Ndege mmoja alie mkononi ni heri kuliko wengi walio msituni. Anza Kwa nafasi unayoona Kuna uwezekano wa kupata then huko utaanza kupambana polepole kuingia kwenye hayo mashirika.
Nina kaka angu aliajiliwa kama Mwl wa secondari kwa masomo ya biashara. Baada ya muda akaomba kuamia Halmashauri kama Afisa hesabu kwa sababu palikuwa na uhaba huo akapata. Amefanya kazi Kwa zaid ya miaka kumi huku akiendelea kusoma na kuomba kazi ktk taasisi na mashirika ili aweze kuhamia.
Mwaka Jana mwezi wa kumi na mbili amepata barua ya kuitwa kazini ktk Bodi Fulani. Na sasa anaenjoy salary nzuri na posho pia fresh.
NB: Vijana tubadilike, tusidharau mshahara wa Serikali wkt wengi bado ni tegemezi. Wengi mnaoona wapo sehemu nzuri Kwa sasa hawakuanzia hapo. Ukifanikiwa kupata kazi kwanza ipende, jitume na ufanye Kwa umakini wako wote hicho ndio kitafungua milango yako unayotaka.