HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

HOJA Kwanini Utumishi wanatumia muda mrefu kuita Watu kazini?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
Jmn nashukuruni Wana JF wote katika kutiana moyo kwenye kipind chote japo siyo Kila comment nilikuwa na jibu lakini nilikuwa naonesha ushirikiano ata kwa Ku like, Ila ningependa kutanguliza shukran zangu za dhati kwa Mungu kunijalia kupata nafasi kweny hizi placements zilizotoka leo za TRA.. tutakuwa pamoja wadau, Mungu awabariki sana
Hongera sana mkuu, ukawe mtumishi mwema
 
Kiukweli nimekandwa na namshukuru Mungu nafsi ina Amani japo sikupambana kukosa naamini bado nina nafasi wapambanaji tusikate tamaa bado nafasi tunayo one day yes.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Pole sana mkuu, una riziki yako mahali ila muda bado haujawadia. Usife moyo, usikate tamaa, endelea kupambana zaidi. Tuendelee kuombeana kama kawaida yetu humu
 
Mkuu jamaa wanatazama nankuchukua wale waliofanya vizuri zaidi katika usaili, hizo CV na GPA kila chuo kina namna ziafanya kwa graduate wake.

Tukubaliane tu, tuliobaki hatukupata alama za kutosha.



Kwanini wayatoe mara tu baada ya Rais kuwasema ?
 
Kwanini wayatoe mara tu baada ya Rais kuwasema ?
Huo ni urasimu wao tu, na ndio uliopelekea kuwepo kwa uzi huu, tizama kichwa cha uzi huu kimeuliza kuhusu nini?

Ni vitu ambavyo tulio nje tunakosa majibu ya moja kwa moja, na hata baadhi ya waliopata ajira wameshuhudia humu kuwa, barua zao zilisainiwa tarehe za nyuma, mwezi mmoja nyuma, kabla ya placement kutoka.
 
Bora huu mkeka wa TRA umetoka..
Sasa tunawaza mikeka ya November na December tu,, according to mkwara wa Mama yetu Leo.. hii mikeka iliyobaki bila shaka itatoka huu mwezi Ferbuary
Kwa kweli nasi tunasubiri kwa hamu.Na Mimi naimani Kubwa PSRS watakuwa wameshaktuka na kuamshwa.
 
Leo ni Kama vile wamekurupishwa Na kulazimika kutoa majina ambapo mashaka ni mengi!

Huenda hawakujiandaa kutoa yale majina, huenda watu genuine wameachwa sababu ya zimamoto style ya kulazimika kutoa yale majina.

Kuna watu wana cv GPA za vyuo vya kueleweka wameachwa! Imagine!

Bora ivunjwe ijulikane moja maana miueyusho tu!
Mkuu ajira haiangalii GPA. Kuna mtu alikuwa miongoni mwa walioongoza written ila hajapata kazi
 
Huo ni urasimu wao tu, na ndio uliopelekea kuwepo kwa uzi huu, tizama kichwa cha uzi huu kimeuliza kuhusu nini?

Ni vitu ambavyo tulio nje tunakosa majibu ya moja kwa moja, na hata baadhi ya waliopata ajira wameshuhudia humu kuwa, barua zao zilisainiwa tarehe za nyuma, mwezi mmoja nyuma, kabla ya placement kutoka.



Kwa hiyo kumbe tunakubaliana kuwa hao jamaa ni shida kama Rais alivyosema!
 
Kwa hiyo kumbe tunakubaliana kuwa hao jamaa ni shida kama Rais alivyosema!
Shida ni katika huo urasimu wa kutangaza au kutoa placement. Kwa washiriki wengi bado wanaimani na namna wanavyoendesha mchakato, shida ipo hapo katika kuhitimisha, hilo moja.

Pili, kumbuka aliyetoa hilo tangazo ni mwanasiasa, na katika nchi zetu hizi, wanasiasa hutumia hizi kwa advantage zao japo ukweli kinachopelekea haya wanayafahamu.
 
Nilichukua muda kidogo kuweza kuvuta pumzi na kutoa maoni yangu kuhusu interview ya TRA.

Kwanza nianze kwa kuwapongeza mliochaguliwa ni bahati na inapaswa kumshukuru Mungu.

Binafsi tukianza na interview ya TRA iliyopita niliikosa kwa marks 0.5 iliniuma sana ikabidi nikubaliane na hali na kujipanga kwa interview inayofuata na namshukuru Mungu nilifanikiwa kutinga oral ambayo leo imetoka ila bado Mungu hakunipa kibali cha kuwa miongoni mwao na kwakuwa nimegraduate muda mrefu sasa huenda nikaangazia mambo mengine.

Shuhuda za status (Selected for Null then Selected for practical then Selected for null then Selected for practical) Je, status zina determine selection? bado ni fumbo!

Kila la kheri mnaosubiria pdf na wale mnaotarajia kwenda kwenye oral interview.

Pole sna mwamba tuendelee kupambana. Umegraduate mwaka gani?.
 
Najikaza kua niko strong ila kiukweli this is more than pain kwa yanayonisibu right now.

Nina madeni chungu nzima na hata sikopesheki.

Wife mwezi ujao anajifungua sina pesa .

TRA lililokua tumaini langu nimedondokea pua .

Sijui what next.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Hello ndugu pole lakini usikate tamaa believe me hiyo ya TRA haikuwa katika mpango wa Mungu kwako bali muombe Mungu bila kuchoka atakupatia nafasi nyingine kadri ya mapenzi yake.Mie ni Muhenga but I feel your pain iliwahi kunipata miaka hiyo late 90's wakati TRA imeanzishwa nikiwa hoi nafanya kibarua katika kampuni za wahindi mitaa ya Stendi ya Kisutu(Miaka hiyo mabasi ya Moshi Arusha yalikuwa yanaanzia hapo) nikawa nimeitwa interview TRA lakini nikachelewa kufika interview kwa sababu ile barua ya Invitation ya Interview iliyotumwa kwa REGISTER ya POSTA(Wakati huo hakuna mitandao wala simu za mikononi) nilichelewa kuipata kwani Box ya Posta niliyotumia ndugu hawakunitafuta kunipatia hiyo barua,hivyo siku moja nilipopita kwa hao ndugu nikakuta naitwa interview lakini deadline ilikuwa imepita kwa siku moja na nilipoenda Chuo cha Kodi Mwenge nikakuta walishafunga zoezi nikajaribu kujieleza lakini it was too late.
Kwa kweli nilikuwa frustrated na very desperate na iliniuma sana na nikajiona nina mkosi lakini baadae nikapiga moyo konde na nikaendelea kufanya application kwingine na baada ya mwezi mmoja nikaitwa interview kwenye shirika moja la umma ambalo lilikuwa lipo vizuri kama TRA na fortunately nikawa selected na kupata ajira ambayo nimekuwa nayo hadi leo.
Cha kushangaza,kuna jamaa kama wawili nilikuwa nawafahamu waliopata ajira TRA katika kipindi hicho nilichokosa hawakudumu kazini hapo TRA walifukuzwa kazi kabla hata ya kufikisha three(3) years kwa hiyo nikawaza pengine na mie labda nisinge-survive hapo kazini,japo simaanishi kuwa hakuna Job security bali najaribu kuelezea kuwa haya mambo yana lots of dynamics.
Hivyo,naku-inspire usikate tamaa endelea kupambana wakati wa Bwana ukifika utapata sehemu ambapo kuna fungu lako
 
Back
Top Bottom