Hizi notion huwa mnazitoa wapi Joseph? Huwa mnalijadili hili kwa eksipiriensi gani?
Au tu ni njia rahisi ya kujustify kwanini ndoa zinasumbua… that’s purely simplification.
Siku moja nikakuta sub thread moja kwenye social platform fulani, mleta post ameuliza “kwa tulioolewa bikra, niambie kwanini unajutia kuolewa, na kwanini you started cheating “ moderator nadhani ni mkenya.
Kulikuwa na comments walau elfu 5, kazi yangu ya umbea nilikuwa nasoma na ku view profile za watu 😅
Nikafanya content &thematic analysis kupitia comments, opinions na patterns… conclusion ikaja hivi: Wanawake wanacheat back sababu ya kuvurugwa na wanaume, common patterns inasema walioolewa wadogo miaka 17/16-20 wakifika miaka 23 wanakuwa wameshaanza kuchepuka… Walioolewa wakubwa 25/30’s wana tendency ya kuishi kwenye ndoa kama wameachika ikiwemo kuchannel muda&energy zao kwenye kazi/biashara na kuchepuka.
However, ukisoma comments za wanaume utagundua walioa bikra wako okay “kuanzisha” mwanamke akianza kuchepuka he will care less, ni kama ule msemo wa nimeanzisha hao wengine watajua wenyewe, purely it’s good for the men’s ego.