HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
"365 ZA KUJIVUTAVUTA"

View attachment 2637528


Leo ni tarehe 28/05/2023, ni mwaka mmoja kamili tangu sekretarieti ya ajira PSRS itangaze nafasi za kazi MDA&LGA (maarufu kama mkeka wa taifa) mnamo tarehe 28/05/2022.

Tukiwa katika maadhimisho haya mujarab ya kusherekea siku 365 za PSRS "kuendelea na mchakato" wa ajira tajwa hapo juu, ninakuletea makala "fupi" pamoja na maoni yangu ya jumla kuhusu kinachoendelea (ucheleweshaji wa michakato ya ajira).

Utangulizi:-
Rais wa awamu ya sita alipoingia madarakani, pamoja na mambo mengine, alifanya tathmini ya rasilimali watu serikalini na kugundua kuna upungufu mkubwa wa watumishi. Kwa kuanzia aliridhia kutangazwa kwa ajira 32,000 ili "kuziba magepu".
Katika ajira hizo, sekta za elimu na afya ndio zilikua na uhitaji mkubwa zaidi. Hayo yalielezwa na waziri wa utumishi wa wakati huo Mh Jenista Mhagama mnamo 6/4/2022.
View attachment 2637532

Wiki moja baadae Mh. waziri Mhagama alitoa mchanganuo kama ifuatavyo:-
View attachment 2637536
Hapo juu ni ajira za afya na elimu ambazo zenyewe zilitolewa kwa uratibu wa TAMISEMI.
Hadi sasa watu hao tayari wapo kazini na wameshakula mishahara zaidi ya nane.

View attachment 2637542
Hapo juu ni nafasi za kada zingine ambazo ziliratibiwa na PSRS. Kada hizi ndizo zilizozaa tangazo la kazi la MDA&LGA la 28/05/2022 (mkeka wa taifa) ambalo leo ndio tunalifanyia ANNIVERSARY au BIRTHDAY ya kutimiza mwaka 1 bila kukamilika.
"365 za kujivutavuta"
View attachment 2637562
Na huu ndio mwisho wa utangulizi.

Hadi sasa:-
PSRS hadi dakika hii na sekunde hii bado hawajakamilisha mchakato mzima wa kuwaajiri watu 2057 kwa mujibu wa tangazo tajwa hapo juu.
Sababu zinaweza kuwa nyingi, hata milioni zikafika, zinaweza kuwa zinawahusu wao au haziwahusu wao, lakini FACT ON THE TABLE ni kwamba ni mwaka sasa na bado hawajakamilisha zoezi hilo.

Maoni yangu:-

1. Nawapongeza PSRS kwa utendaji wao wenye "muonekano wa kutokua na upendeleo", lakini sifurahishwi na kasi ndogo ya utendaji wao. KUJIVUTAVUTA.

2. Mimi nitakua mtu wa mwisho kuamini kwamba utendaji wa PSRS hapa ndipo ulipoishia. Kwamba hakuna namna inayoweza kufanyika kuboresha utendaji wao. Na kama wao wanaamini "this is the best we can expect from them", basi kama taifa tutakua tupo kwenye shida kubwa mno.

3. Kuna madai kwamba PSRS "wanacheleweshwa na waajiri". Mimi nasema "if PSRS are innocent, then they are not smart". (They cannot be both)
Taasisi yoyote ile katika utendaji wake, inapaswa kutoa huduma bora ili "ijijengee reputation" yake. Kama wao PSRS wanabeba makandokando ya waajiri, yanayopelekea wao kuonekana wanatoa huduma mbovu, then they are not smart.

4. Aina ya utendaji wa PSRS inatoa mwanya kwa "wajanja" (taasisi zinazotaka kuajiri zenyewe) ziweze kuruhusiwa kufanya hivyo. Aina hii ya utendaji wa kutumia mwaka mzima kuajiri watu elfu mbili, ina suggest kwamba taasisi hiyo "imezidiwa na kulemewa" na hivyo inahitaji zaidi "kusaidiwa kazi" badala ya "kuongezewa kazi zingine."
Nimeona TRA jana wamefanya, endapo TPA nao wakitaka kufanya hivyo, inakua easy kuwashinda PSRS (kwa hoja mbele ya third party, awe Rais au PM) hata kama TPA watawakilishwa na bibi yangu mzaa baba katika kikao hicho.
Reputation ya utendaji ya PSRS kwa siku za hivi karibuni inawatafuna wenyewe.

Vipimo vyangu vya kutoridhishwa na kasi ya PSRS ni hivi hapa:-
A. Wanalalamikiwa na wanaowahudumia (job seekers). Ndio maana leo tuna huu uzi (Kwanini utumishi wanachelewesha.....)

