Kwanini Simu za iPhone zina specifications ndogo?

Kwanini Simu za iPhone zina specifications ndogo?

Mzeee raia wana ipendea camera ya nyuma tu na kale ka apple pale nyuma basi lakin pale amna simu... ukitaka u enjoy chukua samsung s8
Yeap iPhone ni jina tu. Kwa matumiz hamna ktu, kwa anayeta simu nzur kuliko zote asubiri galaxy s10 yenye speed ya internet 5g cyo 4g tena, Real display fingerprint. Nk.
Samsung-s10-04.jpg
 
Kikubwa kinachofanya iphone ionekane ya matawi ya juu ni branding. Sehemu kubwa ya apple products wanauza brand. Na steve jobs alifanikisha hili through demand and supply but tangia afe iphone zimekua kama techno nowdays na feki nyingi sokoni. Hiki kitu pia huko nyuma kilifanikiwa na samsung kipindi hicho ambacho samsung zilikua hazi depreciate value but zinatoweka sokoni. Kipindi hicho ambacho nokia alie dominate soko lakin simu zake ndo baada ya muda imeshuka bei sababu ya matoleo mengi na wingi wa simu sokoni.

Kingine kikubwa kuhusu apple na hichi ndo kinafanya hadi leo simu zake ziomekane ziko juu and preferred by most people from officials to drug dealers and warlords nk ni swala la data security and privacy.
Hapa uta refer ile kesi ya FBI kutaka kufungua simu ya gaidi na apple wakagoma ikaenda mahakamani but waka rule in favor of na apple wakashinda.
Katk hii dunia ya sasa hivi most softwares zina back doors ambazo security agencies wanazitumia kua access anything in the name of national security.

So thats what apple is selling na sio swala la camera or other phone specifications coz samsung among other phones wanampita.
 
So which is which!? Samsung s6 edge or IPhone 6s!??......
Maana nashindwa fika conclusion hapa .....comments bado zinahitajika!! Nataka niingie shop nidake moja wapo.
 
Baki kwenye Tecno mzee,hii Dunia ina machaguo mengi sana hauwezi kuyafanya yote lazima utofautiane na wenzio tu.
Kwangu mimi iPhone ni tafsiri sahihi ya neno simu nina-enjoy kuliko unavyodhania kama vile matumizi ya simu yanavyotaka tatizo watu wengi ambao ni Android addict wanataka kugeuza simu kila kitu walale umo umo,simu ipike pilau,simu abandike maji ya kuoga yaani vurumai tupu ndio maana mnalalama kua iOS sio friendly ni mazoe yenu ya kuzoazoa.
Kwa hy mnapenda hizo simu zetu za kulala saa 2 km kuku sio??
 
Nimetumia 1phone 6+ kwa miezi 6 nikaona mauzauza tuu nikabadilishana na mtu TECNO CX, now nipo sumsung,
Watu wenye hizi simu wanaona ufahari sana kuanazo lkn nafsini mwao mungu ndio anajua.
 
Yaani ukimuona mtu anaongelea DUAL SIM CARDS kwenye Flagship smartphones halafu ni za big brand, ujue huyo ni mtumiaji wa hizi akina tecno, itel, mi, n.k

Nina asilimia kubwa, mtoa mada, hajawahi kutumia iphone, anaona tu watu wanatumia iphone. Ukishika iphone X mkononi tu unaelewa kama umeshika milioni 2 ivi, yaani ushike tu usiiwashe wala usiitumie, basi utakubali bei iko sawa. Shika Android sasa, cheap!
Kwa hiyo kauli ya sentesi ya mwisho unadhibitisha kabisa iphone sio nzuri kwa matumizi bali kua nayo tu ni unaonekana mtu,
Yaani hii nafananisha na mwenye gari premio na mwenye brevis zote speedmeter 180, mwenye brevis anajisifu gari yake inakimbia na ina nguvu lkn hakuambii kua kwa mwendo wa km500 anatumia fulltank2 wakati mwenye premio anatumia fulltank1
 
Wakuu habarini.
Naomba kujua kwann Iphones zina specifications ndogo ukilinganisha na Simu nyingine zote hata ambazo zinachipukia.

