I feel good
JF-Expert Member
- Oct 21, 2016
- 1,694
- 2,987
Mbona Jibu unalijua halafu unauliza tena!!!Ni kwa nini katika Uislamu wanawake na wanaume hawachanganyikani katika chumba kimoja msikitini?
Mbona Jibu unalijua halafu unauliza tena!!!Ni kwa nini katika Uislamu wanawake na wanaume hawachanganyikani katika chumba kimoja msikitini?
wanakuwepo mkuu , hata kama ni kwa uchacheSijawahi mkuu, hata videos zote masheikh wakitoa mawaidha huwa naona waumini wanaosikiliza msikitini ni wanaume tu.
Maelezo ni mazuri ila yanaeleweka sana kama utaayaweka katika muktadha wa kibaiolojia lakini yanaacha maswali lukuki katika muktadha wa uthabiti wa imani katika kumudu majaribu.Mkuu swala hilo linaitwa Ikhtilat kwa lugha ya kiarabu..
sasa nini faida yake:
1. Kulinda Unyenyekevu (Khushui')
Unajua swala ya kiislamu inavyofanyika kuna kugusana baina ya vidole vya miguu na kuna kulinganisha mabega na zaidi kuna rukuu na sigda inayomtaka muumini kuinama na kuinuka na kuinamisha kichwa chini jambo ambalo kama utaswali na mwanamke pembeni linaweza kuondoa utulivu kwa kuamka matamanio na kukuondoa kwenye swala (unajua tena wenzetu wameumbwa na magnnetism)
2. Kuepuka Vishawishi (Fitna)
Uislamu unasisitiza kuzuia mazingira yanayoweza kuleta vishawishi kati ya jinsia mbili katika maeneo ya ibada. Kwa kutenga sehemu za kuswali, jamii inajenga mazingira ya heshima ambapo kila mmoja anaweza kuabudu kwa uhuru.
3. Sunnah
Wakati wa Mtume Muhammad (S.A.W), wanawake waliswali msikitini lakini walikuwa nyuma ya safu za wanaume. Mtume alisema kuwa safu bora kwa wanaume ni za mbele, na safu bora kwa wanawake (katika mazingira ya pamoja) ni za nyuma. Baadaye, kadiri idadi ya watu ilivyoongezeka, kuta au vyumba maalum viliwekwa kwa ajili ya urahisi na faragha zaidi.
SASA mkuu nakurudishia swali kuwa je kwenye biblia au tamaduni za zmani hakuna hiki kitu namaanisha kabla ya uislamu yaani hiki kitu ni kipya ???
hapana sio ktu kipya
Katika nyakati za Wana wa israel na hata baada ya hapo, Hekalu la Yerusalemu lilikuwa na sehemu maalum iitwayo "Ezrat Nashim (עֶזְרַת נָשִׁים)" Yaani Court of the Women.
Wanawake hawakuruhusiwa kuingia katika maeneo ya ndani yaliyotengwa kwa wanaume wa Kiisraeli au makuhani. Huu ulikuwa mgawanyo wa wazi wa kijinsia katika ibada.
Japo kwenye Katika Hekalu la Pili la Yerusalemu (Hekalu la Herode), hili lilikuwa eneo la nje ambapo Wayahudi wote (wanaume kwa wanawake) waliruhusiwa kuingia kwa ajili ya ibada za kawaida na kusikiliza mafundisho. ila wanawake hawakuruhusiwa kupita eneo hili kwenda ndani zaidi kuelekea madhabahuni (eneo lililoitwa Ezrat Yisrael ambalo lilikuwa maalum kwa wanaume tu).
Hadi leo, katika madhehebu ya kiorthodox ya Kiyahudi (ambayo yanafuata sheria za kale za Torati), wanaume na wanawake hukaa sehemu tofauti, mara nyingi zikitenganishwa na ukuta au pazia liitwalo Mechitza.
katika ukristo kwenye Mila za Kale Kwa karne nyingi, katika makanisa mengi ya kale (ikiwemo baadhi ya makanisa ya Orthodox na Katoliki ya Mashariki), wanaume walikaa upande mmoja wa kanisa na wanawake upande mwingine.
Ingawa Biblia haisemi waziwazi ila inasisitiza juu ya utaratibu na staha. Kwa mfano, katika 1 Wakorintho 14:34-35 na 1 Timotheo 2:11-12, kuna maelekezo yanayoweka mipaka ya ushiriki wa wanawake katika mazingira fulani ya ibada ya hadhara ili kudumisha utaratibu.
Ki ufupi Mgawanyo wa jinsia si jambo la kiislamu pekeeni utaratibu uliokuwepo katika dini zote za Ibrahimu (Uyahudi, Ukristo, na Uislamu) kwa lengo la kudumisha staha na heshima katika nyumba za ibada, ingawa Ukristo wa kisasa katika madhehebu mengi umeacha utaratibu huo.
ukristo umetoka kwenye Uyahudi au umesahau mkuu hata biblia imetoka kwa wayahdi kasoro agano jipya..Ni kweli Kuna makanisa mengi tu wanawake wanakaa upande tofauti na wanaume, nilikuwa nategemea jambo kama hili pia misikiti badala ya wanawake kutengewa kwenye chumba tofauti kabisa.
Hata hivyo mfano wako wa hekalu sio sahihi kwa sababu Ukristo na Uyahudi ni dini tofauti kabisa.
Uislamu umetoka kwenye Uyahudi na Ukristo lakini ni dini tofauti kabisa mkuu.ukristo umetoka kwenye Uyahudi au umesahau mkuu hata biblia imetoka kwa wayahdi kasoro agano jipya..
ni sawa na wamormoni wakatae kuwa hawajatoka kwa wakristo
Mimi nawaelewa watu wa dini wanapojitenga na wanawake kwa kutoa sababu za kibailojia na kimwili, ni kweli hizo sababu ni za msingi na zinaelezeka kisayansi.Hakika dini zina contradictions nyingi na kubwa sana, ila ndio hivyo binadamu nao wan cognitive dissonance ya hali ya juu sana.
