Nauliza tu swali kwanini wake za watu ni wepesi na wanaongoza kuchepuka kuliko wasichana wasioolewa?
Wake za watu ndio wanaongoza kuchepuka
With experience Nimetongiza wanawake 8 na wote nimekuja kugundua ni wake za watu na wote wamekubali na 5 nimetoka nao na 3 wananisumbua
Nauliza kwanini wake za watu ndio wanagawa sana kuliko wasichana wa kawaida
Ndoa zipo salama kweli nawaza Sana tunaelekea wapi?
Nimejaribu kusoma maoni ya Wananchi wenzangu humu wengi wamejaribu kushare uzoefu kuhusu mada tajwa na wengine kupendekeza possible solutions ili kupunguza risks/athari za uchepukaji nami naomba nichangie kidogo.
Kuna ugonjwa mmoja ndani ya Nafsi ya Mwanadamu unaitwa "Ubinafsi"(Selfishness) yaani mtu kujiona yeye ni bora zaidi kuliko mwingine.
Mgonjwa wa ugonjwa huu asipotibiwa especially kabla hajaingia kwenye Ndoa ili awe anamuona mwenzake ni bora kuliko Nafsi yake nawahakikishia 100% lolote litatokea at any time T.
Kulingana na majukumu yangu ya kijamii(Kiroho & Kisaikolojia) na kesi ninazoletewa kuhusu malalamiko yaliyo ndoani ikiwemo "Kukinaiana plus Uchepukaji" sababu kuu ni kwamba Nafsi za hawa watu hazikuponywa ugonjwa mbaya kuliko magonjwa yote duniani kwenye Nafsi ya Mwanadamu uitwao "Ubinafsi"(Selfishness).
Ile hali ya kumpenda Mke au Mume kama Nafsi yako naturally wengi hawana kwa sababu mizizi ya Ubinafsi imetamalaki ndani yao.
Sasa,kwa sababu Mimi ni Mathematician pia,huwa siangalii tu tatizo na kuliacha hewani. Lazima nichimbe ndani sana kwamba solution yake ni nini?.
Nimejaribu kuangalia suluhisho la kudumu la watu kuondokana na Ubinafsi ni nini. Nimegundua ni watu kumpokea Yesu Kristo mioyoni mwao ili awaambukize(awamiminie) Sacrificial Love(UPENDO wenye asili ya kujitoa sadaka kwa ajili ya ustawi wa wengine) ndio maana ukiniona nipo busy kumuhubiri Yesu Kristo nyumba kwa nyumba au mtaa kwa mtaa usidhani nimekosa kazi za kufanya au nati kichwani mwangu zimelegea la hasha!. Nakuwa napambana kuuondoa ugonjwa mbaya zaidi duniani uitwao UBINAFSI.
Nawaibia siri Mke wangu huwa anahofia sana Mimi kutangulia kufa. Mwanzoni nilijua anatania ila kadiri siku zinavyozidi kwenda nimegundua yupo serious na hofu yake hiyo. Basi Mimi huwa namfariji kwamba siku Mungu ataponiambia "aga kwa maana muda wako wa kuishi duniani umekwisha",nitamwomba akuandae kuishi bila Mimi kwanza. Guess what🤣🤣🤣🤣huwa hanielewi kabisa na wala huwa hataki kuelewa. Kuna UTAMU usioelezeka mioyo miwili iliyoponywa ugonjwa wa Ubinafsi na Yesu ikiungana.
Wale niliowakwaza nisameheni bure maana nimeshindwa kabisa kuvunga kushare UKWELI huu ambao kwa wengine utaonekana ni mchungu.
Wito wangu. Kama kuna mtu au watu humu mmepewa Karama ya kumuhubiri Yesu Kristo hasa kwa vijana ambao hawajaingia Ndoani bado,nawaombeni sana muhubirini Yesu kwa bidii zote. Kwa sababu bila yeye hakuna suluhisho la kudumu la ugonjwa wa UBINAFSI ambao ndio chanzo kikuu cha matatizo mengi sana hapa duniani. Mkilala tu,huko mbeleni suala la NDOA litabaki makumbusho!