Kwanini Tanganyika Law Society isifutwe?

Kwanini Tanganyika Law Society isifutwe?

Sasa wewe mkuu ndugu yangu
Unataka kulinganisha uhai wa mtu na vitu vilivyoharibiwa vyenye thamani billion 125 (kwa mujibu wa Tume).
Unasahau kwamba hata mtu Moja tu Angeweza kumiliki kampuni inayoweza kulipa kodi serilikalini zaidi ya hiyo hera, ndiyo maana serikali haitaki yajirudie japokuwa wanajimwambafai ila ukweli wanaujua.
Huyu jamaa ni mpumbavu tu.

Analinganisha visivyolinganishika.
 
Utafuta vingapi au hujasoma katiba inasema kuhusu uhuru wa kutoa maoni, unapotoa hoja linganisha hiyo hoja yako kwa kutazama na nchi nyingine au na vyama vya sheria vya nchi nyingine kama Kenya au vile kutoka nchi za jumuia ya madola, tu wepesi sana kukalipia ila kukalipiwa hatutaki.
Haki yako itamezwa na haki ya wengi, dunia nzima iko hivyo. Huwezi kuchoma mali ya watu 70m hadi walioko tumboni eti kwasababu wewe ulienguliwa ugombea ubunge. Tz ina katiba halali kabisa, huwezi kuchoma nchi nzima eti kwasababu tu kuna watu hawataki kukusikiliza madai yako ya kutaka kubadili kifungu au katiba yote.
 
Ni jambo la hatari kwa taasisi ya umma kama vile Yanga, Simba, Tanganyika Law Society (TLS) au TFF kuchukua mwelekeo kamili wa kisiasa. Madhara yake ni makubwa sana. Na Unaweza kutambua uelekeo wa taasisi kwa kuangalia na kuwasikiliza viongozi wakuu wa taasisi husika.

TLS iliwahi kuongozwa na Mh. Tundu A. Lissu na sasa inaongozwa na Mh. Mwabukusi. Viongozi hawa kama ukiwasiliza na kuangalia utendaji wao wakiwa viongozi wakuu wa TLS utagundua kuwa wanaongea na kutumia lugha na tone ileile ya baadhi ya vyama vya siasa, kuonyesha kuwa TLS inaelekea kuwa chama cha siasa au inasaidia vyama vya siasa au imetekwa na vyama vya siasa au inatumiwa vibaya na vyama vyaa siasa.

Pia soma Pamoja na Mapugufu Yake ya Kibinadamu Wito Wanasheria Wote, Kwenye Hili, Tusimame na Rais Wetu wa TLS Wakili Boniface Anyisile Kajujumele Mwabukusi

Matukio ya October 29 yalinishitua sana kuona msimamo wa TLS imekataa kulaani uharibifu wa mali za watanzania kama vile barabara, vituo vya polisi, TRA, mahakama, hospitali, sheli, magari, maduka, ofisi za serikali, nk. Mali ambazo chimbuko lake ni kodi za watanzania wote, misaada, mikopo na juhudi za watu binafsi. TLS ilisimama moja kwa moja upande ule wa watu wachache walioharibu mali za watu wengi sawasawa na upande uleule waliosimama chama cha siasa cha chadema.

Kama TLS haiwezi kutetea uharibifu wa mali (barabara, reli, ofisi za umma, polisi) za watanzania wote (65m) zinazotumiwa na watanzania wote 65m wenye vyama na wasiokuwa na vyama, watoto, wazee, wajane, walemavu, wanaume na wanawake dhidi ya kikundi cha watu wachache wenye hasira na wanaodai haki yao ina faida gani kuwepo ndani ya jamii yetu?

Je, kuna sheria inayomruhusu mtu kama akiwa amekasirika au kudai haki yake kujichukulia sheria mkononi? Je, hasira ni kinga wakati wa kutenda kosa? Je, kudai haki yako ni kinga wakati wa kutenda kosa? Yaani kama mtoto akidai haki yake kwa baba yake anaweza kumlawiti baba yake ili ampe haki yake bila kuwa na hatia?

