Kwanini Simu za iPhone zina specifications ndogo?

Sasa kama huzipendi na “una uwezo wa kununua” si uachane nazo sasa. Endelea kununua samsung upate picha za kuuza sura insta. iPhone dont save garbage plus it’s security is high
Tatizo linakuja pale unapo nunua kofuli la milioni moja kufungia mali ya thaman ya laki 5.

Ina security kubwa lkn ulichokihifadhi ni kipi hasa??

Picha za uchi?
 
Uko sahihi bro. Yani mtu hata kuweka app ya Maswa yetu blog ni shida [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]

Wewe baki hukohuko kwenye Tecno hakuna haja ya kuja huku kampuni pendwa! Huku sio kila App inaingia tuu huku zinaingia app zenye ubora tuu, Pia tuna Security ya hali ya juu saana ! Hizo ineractions unazosema cjui bluetooth, pc mpaka itunes hizo ndo zinaua tecno zenu mnaingiza mavirus bila kujua ndo maana huku wamezj limit kwa usalama hutokuja kusikia milele iphone imestack, iphone imezima ghafla, iphone imeungua wakati wa kuchaji, cjui message hazijngii kisa insufficient storage, mara unagoogle kitu linafunguka li page lingine limeandikwa redirect [emoji23][emoji23] hizo shida huku iphone hatuna! Lock tu ya kawaida walishindwa FBI kuitoa, ila tecno lock tu hata mm naitoa naizima naiwasha huku nimehold power button na volume button then na restore mchezo unaisha huku kwetu ukiibq iphone ina lock aisee kauze kioo maana hakuna kitu utafanya
 
Utakuwa umeshindwa kuelewa statement. Iphone is worth the money you paid for, from hardware to software.

Huo mfano wako wa gari, mwenye premio mbona hasemi anatumia mda gani kufika hio safari ya 500km?
Kigezo chako wewe ni mafuta tu kwenye gari?
Mkuu na hizi torch barabarani mbona mtafika sawa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],

Kinachoiweka Iphone sokoni ni security tu. Lkn mimi sina cha kuficha sanaa,

Siwezi nunua kofuli la milioni moja kuficha mali ya laki 5
 
Security unaficha nini???????

Picha za uchi?????

Mana watu wanakomaa na security lkn ukiangalia anachokificha hakuna.
 
Umenena vyema Mwalimu!

Kitu kingine cha kuongelea ni kwamba Apple wao wameweza kuoptimize OS yao na Hardware i.e. iOS imetengenezwa kufit processor, gpu, na RAM management. Hii inapelekea kuwa na uwepesi na speed convenience kwenye kufungua na kutumia apps na games.

Shida ya Android ni kwamba ni mfumo wazi ambao hata wewe ukitaka utaweza download na kuedit unavyotaka (Open Sources OS). Kila kampuni inayotumia Android (unless unaongelea Android One) inai'customize Android OS ili kujiweka tofauti na makampuni mengine. Na hii wanafanya kwa kuweka skins (mabadiliko ya kimuonekano na matumizi) zao juu ya Android OS. Na zaidi ya hapo wanajaza bloatwares (apps zao ambazo unalazimishwa kuwa nazo hata ka huzitumii). Sasa hii ndo inapelekea mara nyingi kwa uzoefu wangu, kwa simu za Android in the long run kuanza kuchoka na kuwa slow hata kama uliinunua ikiwa na RAM 4Gb, octa core processor, n.k...

Na kwenye RAM pia teknolojia iliyotumika inamata wazee. Alichosema jamaa ni kweli, RAM za DDR4 zina clock speed kubwa sana lakini ni ghali kuliko hizi za DDR3 ambazo ni bei nafuu lakini clock speed ziko chini (sio chini kiviile, ila inaweza kuwa 30% chini ya DDR4). Sasa ndo unakuta RAM kuubwa lakini we jua tu teknolojia iliyotumika ndo iko nyuma.

Ila kwenye customization na uwezo wa mtumiaji kutumia kifaa to the fullest, asee Twende mbele turudi nyuma, Apple hawezi mkutia Android hata siku moja na ndio maana Android ndio Operating System yenye Market Share kubwa kuliko iOS.

Ila tukirudi kwenye security issues, tuwe wakweli, Android inaongoza kwa kuwa na udhaifu sana kutokana na Nature yake ya kuwa Open Source system na watumiaji wake wengi kutokuwa waangalifu na vitu wanavyoweka kwenye simu zao. Hapa Apple yuko vizuri.

Na kwenye suala la ubunifu, Apple kidogo wako nyuma. Inawachukua muda mrefu kidogo kuja na kitu kitakachoshangaza watu. Na vifaa vyao vingi wanasource toka kwa makampuni yanayotumia Android mfano. Camera sensor toka kwa Sony, screen tech ya Samsung, etc.

Binafsi ni mtumiaji wa Android, ila kimtizamo naona kila upande una ubora wake na mapungufu yake na kila Team ina haki ya kutetea upande wake.
 
