Mambo mabaya kwenye simu ambayo ulimwengu wa Tech unalazimisha tuone ni ya kawaida

Reuben Challe

JF-Expert Member
Dec 10, 2021
2,761
5,039
Source: Twitter

1. Notch kubwa kwenye iPhone
Screenshot_2023-07-24-13-23-58-964_com.android.chrome.jpg

Flagship za Apple kama iPhone X series, 11 series, 12 series na 13 series zimekuwa zikija na notch kubwa kwa juu kwenye display ambayo imekuwa ikizuia kuona sehemu kubwa wakati wa kuangalia video. Hata hivyo kampuni imekuwa ikifanya hivyo kuanzia mwaka 2017 hadi 2022. Ila at least kwa sasa iPhone 14 Pro Max imekuja kupunguza hiyo notch ambayo ilikuwa kubwa kwenye iPhone 13 series na wenzake

2. Baadhi ya midrange za Samsung kuja na chipset ambazo zipo behind competition
Screenshot_2023-07-24-10-58-38-493_com.android.chrome.jpg

Kwenye picha ni Samsung Galaxy A54, moja ya midrange bora zaidi kwa sasa. Simu hii inakuja na chipset ya Samsung Exynos 1380 ambayo ni weak kuliko wapinzani katika bei hiyo. Exynos 1380 ina matatizo ya overheating pia wakati wa kucheza heavy games. Wapinzani kama Google Pixel 7 na Xiaomi Poco F5 wanakuja na chipset zenye nguvu kushinda ya Samsung Galaxy A54
Kwa mfano Google Pixel 7 inakuja na Google Tensor G2 na Poco F5 inakuja na Qualcomm Snapdragon 7+ Gen 2 ambazo ni strong kuliko Samsung Exynos 1380 ya kwenye Galaxy A54

3. Xiaomi, Oppo, Vivo na One plus kuendelea kulimit selfie camera kwenye flagship zao kurekodi maxum 1080p video tu
Screenshot_2023-07-24-10-56-25-116_com.android.chrome.jpg

Screenshot_2023-07-24-10-41-29-728_com.android.chrome.jpg

Picha ya kwanza ni Xiaomi 13 Ultra(juu) na ya pili ni Oppo Find X6 Pro. Hizi ni miongoni mwa simu zenye kamera bora zaidi mwaka huu lakini cha ajabu ni kwamba kamera zao za mbele bado haziwezi kurekodi video za 4K@30fps, matokeo yake zinaishia 1080p tu.
Hata Samsung Galaxy A54 inarekodi 4K video kwenye kamera ya mbele. Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba hata midrange kutoka kwa Xiaomi wenyewe (Xiaomi Civi 3) inaweza kurekodi video za 4K kwenye kamera ya mbele ila flagship yao 13 Ultra haina uwezo huo.
Jambo jema ni kwamba kwa sasa Oppo wameshatoa software update ambayo imeongeza 4K video recording kwenye Oppo Find X6 Pro na pia Xiaomi 14 Pro inatarajiwa kuja na 4K selfie camera mwishoni mwa mwaka huu

4. Xiaomi kuchelewesha security updates kwenye baadhi ya models zake
Screenshot_2023-07-24-10-37-30-823_com.android.chrome.jpg

Kwenye picha ni moja ya models za Poco ambayo hadi sasa imeishia MIUI 14.0.2 update tu wakati simu kama Xiaomi Civi 1S imeshapata MIUI 14.0.9
Tabia hii inafanya baadhi ya watumiaji wa Xiaomi kuchelewa kuhamia kwenye new security update na hivyo kuleta kero. MIUI 14 imekuwa available tangu December mwaka jana lakini cha ajabu simu kama Redmi 9 zimekuja kupata MIUI 14 update kwenye hii miezi ya karibuni, na hii ni kwa sababu MIUI 14 Global ilichelewa kuwa released.
Wale wa Chinese version wanapata updates za haraka.
Jambo jema ni kwamba kuna feature kwenye simu za Xiaomi inayokuwezesha kupata updates za haraka sambamba na Chinese version

