Moshi: Shule ya Sekondari Mji mpya ina uhaba wa Walimu wa Sayansi, walazimika kuchangisha fedha na kuajiri Walimu wa Muda

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,024
1,616
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mji Mpya iliyopo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameiomba Serikali kuwapatia walimu wa masomo ya Sayansi pamoja na kuweka vifaa katika maabara ya Kemia ili kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia ili kufikia malengo yao ya ufaulu.

Shule hiyo yenye wanafunzi 825 changamoto kubwa imetajwa kuwa kwa walimu wa Fizikia na Hisabati hali ambayo husababisha wakati mwigine wazazi kuchangia kiasi kdogo cha fedha ili kuajiri walimu wa muda wa kufundisha masomo hayo

Wakizungumza wakati wa kupokea meza na viti 100 kutoka kwa Mbunge wa Moshi Mjini, Priscus Tarimo, wanafunzi hao wamesema kukosekana kwa walimu wa Sayansi kumewafanya kusoma katika mazingira magumu.

Akitoa taarifa Mkuu wa Shule hiyo, Charles Mkenda amesema wanakabiliwa na changamoto mbalibali na kwamba ukosefu wa walimu wa Sayansi umekuwa kikwazo kikubwa kwa wanafunzi wanaosoma masomo hayo na kwamba kuna wakati hulazimika kuchangisha wazazi ili kuajiri walimu wa muda

Alisema changamoto nyingine ni upungufu wa viti na meza, uchakavu wa miundombinu ya baadhi ya madarasa na kutokamilika kwa uzio na kwamba utatuzi wa changamoto hizo kutaboresha mazingira ya ufundishaji na kujifunza.

“Hapa tumepata meza na viti 100, tunamshukuru mbunge wetu, kwani hii imepunguza upungufu uliokuwepo na sasa upungufu uliyobaki ni meza na viti 100, lakini pia tunaomba uzio wa shule umaliziwe ili kupunguza tatizo la utoro wa wanafunzi”.

Chanzo: Mwananchi
 
Tanzania hakuna tatizo la walimu mashuleni nipo tayari kutoa ushahidi mahakamani walimu wanarundikana sehemu moja kuna shule mwalimu kwa week ana kipindi kimoja tu na hata wakipangiwa wanahama wanarudi mjini tatizo lipo ila sio kwa ukubwa huo.
 
Mbna wameajiriwa wengi wa msingi huu mwaka.
Ndio ila Bado Kuna uhaba mkubwa sana,mfano shule za msingi kwenye kata ninayoishi Kuna shule mbili kila shule ina walimu 4,hizo nyingine 3 Zina walimu 6 kila Moja.
 
Tanzania hakuna tatizo la walimu mashuleni nipo tayari kutoa ushahidi mahakamani walimu wanarundikana sehemu moja kuna shule mwalimu kwa week ana kipindi kimoja tu na hata wakipangiwa wanahama wanarudi mjini tatizo lipo ila sio kwa ukubwa huo.
Kwa shule za sekondari nakubaliana na wewe ila shule za msingi kwenye hizi halmashauri za vijijini Kuna uhaba mkubwa sana hata ukiangalia shule zilizoko mjini karibu na halmashauri nazo Zina upungufu wa walimu.
 
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mji Mpya iliyopo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, wameiomba Serikali kuwapatia walimu wa masomo ya Sayansi pamoja na kuweka vifaa katika maabara ya Kemia ili kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia ili kufikia malengo yao ya ufaulu.

Shule hiyo yenye wanafunzi 825 changamoto kubwa imetajwa kuwa kwa walimu wa Fizikia na Hisabati hali ambayo husababisha wakati mwigine wazazi kuchangia kiasi kdogo cha fedha ili kuajiri walimu wa muda wa kufundisha masomo hayo

Wakizungumza wakati wa kupokea meza na viti 100 kutoka kwa Mbunge wa Moshi Mjini, Priscus Tarimo, wanafunzi hao wamesema kukosekana kwa walimu wa Sayansi kumewafanya kusoma katika mazingira magumu.

Akitoa taarifa Mkuu wa Shule hiyo, Charles Mkenda amesema wanakabiliwa na changamoto mbalibali na kwamba ukosefu wa walimu wa Sayansi umekuwa kikwazo kikubwa kwa wanafunzi wanaosoma masomo hayo na kwamba kuna wakati hulazimika kuchangisha wazazi ili kuajiri walimu wa muda

Alisema changamoto nyingine ni upungufu wa viti na meza, uchakavu wa miundombinu ya baadhi ya madarasa na kutokamilika kwa uzio na kwamba utatuzi wa changamoto hizo kutaboresha mazingira ya ufundishaji na kujifunza.

“Hapa tumepata meza na viti 100, tunamshukuru mbunge wetu, kwani hii imepunguza upungufu uliokuwepo na sasa upungufu uliyobaki ni meza na viti 100, lakini pia tunaomba uzio wa shule umaliziwe ili kupunguza tatizo la utoro wa wanafunzi”.

Chanzo: Mwananchi
Mnalazimisha watoto wengi kusoma science mwisho wa siku wanaangukia pia

Kungekuwa na utaratibu wa kubwa na wanafunzi wachache katika science
 
Kwa shule za sekondari nakubaliana na wewe ila shule za msingi kwenye hizi halmashauri za vijijini Kuna uhaba mkubwa sana hata ukiangalia shule zilizoko mjini karibu na halmashauri nazo Zina upungufu wa walimu.
Kwa utaratibu wa walimu kuhama ulivyo kwa sasa tatizo la watumishi haliwezi kuisha kuna shule mwalimu humuoni mwezi darasani yaani wapo wengi mpaka wana jipa likizo
 
Back
Top Bottom