Kwanini TLS haihangaiki na wale walioharibu mali za umma na watu binafsi kwa kisingizio cha hasira na kudai haki? Je, TLS ni chama cha siasa?

Je, kudai Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kunahalalisha wanaodai kuchoma mali za watanzania wote? Kwanini TLS haisemi kitu kama vile nao ni sehemu ya madai?

Kwanini Tanganyika Law Society kisifutwe kama kimepoteza uelekeo wake?
Umeandika ujinga tu. Kwa hiyo wewe na hao wauaji wenzako mali ina thamani kuliko uhai wa wale mliowaua siyo! Ndiyo maana na nyinyi mkifa watu wanashangilia.

Halafu ungekuwa una akili ya kufikiri ungegundua kiini hasa kilichosababisha watu kuingia barabarani na kufanya ule uharibifu. Ni bahati mbaya sana wewe na hao wenzako hamna hiyo akili! Na ndiyo maana hadi leo mnaendelea kukaza mafuvu yenu.
 
Sasa wewe mkuu ndugu yangu
Unataka kulinganisha uhai wa mtu na vitu vilivyoharibiwa vyenye thamani billion 125 (kwa mujibu wa Tume).
Unasahau kwamba hata mtu Moja tu Angeweza kumiliki kampuni inayoweza kulipa kodi serilikalini zaidi ya hiyo hera, ndiyo maana serikali haitaki yajirudie japokuwa wanajimwambafai ila ukweli wanaujua.
Kama ukiwaza hivyo basi walinzi wa Bank na wanaosindikiza magari yenye fedha wasingepewa bunduki zenye risasi, wangepewa fimbo tu za kimasai tu na viwembe. Unaongea upuuzi, wewe unadhani kama wasingeminywa kama vile walipanga kuchoma nini na nini wapi hadi wapi vyenye gharama kiasi gani?. Na wakati mwingine huwa hatujali gharama ambayo wangetupatia watanzania bali huduma ambazo tungezikosa. kuna watoto walikufa kwa kushindwa kufika hospitali, wengine hawakwenda shule, viwanda vilifungwa, bandari haikufanyakazi, nk ni matriolion ya hela sheikh. Bora walivyominywa.
 
Matukio ya October 29 yalinishitua sana kuona msimamo wa TLS imekataa kulaani uharibifu wa mali za watanzania kama vile barabara, vituo vya polisi, TRA, mahakama, hospitali, sheli, magari, maduka, ofisi za serikali, nk. Mali ambazo chimbuko lake ni kodi za watanzania wote, misaada, mikopo na juhudi za watu binafsi.
je hivi ni vya thamani zaidi ya maisha ya Watanzania wengi waliouawa bila kosa lolote?
 
Umeandika ujinga tu. Kwa hiyo wewe na hao wauaji wenzako mali ina thamani kuliko uhai wa wale mliowaua siyo! Ndiyo maana na nyinyi mkifa watu wanashangilia.

Halafu ungekuwa una akili ya kufikiri ungegundua kiini hasa kilichosababisha watu kuingia barabarani na kufanya ule uharibifu. Ni bahati mbaya sana wewe na hao wenzako hamna hiyo akili! Na ndiyo maana hadi leo mnaendelea kukaza mafuvu yenu.
Hakuna sababu yoyote itakayohalalisha watu wachache wachome mali ya watanzania 70m. Yaani kama mimi ninakudai 20,000 hutaki kunilipa utakuwa radhi kuniona naichoma moto nyumba yako na kumbaka mkeo ili unilipe deni langu? Utaniacha hivihivi nambaka mkeo kisa nakudai? usiseme upuuzi.
 
je hivi ni vya thamani zaidi ya maisha ya Watanzania wengi waliouawa bila kosa lolote?
wewe hukuuliwa kwakuwa hukwenda kuchoma TRA. Watoto wa Lissu na Lema na heche na mwabukusi na Kibatala na Nshala hawakuuliwa kwakuwa hawakushiriki kwenye uchomaji wa sheli za watu. Ni watoto wa wajinga na watukutu tu ndio walishiriki hivyo kuuliwa kwenye tukio.
 