5. One UI kuwa nzito kwenye simu za low end
Screenshot_2023-07-24-13-32-06-786_com.android.chrome.jpg

Kwenye picha ni Samsung Galaxy A13, moja ya simu zenye UI nzito zaidi kwa sasa.
Samsung anajitahidi sana linapokuja suala la software quality kwa sababu software zao ni nzuri na zina features nyingi ambazo ni useful kwa matumizi ya kila siku na pia UI ikiwa na matatizo basi wanafix haraka kwa kupitia software update. Lakini kutokana na hii UI kuja na mambo mengi imefanya iwe UI nzito sana kuliko UI nyingine za Android.
Samsung pia amejitahidi kutumia One UI Core kwenye baadhi ya simu zake za low end ambayo imepunguzwa features nyingi ili walau iwe nyepesi.
Lakini bado simu kama Samsung Galaxy A13 zinashindwa kuhimili uzito wa One UI na kufanya iwe very sluggish. Features za muhimu za One UI kama multitasking hazifanyiki effectively kwenye low end kutokana na uzito wa UI na RAM ndogo.
One UI inafanya vizuri sana kwenye midrange na flagship zao. Aidha One UI Core inafaa zaidi kwenye low end

6. Midrange phones kutokuja na stereo speakers
Screenshot_2023-07-24-10-52-09-725_com.android.chrome.jpg

Kwenye picha ni Vivo V27, midrange nzuri kutoka kwa Vivo. Lakini jinsi kampuni hii ilivyo haina aibu wameamua kuweka speaker moja tu, matokeo yake imetoa unimpressive results kwenye gsmarena audio test.
Hata Redmi 10 inakuja na stereo speakers katika bei ya 370,000 tu ila hii simu kutoka kwa Vivo ambayo inakaribia milioni 1 hivi bado inatumia mono speaker.
Kwa sasahivi ni aibu kwa midrange kuja na mono speaker. Hata Samsung anayefahamika kwa bei za juu bado anaweka stereo speakers kwenye midrange zake, sijui Vivo V27 inakwama wapi

7. Simu kutokuja na chaja kwenye box kwa kisingizio cha kutunza mazingira
Screenshot_2023-07-24-11-23-03-409_org.videolan.vlc.jpg

Sony Xperia 1 V inakuja na simu tu ndani ya box. Hakuna kitu chochote kile zaidi ya simu. Labda kama utahesabia na pin ya kutolea line.
Samsung, Apple na Google nao hawaweki chaja kwenye box, wanataka utafute mwenyewe na bei ya chaja pekee inafikia hadi laki 1. Kisingizio chao kikubwa ni kwamba wanatuza mazingira
Flagship za China zinakuja na accessories za muhimu kama chaja kwenye box mfano Xiaomi 13 Ultra na Vivo X90 Pro Plus
Kitu kilichonishangaza zaidi ni kwamba hadi low end sasahivi zinaanza kuja bila chaja. Hapa ninailenga Xiaomi Redmi 12 moja kwa moja. Inasikitisha sana kuona hadi simu cheap kama Redmi 12 inakuja bila charger

8. Makampuni ku rebrand simu na kutumia SoC zilizopitwa na muda
Screenshot_2023-07-24-13-37-19-818_com.wiretun.jpg

Kwenye picha ni Redmi 12. Nadhani kama unaijua Redmi 10 basi utanielewa. Simu hizi ni simply rebranded Redmi 10 tena inakuja na downgrade kama mono speaker na poor night photography. Matokeo yake ni kwamba bado inaendelea kutumia chipset ile ile ya MediaTek Helio G88 wakati kuna chipset nyingi tu nzuri kwa sasa.
Plus bei yake inakaribiana na Redmi Note 12 kwenye sehemu nyingi kwa hiyo sioni sababu ya kununua Redmi 12 wakati Redmi Note 12 5G tayari ipo tena ina SoC nzuri ya Snapdragon 4 Gen 1

9. Kupuuzia matatizo yanayotokea kwenye specific models za simu na ku pretend ni matatizo ya kawaida tu
Screenshot_2023-07-24-10-38-24-840_com.android.chrome.jpg

