HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Sio kupata kazi tu hata ku appear kwenye shortlisted yaani kuitwa kwenye huo usaili ni ngumu sana. Lakin PSRS walikuwa wanaita wote wenye sifa na vigezo vilivyowekwa.
Hapa kwenye kuwa shortlisted ndo tutatafutana, watu watarudi wenyewe hapa kukubali Bora psrs
 
Nina changamoto ya kutopata activation link kwa hizi posts za TRA, je kuna wengine wenye hili tatizo?
 
Mimi Tanroad nina ushahidi tena wa kujionea kabisa , rafiki yangu mmoja yupo Tanroad mkoa fulani, wife wangu aliomba nafasi ya Assistant accountant hapo , nikamuambia shemeji yako nae amejaribu tuma maombi hapo jibu alilonipa akaniambia "duh brother hali imebana nafasi zote wamepewa ndugu au watoto wa wafanyakazi wa hapa , nikajua ni masihara , Wife akaitwa kwenye usaili akafanya mpaka oral akakutana na shemeji ake baada ya usaili, akamwambia shemeji poleni sana , maana nafasi zenyewe zimegombaniwa na staff hapa, kweli kuja kucheki walioitwa kazini ni watoto na ndugu zao nae jamaa yangu alikuwa na mdogo wake nae akapata kazi, kwa hiyo anachokizungumza mwenzetu hapo juu ni kweli maana mimi nimeshuhudia jambo hili Tanroad, so wakati tunapolifurahia hili tujue pia kuna madhara yake mbele ya safari.
Mimi nishawai kufanya Shift incharge hapo TAN ROAD tena ni ya mkataba tu, nilichokutana nacho we acha tu hata matokeo ya oral hawatoi wale jamaa wanawapigia simu waliofaulu kwenda oral. Swali je kuna uhakika gani kama wanaopigiwa simu ndio waliofanya written?
 
Watu wangu wa karibu kibao walikula asali TRA sahizi wananipigia na kudai kama sii PSRS mchakato ungekuwa mgumu bado wanaishukuru psrs
Kuna mtu humu kwenye thread alisema inasemekana TRA wanaitaji watu 1000 baadhi watatoka data base na wengine watafanya interview ndo haya tunayaona(picha linaaza mara system inazingua mwisho wa siku deadline)....hapa hakuna interview zaidi wanaenda kukamiliza dili lao la wanajitolea kwa mgongo wa Utumishi kuwatema
 
Kwenye usaili mnakandwa na PSRS
Ukienda kazini unakandwa na Madiwani,😂😂
 

Attachments

  • Madiwani.jpeg.jpg
    Madiwani.jpeg.jpg
    58.9 KB · Views: 26
Yaani huu mchakato wa ajira bora ungebaki PSRS kwasababu sekretalieti ya ajira ukifanikiwa kuingia oral unaweza baki database pindi taasisi nyingine itakapohitaji watu wenye sifa yako unaweza bahatika , sasa taasisi zikiajiri zenyewe hata ukipata juu ya 50 kwenye usaili wa oral hakuna database, anyway ngoja tuone itakuwaje.

Mkuu, umeongea hoja kubwa sana.
 
Nimejaribu kufungua link hiyo nikapewa mrejesho huu hapa:

Unauthorized Access

You have attempted to access a page that you are not authorized to view.

If you have any questions, please contact the site administrator.


Sasa najiuliza ni nani yuko authorized to view!! Hebu jaribuni kufungua hiyo link ya kufanyia application mjionee hiyo figisu figisu right from day one!!
Mimi si mwombaji wa ajira, nilitaka tu kuona kama ni kweli hiyo link haifunguki kama watu wanavyosema!!

Aisee.
 
"365 ZA KUJIVUTAVUTA"

Screenshot_20230528_072952.jpg


Leo ni tarehe 28/05/2023, ni mwaka mmoja kamili tangu sekretarieti ya ajira PSRS itangaze nafasi za kazi MDA&LGA (maarufu kama mkeka wa taifa) mnamo tarehe 28/05/2022.

Tukiwa katika maadhimisho haya mujarab ya kusherekea siku 365 za PSRS "kuendelea na mchakato" wa ajira tajwa hapo juu, ninakuletea makala "fupi" pamoja na maoni yangu ya jumla kuhusu kinachoendelea (ucheleweshaji wa michakato ya ajira).