Hakuna sababu yoyote itakayohalalisha watu wachache wachome mali ya watanzania 70m. Yaani kama mimi ninakudai 20,000 hutaki kunilipa utakuwa radhi kuniona naichoma moto nyumba yako na kumbaka mkeo ili unilipe deni langu? Utaniacha hivihivi nambaka mkeo kisa nakudai? usiseme upuuzi.
Inakuwaje unatoa mifano isiyo na uhalisia! Kuna mwandamanaji gani aliyembaka mke wako?

Niambie hapa kiini hasa cha yale maandamano kilikuwa ni kipi, na uniambie kama kina mashiko au la! Au uniambie kama wale waandamanaji waliamua tu kuingia barabarani na kuharibu hizo mali zenu.

Ni suala tu la muda kabla ya wananchi walio wengi kushangilia vifo vyenu.
 
Ni jambo la hatari kwa taasisi ya umma kama vile Yanga, Simba, Tanganyika Law Society (TLS) au TFF kuchukua mwelekeo kamili wa kisiasa. Madhara yake ni makubwa sana. Na Unaweza kutambua uelekeo wa taasisi kwa kuangalia na kuwasikiliza viongozi wakuu wa taasisi husika.

TLS iliwahi kuongozwa na Mh. Tundu A. Lissu na sasa inaongozwa na Mh. Mwabukusi. Viongozi hawa kama ukiwasiliza na kuangalia utendaji wao wakiwa viongozi wakuu wa TLS utagundua kuwa wanaongea na kutumia lugha na tone ileile ya baadhi ya vyama vya siasa, kuonyesha kuwa TLS inaelekea kuwa chama cha siasa au inasaidia vyama vya siasa au imetekwa na vyama vya siasa au inatumiwa vibaya na vyama vyaa siasa.

Pia soma Pamoja na Mapugufu Yake ya Kibinadamu Wito Wanasheria Wote, Kwenye Hili, Tusimame na Rais Wetu wa TLS Wakili Boniface Anyisile Kajujumele Mwabukusi

Matukio ya October 29 yalinishitua sana kuona msimamo wa TLS imekataa kulaani uharibifu wa mali za watanzania kama vile barabara, vituo vya polisi, TRA, mahakama, hospitali, sheli, magari, maduka, ofisi za serikali, nk. Mali ambazo chimbuko lake ni kodi za watanzania wote, misaada, mikopo na juhudi za watu binafsi. TLS ilisimama moja kwa moja upande ule wa watu wachache walioharibu mali za watu wengi sawasawa na upande uleule waliosimama chama cha siasa cha chadema.

Kama TLS haiwezi kutetea uharibifu wa mali (barabara, reli, ofisi za umma, polisi) za watanzania wote (65m) zinazotumiwa na watanzania wote 65m wenye vyama na wasiokuwa na vyama, watoto, wazee, wajane, walemavu, wanaume na wanawake dhidi ya kikundi cha watu wachache wenye hasira na wanaodai haki yao ina faida gani kuwepo ndani ya jamii yetu?

Je, kuna sheria inayomruhusu mtu kama akiwa amekasirika au kudai haki yake kujichukulia sheria mkononi? Je, hasira ni kinga wakati wa kutenda kosa? Je, kudai haki yako ni kinga wakati wa kutenda kosa? Yaani kama mtoto akidai haki yake kwa baba yake anaweza kumlawiti baba yake ili ampe haki yake bila kuwa na hatia?

Kwanini TLS haihangaiki na wale walioharibu mali za umma na watu binafsi kwa kisingizio cha hasira na kudai haki? Je, TLS ni chama cha siasa?

Je, kudai Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi kunahalalisha wanaodai kuchoma mali za watanzania wote? Kwanini TLS haisemi kitu kama vile nao ni sehemu ya madai?

Kwanini Tanganyika Law Society kisifutwe kama kimepoteza uelekeo wake?
Screenshot_20250729-090555~2.png
 
Taasisi za kitaaluma ziko nyingi; walimu, wafamasia, madakitari, wauguzi, wanahabari, nk wote wanavyo vyana vya kitaaluma, why TLS inatumika kama kono la chadema?

