta vishawishi kati ya jinsia mbili katika maeneo ya ibada. Kwa kutenga sehemu za kuswali, jamii inajenga mazingira ya heshima ambapo kila mmoja anaweza kuabudu kwa uhuru.
3. Sunnah
Wakati wa Mtume Muhammad (S.A.W), wanawake waliswali msikitini lakini walikuwa nyuma ya safu za wanaume. Mtume alisema kuwa safu bora kwa wanaume ni za mbele, na safu bora kwa wanawake (katika mazingira ya pamoja) ni za nyuma. Baadaye, kadiri idadi ya watu ilivyoongezeka, kuta au vyumba maalum viliwekwa kwa ajili ya urahisi na faragha zaidi.
SASA mkuu nakurudishia swali kuwa je kwenye biblia au tamaduni za zmani hakuna hiki kitu namaanisha kabla ya uislamu yaani hiki kitu ni kipya ???
hapana sio ktu kipya
Katika nyakati za Wana wa israel na hata baada ya hapo, Hekalu la Yerusalemu lilikuwa na sehemu maalum iitwayo "Ezrat Nashim (עֶזְרַת נָשִׁים)" Yaani Court of the Women.
Wanawake hawakuruhusiwa kuingia katika maeneo ya ndani yaliyotengwa kwa wanaume wa Kiisraeli au makuhani. Huu ulikuwa mgawanyo wa wazi wa kijinsia katika ibada.
Japo kwenye Katika Hekalu la Pili la Yerusalemu (Hekalu la Herode), hili lilikuwa eneo la nje ambapo Wayahudi wote (wanaume kwa wanawake) waliruhusiwa kuingia kwa ajili ya ibada za kawaida na kusikiliza mafundisho. ila wanawake hawakuruhusiwa kupita eneo hili kwenda ndani zaidi kuelekea madhabahuni (eneo lililoitwa Ezrat Yisrael ambalo lilikuwa maalum kwa wanaume tu).
Hadi leo, katika madhehebu ya kiorthodox ya Kiyahudi (ambayo yanafuata sheria za kale za Torati), wanaume na wanawake hukaa sehemu tofauti, mara nyingi zikitenganishwa na ukuta au pazia liitwalo Mechitza.
katika ukristo kwenye Mila za Kale Kwa karne nyingi, katika makanisa mengi ya kale (ikiwemo baadhi ya makanisa ya Orthodox na Katoliki ya Mashariki), wanaume walikaa upande mmoja wa kanisa na wanawake upande mwingine.
Ingawa Biblia haisemi waziwazi ila inasisitiza juu ya utaratibu na staha. Kwa mfano, katika 1 Wakorintho 14:34-35 na 1 Timotheo 2:11-12, kuna maelekezo yanayoweka mipaka ya ushiriki wa wanawake katika mazingira fulani ya ibada ya hadhara ili kudumisha utaratibu.
Ki ufupi Mgawanyo wa jinsia si jambo la kiislamu pekeeni utaratibu uliokuwepo katika dini zote za Ibrahimu (Uyahudi, Ukristo, na Uislamu) kwa lengo la kudumisha staha na heshima katika nyumba za ibada, ingawa Ukristo wa kisasa katika madhehebu mengi umeacha utaratibu huo.
Platinum member 😳Tabia za hovyo na za kishenzi za familia yako,usifanye kua ndio ikawa kua ndio tabia za watu wote wa dini hiyo,usihukumu dini yote kwa tabia za familia yako,
Yani hicho kifamilia chako cha hovyo ndio kikufanye uhukumu watu wote wa dini hiyo Dunia nzima?
Wapi nimesema mimi mjanja ?Sio kweli kuna wanawake wajanja tu ni waislam unataka kusema wewe ni mjanja zaidi yao ?
Kumwambia mtu ukweli ndio hua mnatafsiri kua ni hasira huko kwenu?Platinum member 😳
Kwanini una hasira kali just relax bro👍
Wapi nimesema ni kosa?Wapi nimesema mimi mjanja ?
Siku hizi JF ni kosa mtu kutoa mtazamo wake?