Wanaume kama umebahatika umeajiliwa na ukafikia kustaafu,usifanye kosa
kutumia mafao yako kujenga nyumba n.k
weka pesa yako kwenye mifuko ya akiba kama vile UTT na benki kuu
siku nguvu zikiisha hata kama mkeo hakupendi atapenda pesa,utatunzwa hadi umauti ukukute,
Tatizo kubwa linalowakumba wanaume,mshahara wote unatunza familia.
unasomesha watoto,unashindwa kujenga nyumba ya ndoto yako.
kununua gari ya ndoto yako,ukipata mafao ya uzeeni unajenga nyumba na kununua gari
na pesa yote inaisha,unaanza kulaani watoto kwa kutokukutunza.
Ni kweli watoto wana wajibu wa kuwatunza wazazi wao,ila
wanaume tujitahidi kuweka akiba,tusijisahau.