Hapa ni ama TLS ionywe, ifutwe au viongozi wajinga wachukuliwe hatua kali saaana ikiwemo kuondolewa kwenye uongozi na shirikisho ili waende wakawe huru kuendesha siasa kwenye vyama vya siasa kuliko kutumia TLS kama kichaka.
Screenshot_20260617-221102~2.png
 
Inakuwaje unatoa mifano isiyo na uhalisia! Kuna mwandamanaji gani aliyembaka mke wako?

Niambie hapa kiini hasa cha yale maandamano kilikuwa ni kipi, na uniambie kama kina mashiko au la! Au uniambie kama wale waandamanaji waliamua tu kuingia barabarani na kuharibu hizo mali zenu.

Ni suala tu la muda kabla ya wananchi walio wengi kushangilia vifo vyenu.
Hiyo haiwezi kutokea wewe na mimi tukiwa bado hai. usijidanganye aloo
 
Kuna Taasisi nyingi ambazo hazina maana zingefutwa kwanza hizo, siku zote tenda haki
 
Inakuwaje unatoa mifano isiyo na uhalisia! Kuna mwandamanaji gani aliyembaka mke wako?

Niambie hapa kiini hasa cha yale maandamano kilikuwa ni kipi, na uniambie kama kina mashiko au la! Au uniambie kama wale waandamanaji waliamua tu kuingia barabarani na kuharibu hizo mali zenu.

Ni suala tu la muda kabla ya wananchi walio wengi kushangilia vifo vyenu.
wewe na mimi na wa humuhumu mtandaoni tu, hebu nenda ukaandamane tuone!! Hata Lissu na Heche siku ya maandamano hawakwenda sembuse wewe na mimi. Walifanya kila mbinu siku ile wasishiriki moja kwa moja.
 
IF dem want to win the revolutiion
must win it with rastas..
cant win no other way
because if you win other way
YOU GONNA FIGHT AGAIN.

NESTA MARLEY.
 
Mwendokasi, TRA na polisi na ofisi za serikali ya mitaa sio mali ya CCM, ni mali ya watu wote, kuunga mkono watu wanaochoma mali kama hizi ni uhalifu. Hakuna chama cha siasa kitakachoingia madarakani ambacho kitakuja na ofisi zake za serikali, vituo vya polisi wala barabara zake. Kuzichoma moto kwasababu ya kutafuta haki na maisha bora ni zaidi ya usaliti kwa watanzania na taifa. Unaturudisha nyuma miaka mingi sana kutoka hapa tulipo. TLS inaunga mkono watanzania kurudi nyuma kwa miaka mingi.
Kwani Frelimo na ANC nk walipokuwa wanapigania demokrasia walikuwa wanalipua mali za chama cha Makaburu cha National party peke yake? Hapo bwana linakuwa suala la ukimwaga mboga namwaga ugali. CCM wasipotaka haya yote wakubali usawa wa uwanja wa kuchezea na wapinzani. Hali iliyopo inaweza kuharibika hata zaidi
 
Sheikh mwaipopo namuelewa kwasababu ameamua kusimama upande wa watanzania 65m wakiwemo watoto na walemavu ambao wanatumia barabara hizo zilizochomwa kwenda hospitali na vituo hivyo vya polisi vilivyochomwa wanavyotumia kutoa taarifa wanapolawitiwa au kutendewa mabaya. TLS wanasema ilikuwa sawa kuchomwa moto na wachache wenye malalamiko yao.
Hajasimama upande wa Watanzania kwani hata sampling tu ya Watanzania walivomshambulia kwa upumbavu ule alioropoka ilidhihirisha kuwa kauli zake za ki-terrorist Watanzania wamezikataa na kuzipinga tofauti na za viongozi wa TLS ambazo zaidi ya kukinzana na chawa wa mafisadi huwa zina support kubwa ya Watanzania wasio affiliated na mambo ya vya siasa.
 
