Tahadhari kwa Wizara ya Elimu; Walimu wa hisabati shule za msingi hawapo

Mbogi

JF-Expert Member
Oct 10, 2021
681
825
Uhakika wa uchunguzi uliofanywa ktk shule za mkoa wa Dar es salaam ulio na walimu wengi umeibua chanzo kikubwa cha kufeli kwa wanafunzi somo la hisabati katika matokeo ya mtihani wa taifa kuwa ni uhaba mkubwa Sana wa walimu wa somo la hisabati ambapo walimu karibia wote wanaofundisha somo la hisabati shule za msingi kuanzia darasa la Kwanza hadi darasa la tano siyo walimu waliopata mafunzo na mbinu za ufundishaji wa somo hilo.

Uchunguzi umebaini kuwa katika shule moja wapo walimu wawili tu au mmoja anayeweza na aliye na taaluma ya mafunzo sahihi ya somo hili ambaye katika shule zote huyo ndiye hutumiwa kwa darasa la saba huku wakiwapokea wanafunzi wakiwa tayari Wana msingi mbovu wa somo hilo.

Chonde chonde tunaiomba serikali kuchukua hatua za haraka na za maksudi kuokoa jahazi kuajiri walimu wa Hisabati vinginevyo tutarajie matokeo mabaya zaidi mwaka ujao na mbaya zaidi kukosekana kwa wataalamu wa uchumi na wengineo.

NAWASILISHA KWA MJADALA WA MAONI NA USHAURI JUU YA JANGA HILI.
 
1. Who cares? kikubwa Maboss wizarani wanapata mishahara na stahiki zao zote na pia VX zimejaa mafuta full-tank. Hayo mengine mtajuana huko BUZA SEC

2. Tumechagua ujinga kama agenda yetu ili tuendelee kupata chawa na cheap labour
 
Back
Top Bottom