Sijaona Iphone inayozidi hivi vigezo

Maximum RAM 3gb
Maximum Camera 12 Mega Pixels
Maximum Battery size </ = 3000 mAh

Hawa jamaa Inovation yao ipo katika mlengo upi???.

Hizi simu sijawahi kuzitumia na nahisi sizipendi japo ninapesa ya kununua Iphone niitakayo. Lakini naona simu kama ya waganga wa kienyeji. Maana Masharti ni mengi kuliko Enjoyments.

Yani kumiliki hizi simu ni kama Mkinga mfanya biashara anaelala chooni ilihali ana majumba ya kifahari

1. No interaction with PC without Itunes
2. No Bluetooth compatibility with other devices except Its Generic Siblings
3. Kupata Apps za local developers ni Msala.
4. No downloading on Websites and blogs
5. Poor documents perusing and management
6. No memory extension.
7. Finger print zinakufa Ovyo kuliko simu zozote
8. Poorness of IOS Ecosystem
9. No access of payable services in some many regions ( Especially Africa)
10. Poor navigation of ( BACK ) Button
Sijui watu wenye Iphone huwa mna enjoy nini kwenye simu zenu.
11. No dual SIM
12. No File Management App
13. Safari si a default Browser no way ndugu yangu

Naomba ushirikiano
Tatizo ni pale mtu unapotumia iphone ukitaka i behave kama android wakati ni platform mbili tofauti, Landrover 110 ilikuwa haichambui oil wala mafuta inapiga kazi bila kuwasha taa ya check engine wala miss lakini haiifanyi iwe gari bora kuliko evoque inayochambua oil na mafuta.
Apple kwanza wana sera moja ya kujaribu kuzuia piracy kuanzia kazi za wasanii mpaka apps za developers ndiyo maana wanazuia kudownload ovyo ovyo vitu vya watu na apps zao.
Pia kupitia kudownload na kuweka vitu via njia maalum ni ulinzi tosha dhidi ya wadudu na hacking ndiyo maana appstore haina apps ambazo ni takataka kama google play kuna kila utitiri wa apps za ovyo.
Local developers hawajazuiwa kuweka apps appstore ila wanahitajika kulipa fees na itachekiwa kabla ya kuruhusiwa ilil linafanya mtu awe serious mtu hawezi kudevelope ujinga ujinga akaweka wakati itamcost kulipia lazima aweke kitu cha maana.
Hawaruhusu memory expansion kwasababu memory stick nyingi ni fake ni zinafanya simu ziwe slow zinakwasababu ya slow reading and writting speed.
Unapoongelea econsystem una maana gani? ios ina ecosystem safi kabisa kuna interaction kubwa between ios na bidhaa nyingine za apple kuanzia smart watches zao, tvs, mac os driven devices na icloud based services zao sasa sijui unaongela nini. Unaweza fanya kazi kwenye mac ukaja iendeleaza kwenye ipad au simu kwasababu zina sync automaticcally.
Navigation yake iko poa sana unless we ni mgeni au mtumiaji amekariri, jambo moja ambalo lilifanya ios iwapiku wengine hata mac os ni kuwa na simple and friendly user interface sema watumiaji wa tanzania wamekariri wanataka kila kitu kiwe kama walivyozoea ndiyo maana hata windowsa alipata shida kuwahamisha kutoka start button.
Dual sim card za nini tazama apple kalenga market ya wapi.
kuhusu ram, ios iko smooth hahitaji ram kubwa ku run smoothly kuna simu za android zina ram mpaka 6gb lakini sinachelwa kuwaka na zina rug wakati iphone kustack ni nadra na apple hana tabia ya kuweka vitu ambavyo havina maana kwenye gadgets zake sa akuwekee ram 5gb wakati ios hahitaji hiyo ku run smoothly atakuwa na maana gani? In future may ikitoka ios 16 huko huenda itahitaji ram 5gb.
megapixel tu hazi determine ubora wa picha itakayopigwa na simu, ubora wa picha unakuwa determined na vitu vingi ndiyo maana iphone 4 ilikuwa na migapixel 5 lakini ilikuwa na picha bora kuliko sim nyingi zenye megapixel nyingi.
Yah safari ni default browser, hii setback na mtu wakati wanunua iphone jua ni ios siyo android kama wataka kitu kinachokupa uhuru nunua android sasa unanunua kitu ukijua kina limitations halfu later unalalamika utakuwa mwehu.
 
