HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Hii sehemu ya kujaza refference details n mm tu ndo napata shida au kuna sehemu nakosea,,
Naambiwa an email is invalid, wakt naingiza kama ilivyo na wala haijakosewa. Nakosea wapi wadau
 
Sasa kwa nini watu wasiombe tu kupitia psrs then wao wachukue majina yao washortlist wasimamie mchakato wao..kuliko kuanzisha mfumo mpya tena au kuna lililo nyuma ya pazia
Unafikiri wakifanya hivo watoto wao wataingizwa vipi? We hujiulizi wale waliobakishwa database ndio basi tena, hiyo ni njia ya kuwaweka hao wanaowaita wakujitolea mda mrefu na waliomaliza mwaka jana na mwaka huu keshokutwa kontena jingine linamwagwa mtaani, kwahyo wewe hapo omba Mungu tu atende muujiza uonekane kama huna memo.

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Wiki nyingine tena ya kuendelea kungojea pdf za mwendo wa kinyonga.
Nilikuwa mfuasi wa psrs kindakindaki na mpingaji mkubwa wa taasisi kumiliki mchakato wa ajira.

LAKINI, KWA KILICHOTOKEA TRA KUJIFANYIA JAMBO LAO Naunga mkono 100%.
Japo najua changamoto ya kujuana itarudi. Ni bora nijue asilimia za kupata kazi ni 20% na nikienda kufanya usaili napata matokeo ya kufeli ontime.
Kuliko niwe na asilimia 95% za kupata kazi alafu nitumie mwaka hadi miaka miwili kupata majibu.
Wakati huo nina;
1. Depression na mastress
2. Shughuli haziendi.
3. napoteza muda.
4. Kazi sipati.
5. Napoteza pesa kuwinda kisichowindika.
6. nahatarisha kibarua nilichonacho
7. Nadhoofika mwili na kupata maradhi kwa mastress na depression
8. natumbukia kwenye kukata tamaa. N.K

Jamani PSRS wakisema mtatukumbuka waambieni hivi

"Nchi yetu haitoweza kutuajiri wote kutokana na uchumi wa nchi yetu ulivyo, tulichokuwa tunataka ajulikane aliyepata kazi na asiyepata kwa wakati sahihi ili maisha yaendelee na sio wote tupate kazi na hatuna sononeko kwenye hili".
 
Mimi nilivyofanya interview kwenye taasisi fulani
Walihitajika watu sita na tuliitwa 16
Kwenye placement wakaitwa wawili
Lakini kuripoti kazini wameenda wote sita
Na hao wanne haijulikani wametokea wapi!
Sina tena imani nao kwa kweli

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mimi nilivyofanya interview kwenye taasisi fulani
Walihitajika watu sita na tuliitwa 16
Kwenye placement wakaitwa wawili
Lakini kuripoti kazini wameenda wote sita
Na hao wanne haijulikani wametokea wapi!
Sina tena imani nao kwa kweli

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Mpaji ni Mungu, yawezekana anakuandalia nafasi nzuri zaidi.
 
Back
Top Bottom