Kwenye picha ni Samsung mojawapo ambayo imekutwa na tatizo la green lines kwenye OLED display. Tatizo hili limekuwa common kwenye baadhi ya models kama Samsung Galaxy Note 9, Samsung Galaxy S20+ na baadhi ya Vivo na One Plus lakini inaonesha watu hata hawajali, wanapretend kama ni normal issue kwa OLED display ku form green lines

10. Flagship za Samsung, Apple, Xiaomi, Oppo, Vivo, One Plus na Google kutokuja na 3.5mm jack
Screenshot_2023-07-24-11-22-29-578_org.videolan.vlc.jpg

Kwenye picha ni Sony Xperia 1 V. Ndio flagship ya maana inayokuja na 3.5mm jack kwa sasa. Hawa akina Samsung, Apple, Xiaomi na wenzake wameamua kuondoa kabisa 3.5mm jack.
Wanataka utumie wireless earbuds ambazo zinauzwa kwa bei ghali kuliko wired earphones, plus unapaswa kuzichaji kila zinapoisha chaji.

11. Samsung kutumia chipset za Exynos kwenye flagship zake za EU variant
Screenshot_2023-07-24-13-41-12-925_com.wiretun.jpg

Samsung Galaxy S22 Ultra inakuja na overclocked Snapdragon 8 Gen 1 lakini EU variant zinakuja na Exynos 2200 ambayo haiwezi kuwa nzuri kama overclocked Snapdragon 8 Gen 1 hata siku moja.
Jambo jema ni kwamba sasahivi wameamua kutumia Qualcomm Snapdragon 8 Gen 2 kwenye Samsung Galaxy S23 Ultra zote.

12. Flagship kuja na 128GB base storage
Screenshot_2023-07-24-11-21-26-141_org.videolan.vlc.jpg

Xiaomi 13 Pro, Samsung Galaxy S23 Ultra na iPhone 14 Pro Max zote hizi zinaanzia storage ya 128GB licha ya kuwa ni simu expensive.
Ingekuwa jambo la busara kama flagship zingeanza kuja na 256GB kama base storage mfano Xiaomi 13 Ultra.

13. Xiaomi imechelewa kuanza USB Type C 3.x, iPhone hadi leo hawajaanza hata kutumia
Screenshot_2023-07-24-13-45-21-332_com.miui.notes.jpg

Mwaka huu kwa mara ya kwanza ndio tunaona Xiaomi anaanza kutumia USB Type C 3.2 kwenye simu zake za Xiaomi 13 Ultra na tablets zake za Xiaomi Pad 6 na Xiaomi Pad 6 Pro. Pia Xiaomi Pad 6 Max iko mbioni kuja. USB Type C 3.x ni muhimu kwa sababu zinawezesha features za muhimu kama video out na faster files transfer.
USB Type C 3.x imewezesha flagship za Samsung kuja na feature ya Samsung DeX, kwa jina lingine inaitwa "Desktop Mode" ambayo imeimprove connection kati ya simu na kompyuta na ni useful kwa matumizi ya ofisini pia
Flagship za Motorola nazo zinakuja na feature kama hii ya Samsung DeX, kwenye Motorola inaitwa "Ready for" ila ndio feature ileile
iPhone hadi leo anatumia USB 2.0 na hatuoni dalili za kuhamia USB 3.2

14. Samsung, Apple na Google hawajahamia kwenye Super fast charging technology hadi leo
Screenshot_2023-07-24-14-54-16-295_com.android.chrome.jpg

Tumeona simu za China zenye uwezo wa kuchaji kutoka asilimia 0 hadi 100 chini ya dakika 30.
Mfano
*Xiaomi 13 Pro inatumia dakika 19 tu kwa kutumia chaja yake ya 120W
*Xiaomi Redmi Note 12 Discovery Edition inachaji kutoka asilimia 0 hadi 100 kwa dakika 9 tu kwa chaja yake ya 210W

Samsung Galaxy S23 Ultra inatumia approximately saa nzima kuchaji kwa chaja yake ya 25W
iPhone 14 Pro Max inatumia charger ya 27W na Google Pixel 7 Pro inatumia 23 W tu (kama nakumbuka vizuri)

Habari njema ni kwamba kuna rumours kwamba Samsung Galaxy S24 Ultra itakuja na 65W fast charger finally. Itakuwa ni improvement kubwa sana kwa simu za Samsung