B. Wanalalamikiwa na mkuu wa nchi. (Hakuna kitu kibaya kama hiki). Rais Samia ameshawahi kusikika akisema kwamba michakato ya ajira inachukua muda mrefu mno kukamilika. Na tangu siku hiyo mimi binafsi sijaona mabadiliko yoyote ya kasi ya utendaji wa PSRS katika hilo.

C. Ajira hizi (MDA&LGA) ni sehemu ya package ya ajira 32000 ukijumuisha na afya na elimu ambazo ziliratibiwa na TAMISEMI. Ukweli kwamba afya na elimu wao walishakamilisha michakato yao kwa zaidi ya miezi 8 iliyopita. Ukweli huu unawaweka PSRS katika mazingira magumu sana kuaminika kwamba kasi yao inatosha na inapaswa kutumainiwa.

D. Muda ni mali, kwa vyovyote vile iwavyo, umeshapita mwaka sasa bado PSRS hawajakamilisha zoezi hili. (28/05/2022 hadi 28/05/2023).

Nawatakieni nyote weekend njema na maadhimisho mema ya "365 za kujivutavuta".

Ulumbi.
Umeiweka vzr sana Ulumbi!
Ngoja tusubiri labda majina yaliyosalia yatatoka kwa mkupuo!
 
Unachofanya na ulichosema ni kweli. Kuna Shida sana Kwa kazi za Utumishi haswa idara kama hizo. Juzi kuja watu walifanya usaili wa FOREIGN AFFAIRS yaani Watu wamefika mpaka oral lakin kuja kuitwa wanaita sura mpya. Wengine unaambiwa max zao zilikua za kawaida ila sim inapigwa maksi zinaongezwa.
Mengine juu ya Utumishi wanazushiwa lakin kuvhelewa kuita watu kazini inatia ashaka sana
 
Sehemu ya kuweka vyeti, barua na mazaga mengine utaikuta mwisho kama umeshamaliza kujaza zile sehemu za mandatory yaani zenye mark ya * nyekundu then nenda sehemu ya search job kwenye menu ya portal then chagua post unayotaka kuapply then itafunguka ndio utaona hizo sehemu za attachments nadhani utakuwa umeelewa
Nashukuru sana mkuu
 
Tatizo nyakati zimebadilika ,ni miaka sita sasa ajira zimekuwa finyu sana ukilinganisha na idadi ya wahitimu ,sasa unapoweka loopholes kama hizi ,hata hao vigogo wana watoto ,ndugu ,rafiki na hata vimada wengi tu na wao wamehitimu ndani ya hii miaka karibia saba sasa na wanahitaji ajira tena kwa kupitia hizo connection za kihalifu kwa rushwa na nepotism ,do the math hapo na ufanye probability ya mtoto wa masikini kutoboa kwenye huo msongamano ,
Corruption na nepotism kwenye hizo taasisi inajulikana ,hamna haja ya kueleweshwa ,tena TRA ni notorious Kwa Hilo suala miaka mingi ,wamekuwa na scandals hizo muda mrefu ,ninyi mnaomsifia huo mfumo ni either hamjui mnaloongea au ni wanufaika wa huo mfumo wa corruption na nepotism ,period .
Kuna taasisi zimekuwa zikiajiti zenyewe kwa muda mrefu tangia hata PSRS ilivyo anzishwa mfano Tanroads , wanaaajiri mara kwa mara hizo ajira za mikataba ,sasa mtafute mtu ambaye alishahudhuria hizo sahili zao akupe habari ,
Aisee this is seriously bad
ure genius champ.

huu mfumo kurudishwa kwenye taasis husika cc wa kutoka mabwepande tutasota sana ,ebu angalieni mfano ajira za majeshi ni mwendo wa baba kanituma na maelekezo makubwa kutoka juu.
 
Jaman naombeni msaada katika application ya TRA sioni sehemu ya kuweka birth certificate na passport size katika ile system yao aliyefanikiwa naomba msaada
 
Kwa sababu ktk tangazo lao wamesema wanaitaji hivo vitu
Sehemu ya kuweka vyeti, barua na mazaga mengine utaikuta mwisho kama umeshamaliza kujaza zile sehemu za mandatory yaani zenye mark ya * nyekundu then nenda sehemu ya search job kwenye menu ya portal then chagua post unayotaka kuapply then itafunguka ndio utaona hizo sehemu za attachments nadhani utakuwa umeelewa
 
Sehemu ya kuweka vyeti, barua na mazaga mengine utaikuta mwisho kama umeshamaliza kujaza zile sehemu za mandatory yaani zenye mark ya * nyekundu then nenda sehemu ya search job kwenye menu ya portal then chagua post unayotaka kuapply then itafunguka ndio utaona hizo sehemu za attachments nadhani utakuwa umeelewa
dah bahati mbya sikuattach passport size..na nishasubmit..Aisee nilitumiwa link tu niapply jana usiku wala sikuona tangazo lote...Hivi luna namna nikareverse ?
 
Back
Top Bottom