Zijue sababu za wanaume kufa mapema kuliko wanawake

Zijue sababu za wanaume kufa mapema kuliko wanawake

Pdidy

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
61,678
Reaction score
37,859
NIMEONA HII HABARI BBC NASIKITAKA WANAUME TUNAPITIA MENGI SANA

NIANXE KUTOA RIP WOTE WALIOIIUA LWA SABABU MBALI MBALI

Dunia inaadhimisha Siku ya Afya leo ambapo kwa mujibu wa ripoti za Shirika la afya duniai inakadriwa kwamba karibu wanawake 300,000 hupoteza maisha kila mwaka kutokana na ujauzito au kujifungua, wakati zaidi ya watoto milioni 2 hufa katika mwezi wao wa kwanza wa maisha na karibu wengine milioni 2 zaidi huzaliwa wakiwa wamekufa. Hiyo ni takriban kifo 1 kinachoweza kuzuilika kwa kila sekunde 7.

Japo kuna hiyo idadi ya wanawake kufa na hiyo ya watoto lakini kuna hili kuhusu wanaume.
Mwezi huu serikali nchini Uingereza itazindua mpango juu ya afya ya wanaume. Wataalamu wanasema, hatua hiyo imechelewa kwa muda mrefu, na wanaume wana uwezekano mkubwa wa kufa kabla ya wakati wao kuliko wanawake.

Kuna changamoto juu ya afya ya wanaume - mchanganyiko wa tabia za hatari na ukosefu wa kujiamini na ujuzi wa kutafuta huduma za afya.

Huko Uingereza wanaume wana uwezekano mkubwa wa kuvuta sigara, kunywa pombe, kutumia dawa za kulevya na kuwa na kiwango kikubwa cha lehemu (cholesterol) na shinikizo la damu.

Mambo hayo huchangia kwa kiasi kikubwa, wanaume kufa mapema kuliko wanawake – ikielezwa kuwa hufa mapema kwa miaka minne kuliko wanawake. Pia wanaume wana uwezekano wa karibu 60% kufa kabla ya umri wa miaka 75 kutokana na ugonjwa wa moyo, saratani ya mapafu, ugonjwa wa ini na katika ajali.

Prof Alan White, ambaye alianzisha shirika la misaada la Men's Health Forum na kuanzisha kituo cha afya cha wanaume katika Chuo Kikuu cha Leeds Beckett, anasema suala hili linahitaji kuchukuliwa kwa uzito zaidi.
Anatoa mfano wa janga la Covi 19, wanaume 19,000 zaidi ya wanawake walikufa kutokana na Covid.
 
Watu wanapitia magumu na hawasemi,unakua na ndugu,jamaa or rafiki,usoni unamuona kabisa hayupo sawa,unauliza are you okay??uko poa??always jibu huwa "Fresh mzee"

Now nimejifunza kama nikiona haupo sawa siulizi kama upo sawa,instead nauliza " what's going on in your life,? Mwaka huu unaonaje?Mke familia,watoto??uchumi vipi kaka,kama sio poa leta maneno", huwa natafuta namna ya kuuliza maswali that spark conversations .

Male mental health is on a decline,mimi pia kuna time nilipitia kama ningekua jasiri kidogo ningetangulia,kilichofsnya niwe hai ni kufikiria mama yangu anavyonipenda na kuniamini like for how long will she grieve??

nikimqoute 2PAC kwenye nyimbo yake Thug Mansion,anasema

"Proud times I once contemplated suicide / And would have tried but when I held that gun all I could see was my mama's eyes"

#mensmentalhealthmatters
 
Kwa matatizo niliyonayo nahisi nilishakufa tangu mwaka juzi , kilichobaki msukule wangu tu ndo unaranda randa
 
Wanaume tunapungua sana, ajali nyingi zinaenda na wanaume, harakati za maisha zinafanya wanaume wengi waondoke mapema, kwenye sigara wameandika kabisa ni hatari kwa afya lakini mtu anavuta pakiti nzima kwa siku unategemea nini?
 
Mimi nadhani wanaume kufa mapema ni njia ya nature kutupumzisha na mahangaiko ya kimaisha.
 
Back
Top Bottom