Kwanini tozo za miamala zisitumike kuajiri walimu?

Uhaba wa walimu kimekuwa kilio kikubwa na hatimaye kimegeuka wimbo wa taifa unaoimbwa kila kukicha.

Juzi kwenye taarifa ya habari tumesikia mkoa wa geita ukilalamikia ukosefu wa walimu wa masomo ya sayansi. Ukienda shinyanga kilio ni hicho hicho, tabora kilio hicho hicho, ukienda kusini huko ndio usiseme kabisaa. Yaani ni kilio nchi nzima si shule za mijini si vijijini pote hali ni mbaya.

Mwenyewe ni mwalimu na kwenye shule yangu tunao wanafunzi zaidi ya mianane na walimu wa sayansi tuliopo ni wawili tu. Tunafundisha kwa rotation kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne non stop from morning to evening kwa mshahara ule ule bila hata posho ya overtime au ugumu wa kazi. Yaani briefly tunafanya kazi kama watumwa ndani ya nchi yetu.

Kuna muda hadi unakata tamaa na kutamani kuacha kazi ila ukikumbuka kuna familia nyuma inakutegemea unaamua tu kuendelea kibabe. Yote haya yanatokana na upungufu mkubwa wa walimu uliopo kwenye shule zetu lakini serikali inajifanya haioni kama kuna tatizo. Sasa kuliko kuendelea kutesana na kukosesha wanafunzi masomo, Je serikali haioni umuhimu wa kutumia tozo inazokusanya kwa wananchi kuajiri walimu wa kutosha ili kutatua uhaba mkubwa wa walimu uliopo?

Au wana member nyie mnasemaje?

Karibuni kwa mawazo
Tozo ni kwa ajili wa CCM,
 
Back
Top Bottom