Mkuu, hoja yako ni nzito na inagusa masuala ya msingi kuhusu mustakabali wa nchi yetu na wajibu wa taasisi kama TLS. Hata hivyo, ili kuweka mizani sawa ya kisheria na ukweli wa mazingira uliopo, naomba nikujibu kwa hoja zifuatazo:

1. Kuhusu Kujichukulia Sheria Mkononi, Hasira, na Kinga ya Kosa
  • Hakuna sheria inayoruhusu kujichukulia sheria mkononi: Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya Tanzania (Penal Code, Sura ya 16) haitambui hasira au madai ya haki kama sababu ya kuhalalisha uharibifu wa mali, fujo, au fujo za kiraia.
  • Hasira si kinga ya kisheria (Defense): Kisheria, hasira (provocation) inaweza tu kutumika mahakamani kupunguza ukali wa adhabu au kubadili mashtaka (kama kutoka mauaji ya kukusudia kwenda mauaji ya bila kukusudia), lakini haiondoi kosa la jinai.
  • Kudai haki hakuhalalishi uhalifu: Mfano ulioutoa wa mtoto kumlawiti baba yake ili kudai haki ni kosa kubwa la kijinai la ulawiti. Kisheria, nia njema au madai ya haki hayawezi kusafisha au kuhalalisha kitendo ambacho chenyewe ni haramu (Illegal means cannot justify a legal end).

2. Kwanini TLS Haihangaiki na Walioharibu Mali? Je, ni Chama cha Siasa?
  • Wajibu wa Ulinzi ni wa Dola, si wa TLS: TLS haina mamlaka, silaha, wala askari wa kuzuia uhalifu mitaani. Kazi ya kukamata, kuchunguza, na kuwashtaki watu walioharibu mali za umma au za binafsi ni jukumu la kisheria la Jeshi la Polisi na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (DPP).
  • Kwanini TLS isilaumiwe kwa uharibifu huo: Serikali na vyombo vya usalama vilikuwa na taarifa mapema kuhusu maandamano ya tarehe 29. Kazi yao ya kisheria ilikuwa ni kulinda raia na mali zao, jukumu ambalo walishindwa kulifanikisha. Badala yake, walichochea vurugu zaidi pale walipoanza kutumia nguvu kubwa kupita kiasi (unproportional force) dhidi ya waandamanaji wa amani.
  • Ujipenyezaji wa wahalifu kwenye maandamano: Waandamanaji walikuwa na nia ya msingi ya kuandamana kwa amani. Hata hivyo, katika mkusanyiko mkubwa wa watu, ni kawaida kwa wahalifu (opportunists) kujipenyeza na kufanya uharibifu. Viongozi wa TLS hawakuunga mkono uhalifu huo, lakini huwezi kuilaumu TLS kwa kufeli kwa mifumo ya ulinzi ya serikali yenyewe.
  • TLS si chama cha siasa: Tanganyika Law Society ni taasisi ya kitaaluma iliyoundwa kwa Sheria ya Bunge (TLS Act, Sura ya 307). Inajumuisha mawakili wote wa Tanzania Bara wenye itikadi tofauti za kisiasa. Hata hivyo, viongozi wake binafsi wanapokuwa na mielekeo ya wazi ya kisiasa, inaweza kuleta picha ya taasisi hiyo kuegemea upande fulani, jambo linalohitaji marekebisho ya kiutaratibu ili kulinda weledi lakini si kuifuta taasisi.

3. Je, Kudai Katiba Mpya Kunahalalisha Uharibifu wa Mali?
  • Uharibifu hauhalalishwi: Madai ya Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ni haki za kisiasa na kiraia zilizolindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Kifungu cha 18 na 20 kuhusu haki ya kutoa maoni na kukusanyika). Hata hivyo, haki hizi lazima zitekelezwe kwa amani.
  • Msimamo wa TLS na Uhitaji wa Kauli Yenye Mizani: TLS inasimamia utawala wa sheria na mabadiliko ya kisheria. Hata hivyo, ili kulinda hadhi yake na kuzuia hisia za upendeleo, taasisi hii inapaswa kutoa matamko yenye mizani (balanced statements)—kwa kulaani matumizi ya nguvu kubwa ya polisi na wakati huo huo kulaani vikali uharibifu wa miundombinu unaofanywa na wahalifu wanaojipenyeza.

