Twinawe
JF-Expert Member
- Oct 3, 2016
- 2,552
- 5,676
Ahsante sana babaHello ndugu pole lakini usikate tamaa believe me hiyo ya TRA haikuwa katika mpango wa Mungu kwako bali muombe Mungu bila kuchoka atakupatia nafasi nyingine kadri ya mapenzi yake.Mie ni Muhenga but I feel your pain iliwahi kunipata miaka hiyo late 90's wakati TRA imeanzishwa nikiwa hoi nafanya kibarua katika kampuni za wahindi mitaa ya Stendi ya Kisutu(Miaka hiyo mabasi ya Moshi Arusha yalikuwa yanaanzia hapo) nikawa nimeitwa interview TRA lakini nikachelewa kufika interview kwa sababu ile barua ya Invitation ya Interview iliyotumwa kwa REGISTER ya POSTA(Wakati huo hakuna mitandao wala simu za mikononi) nilichelewa kuipata kwani Box ya Posta niliyotumia ndugu hawakunitafuta kunipatia hiyo barua,hivyo siku moja nilipopita kwa hao ndugu nikakuta naitwa interview lakini deadline ilikuwa imepita kwa siku moja na nilipoenda Chuo cha Kodi Mwenge nikakuta walishafunga zoezi nikajaribu kujieleza lakini it was too late.
Kwa kweli iliniuma sana na nikajiona nina mkosi lakini baadae nikapiga moyo konde na nikaendelea kufanya application kwingine na baada ya mwezi mmoja nikaitwa interview kwenye shirika moja la umma ambalo lilikuwa lipo vizuri kama TRA na fortunately nikawa selected na kupata ajira ambayo nimekuwa nayo hadi leo.
Cha kushangaza,kuna jamaa kama wawili nilikuwa nawafahamu waliopata ajira TRA katika kipindi hicho nilichokosa hawakudumu kazini hapo TRA walifukuzwa kazi kabla hata ya kufikisha three(3) years kwa hiyo nikawaza pengine na mie labda nisinge-survive hapo kazini,japo simaanishi kuwa hakuna Job security bali najaribu kuelezea kuwa haya mambo yana lots of dynamics.
Hivyo,naku-inspire usikate tamaa endelea kupambana wakati wa Bwana ukifika utapata sehemu ambapo kuna fungu lako
Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app