Na wewe huna kazi za kufanya mpaka unawafuatilia wanaume wanaoenda Msikitini kuswali swala zote?Halafu kwa nini wanaume ndio huswali sana na kujazana misikitini, ina maana wanawake allah hawahitaji wamswalie mtume? Wazee wanajazana misikitini kuswali swala zote utadhani hawana shughuli za kufanya, ni kuswali tu!
Kutenganisha wanawake na wanaume kwenye dalaladala kwa bongo ingefaa sana kuwadhibiti wanaume Dunga Dunga wanaombambia wanawake makalioni, ila kwenye sebule tofauti ya wanawake na wanaume kwenye nyumba moja sio mpango.Wanawake wanaweza kuswali chumba kimoja na wanaume ila wataswali nyuma yao
Kuna maeneo kama Msikiti wa Makkah wanawake na wanaume wanaswali eneo moja ila wanatenganishwa tu na na barriers kuonesha mipaka yao
Nia ni kuleta modesty na kutoleta temptation na distraction wakati wa swala
Ukienda mbali zaidi, mafundisho ya dini hayaruhusu mchanganyiko usio wa lazima kati ya wanawake na wanaume ambao hawana mahusiano ya kindugu au ukaribu (mahrim)
Kuna baadhi ya nchi hasa za kiarabu ambazo kwenye public transport kama taxi za mchangio,( kwa Tz ni kama ilivyo bajaj) bus, train wanatenganishwa, kwenye foleni za banks pia wanawake na wanaume wana foleni tofauti, kwenye public schools na colleges pia kuna vyuo au madarasa tofauti
Hata nyumba za waarabu wengi kuna sebule 2, moja ya wanawake na nyingine ya wanaume
Kwa upande mwengine, Makanisa ya Eastern Orthodox mf Ethiopia wanafanya hivyo pia na hata Dar kuna kanisa la Father Nkwera wanafanya hivyo, nimeshuhudia kwa macho yangu wanawake na wanaume wanatenganishwa maeneo
Sasa nini maana ya wanawake wa Kiislamu kuvaa hijabu, niqab au burka??Binafsi nadhani waislam wapo sahihi kabisa kutenganisha wanaume na wanawake, kwanza ni ile nature ya ibada yao, kuinama na kuinuka multiple times wakati wa kufanya ibada kunaweza kuwa kigezo cha kwanza kabisa, lakini pia kuondoa vishawishi vya macho. Huku kwa wakristo hata humu watu wengi wamekiri kuondolewa utulivu na usikivu kwa muingiliano wa hizi jinsi mbili.
Nina swali kwenye maelezo yako, ina maana watu wanamswalia mtume au wanamwaslia Mwenyezi Mungu? Huwa hii statement siielewi!!Halafu kwa nini wanaume ndio huswali sana na kujazana misikitini, ina maana wanawake allah hawahitaji wamswalie mtume? Wazee wanajazana misikitini kuswali swala zote utadhani hawana shughuli za kufanya, ni kuswali tu!
Huo ni mtazamo batili . Majaribu yanayokujia na sio ya kutafuta makusudiHivi kwa muktadha wa dini, kipimo cha imani si ndio majaribu?
Hivi mtu huitwa mshindi kwasababu amemshinda mpinzani au kwasababu ameepushiwa mshindani?
Utasemaje una imani thabiti ikiwa ni muoga kuya-face majaribu?
Hii inaenda sambamba kwa moja kwa wale wanaomini funga zao zinaweza kuharibika ikiwa tu watu wengine watakuwa huru kula mbele yao.
naam hilo nalo lipo.Kuna mtu kasema wanawake wanaruhusiwa kuswalia hata nyumbani tu sio lazima waende msikitini ndio maana misikiti mingine haina sehemu za wanawake,
Ni kweli?
Kujistiri, kutikukaa uchi. Ji utaratibu tu mkuu, na kila imani inakuwa na utaratibu wake.Sasa nini maana ya wanawake wa Kiislamu kuvaa hijabu, niqab au burka??
Wakristo wengine wana Mademu mpaka Kanisani sababu ya Mchanganyiko .Binafsi nadhani waislam wapo sahihi kabisa kutenganisha wanaume na wanawake, kwanza ni ile nature ya ibada yao, kuinama na kuinuka multiple times wakati wa kufanya ibada kunaweza kuwa kigezo cha kwanza kabisa, lakini pia kuondoa vishawishi vya macho. Huku kwa wakristo hata humu watu wengi wamekiri kuondolewa utulivu na usikivu kwa muingiliano wa hizi jinsi mbili.
Reasoning capacity yako ni ndogo sana haswa kwenye mambo ya kidini.Sasa nini maana ya wanawake wa Kiislamu kuvaa hijabu, niqab au burka??
Kama unajifunika kwa hijab, niqab au burka ina maanisha sio rahisi umbile la mwili wako wako kuonekana kwa hiyo hata matamanio ya wanaume yanapungua na inakuwa rahisi kujichanganya bila kuamsha hisia, japo ajabu pia ni kwamba kuna watu kama min -me anasema wanaovaa hivyo ndio huwa anawatamani zaidi!Kujistiri, kutikukaa uchi. Ji utaratibu tu mkuu, na kila imani inakuwa na utaratibu wake.
Hivi wewe kama ni mkristo, unapenda namna baadhi ya wanawake wa kikristo wanavyovaa wakienda ibadani?