Huko juu nilisema Source ni Twitter. Kuna mtu ametaka kujua exact source INGIA HAPA CHINI
Hii ndio source

Andika na source ya bandiko lako kwasababu umecopy na kupaste kama sio kutranslate

Uwe unachanganua kwanza usikae ukategemea iOS na Samsung walete Type C za USB kirahisi hivyo licha ya kukubaliana kwamba 2024 zote zitakua ni Type C
 
Hiyo haijawa copied wala pasted wala translated. Kuna mtu Twitter alitaja hizo point, yeye alitaja tu point bila maelezo. Hayo maelezo nimeyaandika mwenyewe na point nyingine nimeziongeza mwenyewe.
Pia mifano ya simu nimeitaja mwenyewe

Anyway itabidi nirudi Twitter nikaitafute hiyo Source nakuletea muda si mrefu usijali.
Kwanza huko juu nilishaandika Source ni Twitter kwa hiyo usije ukadhani sijui ni wapi ulikotoa hiyo point ya Copy na Paste

Halafu hiyo point yako inayofuata mbona sijakuelewa. Unasema niwe "nachanganua" Kuchanganua maana yake ni kufafanua, mbona nimeleta mifano na maelezo kabisa hapo juu, au kusoma ni shida? Unamaanisha Kuchanganua nini?
Halafu unasema nisitegemee kuona iOS na Samsung wanaleta USB Type C?????
Kwanza iOS ni operating system na Samsung ni simu, unaongelea mambo mawili tofauti. Pili Samsung tayari zinatumia USB Type C kwa hiyo sielewi unachokiongelea hapa.
Hapo juu imeongelewa USB Type C 3.x sasa sielewi nini hujakielewa.

Soma vizuri, ni aidha hujaelewa nini naongelea au ulisoma haraka ili uje kumuattack mleta mada

Source nimeshakuwekea
 
Kwenye hiyo Oppo Find X6 Pro kama selfie camera ilikuja bila 4K capability inakuwaje iwezeshwe na software update while 4K capability ni hardware based? Chief-Mkwawa
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kwenye hiyo Oppo Find X6 Pro kama selfie camera ilikuja bila 4K capability inakuwaje iwezeshwe na software update while 4K capability ni hardware based? Chief-Mkwawa
Vyote vyote mkuu, Hardware inatakiwa iwepo na software pia inahusika. Video ya 4k ni kama Megapixel 8 tu ukitoa Aspect ratio camera yoyote yenye MP 10 kuendelea inachukua 4k.

Camera za MP 8 zipo siku nyingi simu ya kwanza kuwa na MP 8 ilitoka 2008 ila ilichukua hadi 2013 simu kuanza ku record 4k.

So inawezekana hardware kuwepo kwenye simu halafu baadae mtengenezaji kupush software update na ku enable hio hardware
 
Kwenye swala la simu kuja bila charger utetezi wao sijawahi kuuelewa labda wangesema tu ni kujiongezea mapato.
Ukitoa Kampuni kubwa kubwa kama Sony, Apple ama Asus kampuni nyingi zinatumia Proprietary chargers, Chaja zao hazichaji simu nyingine na chaja yako ya Nyumbani haichaji simu zao kwa fast charging, hali hii inapelekea kuwa na Chaja nyingi sana, kiuhalisia sasa hivi tunachafua mazingira kuliko zamani.

Ila soon watalazimishwa tu, waweke PD stabdard kwenye simu na Charger zao.
 
Huku Africa kupata fast charge bado ni mtihaji, nna chaja hapa usiku kucha nachaji na simu haijai kisa simu nimenunua bila chaji sasa kupata chaja og nimeambiwa nilipe 30k kwa fast charge ya 25wt
 
Huku Africa kupata fast charge bado ni mtihaji, nna chaja hapa usiku kucha nachaji na simu haijai kisa simu nimenunua bila chaji sasa kupata chaja og nimeambiwa nilipe 30k kwa fast charge ya 25wt
Issue mkuu ni kutokuingialiana hizo Charger. Kama zote zingeruhusu PD unahitaji charger moja tu kuchaji Simu, Laptop na Vifaa vingine. Ukipata 100W moja inatosha hata kama utajibana ununue 50k-100k. Ila unatoa leo 30k ukibadili simu hio fast charge inakua useless sababu haipeleki moto mwingi aimu nyengine.