Utangulizi:-
Rais wa awamu ya sita alipoingia madarakani, pamoja na mambo mengine, alifanya tathmini ya rasilimali watu serikalini na kugundua kuna upungufu mkubwa wa watumishi. Kwa kuanzia aliridhia kutangazwa kwa ajira 32,000 ili "kuziba magepu".
Katika ajira hizo, sekta za elimu na afya ndio zilikua na uhitaji mkubwa zaidi. Hayo yalielezwa na waziri wa utumishi wa wakati huo Mh Jenista Mhagama mnamo 6/4/2022.
Screenshot_20230528_071229.jpg


Wiki moja baadae Mh. waziri Mhagama alitoa mchanganuo kama ifuatavyo:-
Screenshot_20230528_071738.jpg

Hapo juu ni ajira za afya na elimu ambazo zenyewe zilitolewa kwa uratibu wa TAMISEMI.
Hadi sasa watu hao tayari wapo kazini na wameshakula mishahara zaidi ya nane.

Screenshot_20230528_071914.jpg
Hapo juu ni nafasi za kada zingine ambazo ziliratibiwa na PSRS. Kada hizi ndizo zilizozaa tangazo la kazi la MDA&LGA la 28/05/2022 (mkeka wa taifa) ambalo leo ndio tunalifanyia ANNIVERSARY au BIRTHDAY ya kutimiza mwaka 1 bila kukamilika.
"365 za kujivutavuta"
Screenshot_20230528_072952.jpg

Na huu ndio mwisho wa utangulizi.

Hadi sasa:-
PSRS hadi dakika hii na sekunde hii bado hawajakamilisha mchakato mzima wa kuwaajiri watu 2057 kwa mujibu wa tangazo tajwa hapo juu.
Sababu zinaweza kuwa nyingi, hata milioni zikafika, zinaweza kuwa zinawahusu wao au haziwahusu wao, lakini FACT ON THE TABLE ni kwamba ni mwaka sasa na bado hawajakamilisha zoezi hilo.

Maoni yangu:-

1. Nawapongeza PSRS kwa utendaji wao wenye "muonekano wa kutokua na upendeleo", lakini sifurahishwi na kasi ndogo ya utendaji wao. KUJIVUTAVUTA.

2. Mimi nitakua mtu wa mwisho kuamini kwamba utendaji wa PSRS hapa ndipo ulipoishia. Kwamba hakuna namna inayoweza kufanyika kuboresha utendaji wao. Na kama wao wanaamini "this is the best we can expect from them", basi kama taifa tutakua tupo kwenye shida kubwa mno.

3. Kuna madai kwamba PSRS "wanacheleweshwa na waajiri". Mimi nasema "if PSRS are innocent, then they are not smart". (They cannot be both)
Taasisi yoyote ile katika utendaji wake, inapaswa kutoa huduma bora ili "ijijengee reputation" yake. Kama wao PSRS wanabeba makandokando ya waajiri, yanayopelekea wao kuonekana wanatoa huduma mbovu, then they are not smart.

4. Aina ya utendaji wa PSRS inatoa mwanya kwa "wajanja" (taasisi zinazotaka kuajiri zenyewe) ziweze kuruhusiwa kufanya hivyo. Aina hii ya utendaji wa kutumia mwaka mzima kuajiri watu elfu mbili, ina suggest kwamba taasisi hiyo "imezidiwa na kulemewa" na hivyo inahitaji zaidi "kusaidiwa kazi" badala ya "kuongezewa kazi zingine."
Nimeona TRA jana wamefanya, endapo TPA nao wakitaka kufanya hivyo, inakua easy kuwashinda PSRS (kwa hoja mbele ya third party, awe Rais au PM) hata kama TPA watawakilishwa na bibi yangu mzaa baba katika kikao hicho.
Reputation ya utendaji ya PSRS kwa siku za hivi karibuni inawatafuna wenyewe.

Vipimo vyangu vya kutoridhishwa na kasi ya PSRS ni hivi hapa:-
A. Wanalalamikiwa na wanaowahudumia (job seekers). Ndio maana leo tuna huu uzi (Kwanini utumishi wanachelewesha.....)

B. Wanalalamikiwa na mkuu wa nchi. (Hakuna kitu kibaya kama hiki). Rais Samia ameshawahi kusikika akisema kwamba michakato ya ajira inachukua muda mrefu mno kukamilika. Na tangu siku hiyo mimi binafsi sijaona mabadiliko yoyote ya kasi ya utendaji wa PSRS katika hilo.

C. Ajira hizi (MDA&LGA) ni sehemu ya package ya ajira 32000 ukijumuisha na afya na elimu ambazo ziliratibiwa na TAMISEMI. Ukweli kwamba afya na elimu wao walishakamilisha michakato yao kwa zaidi ya miezi 8 iliyopita. Ukweli huu unawaweka PSRS katika mazingira magumu sana kuaminika kwamba kasi yao inatosha na inapaswa kutumainiwa.

D. Muda ni mali, kwa vyovyote vile iwavyo, umeshapita mwaka sasa bado PSRS hawajakamilisha zoezi hili. (28/05/2022 hadi 28/05/2023).

Nawatakieni nyote weekend njema na maadhimisho mema ya "365 za kujivutavuta".

Ulumbi.
 
Back
Top Bottom