Umenena vyema Mwalimu!
Kitu kingine cha kuongelea ni kwamba Apple wao wameweza kuoptimize OS yao na Hardware i.e. iOS imetengenezwa kufit processor, gpu, na RAM management. Hii inapelekea kuwa na uwepesi na speed convenience kwenye kufungua na kutumia apps na games.
Shida ya Android ni kwamba ni mfumo wazi ambao hata wewe ukitaka utaweza download na kuedit unavyotaka (Open Sources OS). Kila kampuni inayotumia Android (unless unaongelea Android One) inai'customize Android OS ili kujiweka tofauti na makampuni mengine. Na hii wanafanya kwa kuweka skins (mabadiliko ya kimuonekano na matumizi) zao juu ya Android OS. Na zaidi ya hapo wanajaza bloatwares (apps zao ambazo unalazimishwa kuwa nazo hata ka huzitumii). Sasa hii ndo inapelekea mara nyingi kwa uzoefu wangu, kwa simu za Android in the long run kuanza kuchoka na kuwa slow hata kama uliinunua ikiwa na RAM 4Gb, octa core processor, n.k...
Na kwenye RAM pia teknolojia iliyotumika inamata wazee. Alichosema jamaa ni kweli, RAM za DDR4 zina clock speed kubwa sana lakini ni ghali kuliko hizi za DDR3 ambazo ni bei nafuu lakini clock speed ziko chini (sio chini kiviile, ila inaweza kuwa 30% chini ya DDR4). Sasa ndo unakuta RAM kuubwa lakini we jua tu teknolojia iliyotumika ndo iko nyuma.
Ila kwenye customization na uwezo wa mtumiaji kutumia kifaa to the fullest, asee Twende mbele turudi nyuma, Apple hawezi mkutia Android hata siku moja na ndio maana Android ndio Operating System yenye Market Share kubwa kuliko iOS.
Ila tukirudi kwenye security issues, tuwe wakweli, Android inaongoza kwa kuwa na udhaifu sana kutokana na Nature yake ya kuwa Open Source system na watumiaji wake wengi kutokuwa waangalifu na vitu wanavyoweka kwenye simu zao. Hapa Apple yuko vizuri.
Na kwenye suala la ubunifu, Apple kidogo wako nyuma. Inawachukua muda mrefu kidogo kuja na kitu kitakachoshangaza watu. Na vifaa vyao vingi wanasource toka kwa makampuni yanayotumia Android mfano. Camera sensor toka kwa Sony, screen tech ya Samsung, etc.
Binafsi ni mtumiaji wa Android, ila kimtizamo naona kila upande una ubora wake na mapungufu yake na kila Team ina haki ya kutetea upande wake.