Kuna simu zina itwa oppo...one plus...google nexus... aisee ni kiboko
One Plus a.k.a the Flagship Killer. Na kitu U Huawei P20 Pro hadi leo hakuna smartphone yenye kamera kali kama ya P20 Pro!
Binafsi napenda sana hawa underdogs. Pamoja na mapungufu yao, wanajitahidi sana kwenye Research & Development kitu ambacho kinafanya wanakuja na high-end specs at the fraction of what Flagship phones may cost.
Sasa kuna Xiaomi Poco F1, simu ina high-end specs at only $299!. Hii kuna analyst mmoja aliipa jina Flagship-killer Killer coz imeleta unafuu wa bei zaidi ya OP6 yenyewe.
 
Mwenzenu nilianza kutumia simu ya mwanzo ya smartphone Ya HTC Z710e hii simu niilipenda sana kwanza picha zake zipo clear sana ilikuja ikaharibika nikaipeleka kwa fundi ikawashinda Kuna day fulan nilipata safar na nilisafiri nayo nikaipeleka unguja darajan ilikubali vizur tu.

Nikiindoka tz na kuja nchi jiran tu nikaamua kuiuza baada ya kutoka hapo nikadandia kwenye Samsung Note 2 kwakweli nilifurahia sana na manjonjo yake. Nikauza nikaingia kwmeyw Motorola pia nayo nikauza nimerudi kwenye Samsung na ndio nitakayokomaa nayo mpk kieleweke.

Samsung wako vizur sana.
 
Apple kinachomfanya akae sokoni ni ile iCloud basi.
Siyo kweli maana apple ndiye aliyemwondoa Blackberry kwenye peaka ndiye aliye change mwelekeo wa simu na wakati huo hakuwana na icloud.
Na hata ingekuwa ni kweli basi mpe credit kwa kuwa na innovation ya security ambayo ni unbeatable japo katika technology, hakuna ulinzi ambao unaweza ni 100% secure.
 
Tatizo linakuja pale unapo nunua kofuli la milioni moja kufungia mali ya thaman ya laki 5.

Ina security kubwa lkn ulichokihifadhi ni kipi hasa??

Picha za uchi?
Siyo kuficha tu hata mtu akiiba asiitumie ina discourage wizi,
Au uweze kuitrace via icloud iwapo ataiweka heani
Au data zako ziwe safe, mtu kwenye simu anaweza kuwa confidential business emails, family messeges, private pics,
Unakumbuka ile scandal ya wanafunzi wa sauti wakina Nsia na picha za uchi kusambaa? Unajua ilianza kwa kuchua laptop wakampatia fundi awapigie windows akazikuta na kuzihamisha akaanza ku wa blackmail? Sasa imagine unapoteza simu mtu anaiokota anakuta kuna picha zako za ajabu, lazima akublackmail.
 
Ni kweli kabisa mkuu
 
Mkuu na hizi torch barabarani mbona mtafika sawa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23],

Kinachoiweka Iphone sokoni ni security tu. Lkn mimi sina cha kuficha sanaa,

Siwezi nunua kofuli la milioni moja kuficha mali ya laki 5
Kuna sehemu hakuna tochi. Uku Zanzibar nishatembea mashamba mengi, nimekuta tochi mbili tu, ikienda kaskazini kusini kweupe kuchana ikienda kusini kaskazini moto bati tu. Vile vile comfortability ya gari nayo na maisha ya engine. Huwezi kufananisha Brevis na premio ikiwa wewe si mtumiaji wa IST na hivi vi baby walker. wanaoendesha gari wanajua gari sio unywaji wa mafuta tu.

Kama kwenye maisha yako yote utakuwa na laki tano tu ya kuilinda sawa usinunue kufuli ya milioni moja, ila kama unategemea ziongezeke zaidi, ni muhimu kutafuta nzuri hata kama milioni 2.

JUST FYI security matters alot. Facebook juzi kati tu hapo kaingia matatizoni kwa sababu ya kuuza data za watu. wakati wewe unaona haisaidii kitu chochote facebook kushare ulipo, wanaojua maisha wanajali na wanaposikia information zao zimekuwa leaked wanafikia hata kuishitaki kampuni. Faceboo na kina google wanatendezea millions of money through your data.

Apple sio nzuri kwenye security tu, i think huijui iphone. Iphone ina best software and hardware integration na ndio maana unaiona iko smooth. Features zake usable unlike samsung, gesture controls, nambie ushawahi kumuona mtu anapokea simu bila kuigusa samsung yangu? useless features anaongoza samsung.

Why would you spend 1 million on samsung while you can spend less and enjoy the same version of Oreo? 😀
 
Kwani kama Android ina password na mtu akaiba au kuokota ataweza kuifungua?
 
Kwenye camera naona kama iPhone wapo kawaida sana labda sijakutana na iPhone zenye quality. Nnachokiona wapo vzr ni kwenye security tu labda na kutostuck ukiwa unafanya kazi zako ila mengine ni kawaida sanaaa
 
Hata iphone 6 ina latest version ya ios why unaspend kununua iphone 6s, 7 ama 8?
 
Oppo ni simu nzuri nasikia ila wengi hatujazishtukia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…