As far as specification Apple wapo pande mbili kuna vitu wapo vizuri zaidi ya competition na kuna vitu wapo ovyo. Mfano.

1. Soc yao kwa sasa ndio best sokoni hakuna simu yenye processor yenye nguvu kushinda iphone japo kwenye gpu bado qualcomm yupo juu na mambo mengine kama modem na wifi anapitwa na simu za android.

2. Usiangalie tu ukubwa wa ram nipo radhi nitumie simu ya 2gb ram yenye dual chanell na ddr4 memory zenye speed kuliko simu ya 4gb ama 8gb ram ambayo ni single chanell na ram za ddr2 ama ddr3 zenye speed ndogo. Zipo simu zenye ram nzuri zaidi ila iphone zake pia sio mbaya zinapita hizi ram kimeo za kichina. Ukumbuke simu gpu yake inatumia ram ya simu hivyo jinsi ram ya simu ilivyo fasta na ndio apps na games zitarun smoothly.

3. Pia megapixel kwenye camera humaanisha ukubwa wa picha na sio quality. Dslr camera kali unaweza kuta ni 8mp tu. Kifupi kuchukua content za 4k inahitajika mp 8 tu. Ambayo kwa sasa ndio vifaa vya kisasa kama tv na pc vinaitumia. Quality ya picha sana inasababishwa na sensor iliotumika pia kuna vitu kama software, ois, aperture, lens etc vinachangia.

Kuhusu mambo mengine nakubaliana na wewe Apple innovation yao ni ndogo sana na ukikuta kitu chao kizuri basi utakuta kina mkono wa kampuni nyengine mfano display za samsung, memory za smasung etc. Kifupi ana asemble vitu best toka makampuni mengine na sio mvumbuzi kama baadhi ya kampuni nyengine.

Kuhusu software na Ecosystem zao zimetengenezwa kwa watu ambao hawataki mambo mengi kwenye simu, upige simu utumie whatsapp na insta etc.

Ila ukitaka mambo makubwa zaidi vitu kama VR, casting, file management, etc ios si yako.
Nilikua nafuatilia nione coment yako chief, umenena kweli, wenye iphone wanajiona sana lkn ukweli haziwapatii kila wanachotaka.
 
Kwa hiyo kauli ya sentesi ya mwisho unadhibitisha kabisa iphone sio nzuri kwa matumizi bali kua nayo tu ni unaonekana mtu,
Yaani hii nafananisha na mwenye gari premio na mwenye brevis zote speedmeter 180, mwenye brevis anajisifu gari yake inakimbia na ina nguvu lkn hakuambii kua kwa mwendo wa km500 anatumia fulltank2 wakati mwenye premio anatumia fulltank1
Utakuwa umeshindwa kuelewa statement. Iphone is worth the money you paid for, from hardware to software.

Huo mfano wako wa gari, mwenye premio mbona hasemi anatumia mda gani kufika hio safari ya 500km?
Kigezo chako wewe ni mafuta tu kwenye gari?
 
Unataka maelezo yapi zaidi? Nakupa mfano simu mojawapo yenye camera kali kwa mwaka huu ni Huawei P20 pro, ina triple cameras zenye 40mp, 20mp na 8mp zenye aperture ya f/1.8, f/1.6 na f/2.4 respectively.
Hivyo hapo utaona kwamba camera yenye 1.6 ndo kali.
Hizo ni basics ambazo mimi huwa naangalia na zinasaidia kupata kilicho bora.
Wapenda selfie utawajua tuu
 
Back
Top Bottom