Mtoa mada kama nimekuelewa vizuri swali lako ni kwamba kinachoonekana katika saa ndio kitamkwe au wakati uliopo ndio uandikwe kwenye saa, badala ya hii "viceversa" tunayotumia, kwa maana ya kwamba saa 7 kutamka saa 1.
Kwa Tanzania tunatumia huo mfumo wa viceversa mfano sasa hivi ni saa kumi na moja kamili jioni lakini kwenye saa yako ukiangalia ipo 5:00pm.
Kwa nchi za ulaya kilichopo kwenye saa yako ndio kinachotamkwa kwa maana ya kwamba, tukirudi katika mfano wetu wa saa kumi na moja kamili jioni wao wanasema ni saa tano kamili jioni kama ilivyo kwenye saa.
Kwa nchi za kiarabu, tukirudi kwenye mfano uleule wa saa kumi na moja jioni wao wanasema ni saa kumi na moja hivyo hivyo na saa zao zinaonesha hivyo hivyo Saa 11.
Swali la kujiuliza sisi Watanzania utaratibu huu wa kutamka viceversa tumeupata wapi?
Kwa mtazamo wangu hii imetokana na kuchanganya tamaduni tofauti za mataifa ya nje hasa waarabu (waislamu) na waingereza.
Kwanini?
1. Uarabuni siku inaisha saa kumi na mbili jioni. Kwahiyo saa moja jioni ndio saa la kwanza kwa siku mpya na tarehe mpya.
2. Waingereza siku inaisha saa sita usiku, hivyo ikiingia saa saba usiku kwao ndio saa la kwanza na tarehe mpya.
Sasa sisi baada ya utawala wa mwarabu, alipokuja mwingereza tumechukua utamaduni wa mwarabu tukachanganya na mwingereza tukapata kitu chetu "viceversa". Saa zetu tunaziweka zisome kingereza lakini kutamka, tunatamka kwa kiarabu. Matokeo yake ndio hivyo 5:00pm tunasema saa kumi na moja.