Kwa case yako ukipata angalia simu yako inasuport standard gani kama Ni ya Qualcomm Charger za Xiaomi za 27W ni Nzuri na zinapatikana kirahisi.

Kwa BBK (oneplus, Vivo, Realme, Oppo, Iqoo etc) tafuta chaja za Realme ama Oppo.

Kwa PD tafuta mchina aliechangamka kidogo Baseus, Anker etc unapata Aliexpress.
 
Kwenye hiyo Oppo Find X6 Pro kama selfie camera ilikuja bila 4K capability inakuwaje iwezeshwe na software update while 4K capability ni hardware based? Chief-Mkwawa
Inawezekana mkuu.
Hardware ya Oppo Find X6 Pro inasupport 4K video recording kwenye kamera ya mbele ila Stock camera app ndio ilikosa hiyo feature kwa hiyo wameiongeza kwa kutumia software update

Kitu kingine hata hizi simu za low end, kuna nyingine hardware ina support kabisa 4K recording lakini manufacturer analimit camera software kurekodi kwa 1080p tu, wanashindwa ku utilize hardware

Application ya Google Camera ina uwezo wa ku unlock 4K video recording kwenye simu ambazo hardware yake ina support lakini software yake inalimit uwezo huo

Soma haya maandishi yaliyokuwa highlighted kwenye hii screenshot kutoka kwa gsmarena. Hii imeandikwa kwenye page ya 5 ya review ya Oppo Find X6 Pro ya gsmarena.com
IMG_20230725_083706.jpg
 
Issue mkuu ni kutokuingialiana hizo Charger. Kama zote zingeruhusu PD unahitaji charger moja tu kuchaji Simu, Laptop na Vifaa vingine. Ukipata 100W moja inatosha hata kama utajibana ununue 50k-100k. Ila unatoa leo 30k ukibadili simu hio fast charge inakua useless sababu haipeleki moto mwingi aimu nyengine.

Kwa case yako ukipata angalia simu yako inasuport standard gani kama Ni ya Qualcomm Charger za Xiaomi za 27W ni Nzuri na zinapatikana kirahisi.

Kwa BBK (oneplus, Vivo, Realme, Oppo, Iqoo etc) tafuta chaja za Realme ama Oppo.

Kwa PD tafuta mchina aliechangamka kidogo Baseus, Anker etc unapata Aliexpress.
Ni samsung mkuu nahitaji watt 25w sasa nishauri hapo ipi itakuwa bora?
 
Kununua simu bila chaja ni uharamia na utapeli, tunapaa tabu sana wateja
Especially kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania
Huku kupata charger ambayo inaendana na simu yako ni shida mpaka uwe na ujuzi kidogo kuhusu hayo mambo na utaalamu wa kuagiza vitu online.

Apple ndio alianza haya mambo ili kulinda mazingira. Makampuni mengine yakafuata
 
kulinda mazingira kwa kuuza charger separate na simu.

biznez in a polite language.
 
Especially kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania
Huku kupata charger ambayo inaendana na simu yako ni shida mpaka uwe na ujuzi kidogo kuhusu hayo mambo na utaalamu wa kuagiza vitu online.

Apple ndio alianza haya mambo ili kulinda mazingira. Makampuni mengine yakafuata
Hii itapelekea wateja wengi wa dunia ya tatu huku kuhamia kwa mchina
 
Ni samsung mkuu nahitaji watt 25w sasa nishauri hapo ipi itakuwa bora?
Samsung nyingi kibongo bongo ni watts 15, hata simu zao za A series zenye watts 25 wakiweka charger kwenye box inakua 15W.

Ninayo Samsung ya 25W na charger ya Mi ya 27W wait nitest nione effectively kiasi Gani simu inapokea, nitaku update baadae.
 
Poa mkuu hiyo ya watt 15 inaweza jaza simu ya mah 5000 ndani ya saa moja?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom