Serikali yaanza majaribio ya mfumo mpya wa kufundisha kukabiliana na uhaba wa Walimu

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
21,838
38,729
SERIKALI imeanza majaribio ya mfumo wa ufundishaji mbashara ambao mwalimu mmoja anaweza kufundisha wanafunzi zaidi ya 1,000 kwa wakati mmoja.

Mfumo huo ambao kwa sasa unafanyiwa majaribio kwa baadhi ya shule za mikoa miwili ya Pwani na Dodoma, unamwezesha mwalimu kutoka kituo kimoja kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja wakiwa mikoa tofauti.

Utaratibu huo unaleta tafsiri ya kwamba mbali na kurahisisha utendaji kazi, pia ni njia mojawapo ya kukabiliana na uhaba wa walimu, hasa wa masomo ya sayansi shuleni.

Wakati serikali inaendelea na majaribio ya mfumo huo, wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaha wamesema mfumo huo utawasaidia kupata uelewa kwa wepesi na kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa.

#NipasheMwangaWaJamii #
 
Itakua online class tu. Watafaidika wanafunzi na walimu waliopo mjini tu.

Kuna uzi mmoja humu ulikua unaongelea "Umeshawahi kwenda mahali ukajiuliza hawa watu walifuata nini huku?"

Mmoja wa wachangiaji alisema wazi, kuna baadhi ya maeneo kuzaliwa tu ni advantage. Imagine kuna mtu kazaliwa Dar kasoma Dar primary hadi Advance alivo na kila upendeleo na anazidi kuongezewa Flyover, hafu kuna dogo amezaliwa bush mbaya anashare maji ya kunywa na ng'ombe.

My point, kuna wanafunzi wako vizuri sana uko vijijini mchawi ni opportunity. Sio kosa la wazazi wao kuwazaa vijijini ila serikali nayo ingewarahisishia life kidogo.

Sema nn, tuachane na hizi ngonjera, video ya Mapozi ya Blue Melody na Mondy imetoka.
 
Hili niliwahi kulileta humu, naona wamelifanyia kazi.....ukichukulia kwa masomo ya sayansi hasa A-level unakuta kuna shule hazina walimu, wanategemea jitihada za uongozi wa shule kutafuta mwalimu wa kuazima ambaye watamlipa na wanafunzi wenyewe kuhangaika kutafuta tuition.

Nafikri ingefaa waanze kwanza na shule za A-level, ingawaje wasiwasi wangu ni kwamba hao walimu ni kweli hawapo au serikali ndo haitaki kuajiri?
 
Eeee Tanzania yangu nini tumekosea hadi tunajikuta kwenye situation hii?,wenzetu wameshaingia kwenye mifumo ya kufundisha programmed, coding, robotics sisi ndio kwanza tunaingia kwenye matope, why na nani alibadilisha mfumo ule uliokua unatupatia waalimu bora wa science na maths kwa elimu ya msingi na sekondari?

Mkwawa CNE kila mwaka tulikua tunapata super teachers kama 100 kwa masomo ya secondary kwa combinations zote,kuanzia PC,PM,PG,CM,CB na grade 111A kwa primary schools,kenge gani alifuta hii,Marangu CNE super teachers wa English, Chang'ombe CNE kwa waalimu wa 111A (certificate)ku upgrade kwenda Diploma, systems safi na well oiled, sasa why wakavuruga mfumo huu?
 
SERIKALI imeanza majaribio ya mfumo wa ufundishaji mbashara ambao mwalimu mmoja anaweza kufundisha wanafunzi zaidi ya 1,000 kwa wakati mmoja.

Mfumo huo ambao kwa sasa unafanyiwa majaribio kwa baadhi ya shule za mikoa miwili ya Pwani na Dodoma, unamwezesha mwalimu kutoka kituo kimoja kufundisha wanafunzi wengi kwa wakati mmoja wakiwa mikoa tofauti.

Utaratibu huo unaleta tafsiri ya kwamba mbali na kurahisisha utendaji kazi, pia ni njia mojawapo ya kukabiliana na uhaba wa walimu, hasa wa masomo ya sayansi shuleni.

Wakati serikali inaendelea na majaribio ya mfumo huo, wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kibaha wamesema mfumo huo utawasaidia kupata uelewa kwa wepesi na kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa.

#NipasheMwangaWaJamii #
Serikali iko bize kwa vitu vya kijingajingaa...
🤬🤬😏😏
 
Back
Top Bottom