4. Kwanini Tanganyika Law Society Kisifutwe?
  • Umuhimu wa Kisheria: TLS haiwezi kufutwa kirahisi kwa sababu ni chombo cha kisheria (statutory body). Kufutwa kwake kunahitaji Bunge la Tanzania kufanya marekebisho au kufuta kabisa Sheria ya TLS (TLS Act).
  • Njia Mbadala za Kurekebisha Uelekeo: Badala ya kufutwa kwa taasisi nzima, njia sahihi za kisheria na kidemokrasia ni wanachama (mawakili) kupiga kura kuwaondoa viongozi wanaoonekana kuingiza ushabiki wa kisiasa, au Bunge kuweka masharti magumu yanayozuia viongozi wenye nafasi za wazi za kisiasa kuongoza TLS ili kulinda uhuru wa taasisi.

HITIMISHO: NJIA YA UPONYAJI WA KIDONDA CHA OKTOBA 29 NA MASHARTI YA MARIDHIANO
Mkuu, uponyaji wa kweli wa kidonda hiki cha kitaifa hautapatikana kwa maneno matupu au kwa kuilaumu TLS pekee, bali kwa vitendo thabiti vya uwajibikaji na haki kutoka kwa serikali. Ili kujenga msingi madhubuti wa amani na kuwasihi wananchi na serikali kukaa meza moja ya mazungumzo, lazima kwanza hatua zifuatazo zichukuliwe:
  • Kuwataja na kuwashitaki wahusika wote: Watu wote waliohusika na mauaji ya raia pamoja na uharibifu wa mali za umma na za binafsi zilizotokea Oktoba 29 lazima watambuliwe, watajwe hadharani, na wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.
  • Kuwajibishwa kwa viongozi wakuu wa ulinzi: Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) lazima wawajibishwe mara moja kwa kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kikatiba ya kulinda raia na mali zao, na kwa kuruhusu matumizi ya nguvu kubwa yaliyochochea maafa.
  • Uchunguzi wa kina kwa vyombo vyote vya usalama: Wakuu wote wa vyombo vya usalama waliosimamia operesheni hiyo—wakiwemo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kama itagundulika walihusika—lazima wachunguzwe kwa kina na wale watakaobainika kukiuka sheria wafunguliwe mashtaka ya kijinai.
  • Ufariji na fidia kwa wahanga: Serikali lazima itenge fungu maalum la bajeti kwa ajili ya kulipa fidia stahiki kwa familia za waliouawa na kwa wale wote walioumia au kupoteza mali zao katika machafuko hayo.
  • Kukabidhi miili iliyozikwa holela: Miili yote ya waliopoteza maisha ambayo ilizikwa kwa siri au holela na vyombo vya serikali lazima ifukuliwe na kukabidhiwa rasmi kwa familia zao ili izikwe kwa heshima na utu.
  • Serikali ikiri makosa yake kisheria: Serikali lazima ikubali wazi kuwa ilifanya makosa makubwa kuzuia maandamano, na ikiri kwamba haki ya kuandamana na kukusanyika kwa amani ni haki ya kikatiba ya kila mwananchi ambayo haipaswi kukandamizwa.
  • Kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya na Tume Huru: Kama sharti kuu la maridhiano ya kisiasa na kijamii, serikali lazima ikubali kuanzisha rasmi mchakato wa kupatana kwa Katiba Mpya pamoja na kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha haki, amani, na utengamano wa kudumu wa nchi yetu.
Hapo ndipo kidonda hiki kitapata uponyaji wa dhati. Mazungumzo kati ya serikali na wananchi hayawezi kufanyika juu ya misingi ya dhuluma na ukandamizaji; yanaweza tu kufanikiwa ikiwa sheria itachukua mkondo wake na haki kuonekana ikitendeka kwa usawa. Mabadiliko ya kweli yanatakiwa kuanza sasa ili kulinda amani ya nchi yetu.
 
Back
Top Bottom