Kwanini saba iwe moja kwenye masaa?

samjarusha

Member
Apr 22, 2017
9
43
Habari zenu ndg WA jamii forum,,Mimi Nina swali/maswali ambayo nahitaji kujua kama ifuatavyo
Kwanini katika mzunguko WA dunia tunatumia masaa ambayo so sahihi?kwa maana ya kwamba tunatumia;

7kama SAA moja
8kama SAA mbili
9kama SAA tatu ,n.k..
nadhani hapo umenipata sasa swali langu la msingi kwanini tusitumie saa moja kama 1 badala ya 7,au saa mbili kama 2 badala ya 8 n.k
Msaada tafadhali
 
Kwa mujibu wa calendar tunayo itumia sote duniani (The Gregorian calendar, an internationally and most widely used civil calendar. It is named after Pope Gregory XIII, who introduced it in October 1582) siku huanza saa sita na dakika moja usiku tofauti na mazoea yetu kuwa siku inaanza saa 12 asubuhi muda jua linapochomoza.
 
Habari zenu ndg WA jamii forum,,Mimi Nina swali/maswali ambayo nahitaji kujua kama ifuatavyo
Kwanini katika mzunguko WA dunia tunatumia masaa ambayo so sahihi?kwa maana ya kwamba tunatumia 7kama SAA moja
8kama SAA mbili
9kama SAA tatu ,n.k..nadhani hapo umenipata sasa swali langu la msingi kwanini tusitumie SAA moja kama 1 badala ya 7,au SAA mbili kama 2 badala ya 8 n.k
Msaada tafadhali
Chukua muda wa halisi toa wa muda unaonyeshwa kwenye saa kwa kila saa halafu utapata jibu
 
Kwa mujibu wa calendar tunayo itumia sote duniani (The Gregorian calendar, an internationally and most widely used civil calendar. It is named after Pope Gregory XIII, who introduced it in October 1582) siku huanza saa sita na dakika moja usiku tofauti na mazoea yetu kuwa siku inaanza saa 12 asubuhi muda jua linapochomoza.
Cjakupata vzr kli anajua cku huanza SAA sitaUCk so bado nakuwa naswali kwan sa sits uck ikiandikwa 6 na sa saba ikaandikwa 7hatuwezi kutumia
 
Kama mwenzetu mmoja alivyokueleza hapo mwanzoni, utaratibu wa muda unaotawala dunia ni wa wazungu. Tukichukulia kwa Kiswahili au kwa mazoea yetu, tuna ama saa moja asubuhi au usiku, na kwa saa saba ni hivyo hivyo. Kwa utaratibu wa dunia, siku inaanza usiku, pale sisi tunaposema ni saa 7 usiku, ndio mwanzo wa siku/tarehe mpya, ndio maana wao wanasema 1. Tofauti ni kuwa sisi tunatumia zaidi masaa 12, ila wao wanatumia masaa 12 pia na masaa 24 kwa mambo ya utaalamu zaidi.
Tofauti nyingine, ni pale sisi tunapoita ile saa 7 usiku ni usiku, wao wanaita ni 1 asubuhi (am). Saa 1 asubuhi yetu, wao ni mwendelezo wa walichoanza nacho tangu ile saa 7 ya usiku yetu, hivyo wao ni 7am. Saa 7 mchana ya kwetu, kwao (kwa masaa 12) ni saa 1 pm, (kwa masaa 24) ni saa 13, na jioni yao ndio inaanzia hapo.
 
Ajabu ni kwamba mwaka mpya ukifika woote tunasheherekea saa sita usiku. Kesho yake watu wanakuuliza kwa nini saa moja asubuhi inasomeka saa 7. Mbona hamusheherekei hiyo saa 1 asubuhi?
 
Kwa sababu siku inaanza katikati ya usiku ambapo ni saa sita, saa moja baada ya saa sita ni saa saba.
 
Habari zenu ndg WA jamii forum,,Mimi Nina swali/maswali ambayo nahitaji kujua kama ifuatavyo
Kwanini katika mzunguko WA dunia tunatumia masaa ambayo so sahihi?kwa maana ya kwamba tunatumia;

7kama SAA moja
8kama SAA mbili
9kama SAA tatu ,n.k..
nadhani hapo umenipata sasa swali langu la msingi kwanini tusitumie saa moja kama 1 badala ya 7,au saa mbili kama 2 badala ya 8 n.k
Msaada tafadhali
Mtoa mada kama nimekuelewa vizuri swali lako ni kwamba kinachoonekana katika saa ndio kitamkwe au wakati uliopo ndio uandikwe kwenye saa, badala ya hii "viceversa" tunayotumia, kwa maana ya kwamba saa 7 kutamka saa 1.
Kwa Tanzania tunatumia huo mfumo wa viceversa mfano sasa hivi ni saa kumi na moja kamili jioni lakini kwenye saa yako ukiangalia ipo 5:00pm.
Kwa nchi za ulaya kilichopo kwenye saa yako ndio kinachotamkwa kwa maana ya kwamba, tukirudi katika mfano wetu wa saa kumi na moja kamili jioni wao wanasema ni saa tano kamili jioni kama ilivyo kwenye saa.
Kwa nchi za kiarabu, tukirudi kwenye mfano uleule wa saa kumi na moja jioni wao wanasema ni saa kumi na moja hivyo hivyo na saa zao zinaonesha hivyo hivyo Saa 11.

Swali la kujiuliza sisi Watanzania utaratibu huu wa kutamka viceversa tumeupata wapi?

Kwa mtazamo wangu hii imetokana na kuchanganya tamaduni tofauti za mataifa ya nje hasa waarabu (waislamu) na waingereza.
Kwanini?

1. Uarabuni siku inaisha saa kumi na mbili jioni. Kwahiyo saa moja jioni ndio saa la kwanza kwa siku mpya na tarehe mpya.
2. Waingereza siku inaisha saa sita usiku, hivyo ikiingia saa saba usiku kwao ndio saa la kwanza na tarehe mpya.

Sasa sisi baada ya utawala wa mwarabu, alipokuja mwingereza tumechukua utamaduni wa mwarabu tukachanganya na mwingereza tukapata kitu chetu "viceversa". Saa zetu tunaziweka zisome kingereza lakini kutamka, tunatamka kwa kiarabu. Matokeo yake ndio hivyo 5:00pm tunasema saa kumi na moja.
 
Habari zenu ndg WA jamii forum,,Mimi Nina swali/maswali ambayo nahitaji kujua kama ifuatavyo
Kwanini katika mzunguko WA dunia tunatumia masaa ambayo so sahihi?kwa maana ya kwamba tunatumia;

7kama SAA moja
8kama SAA mbili
9kama SAA tatu ,n.k..
nadhani hapo umenipata sasa swali langu la msingi kwanini tusitumie saa moja kama 1 badala ya 7,au saa mbili kama 2 badala ya 8 n.k
Msaada tafadhali
Soma Daniel7:25..utaelewa no namaanisha
 
ukiona siyo sahii acha kutumia, kuna 24 hours mode, weka hiyo uanze kuhesabu masaa kuanzia moja mpaka ishirini na nne

Inategemea anaongelea saa moja ya usiku au asubuhi ama zote. Kama ni zote basi ile ya asubuhi itabaki kuwa hivyo hivyo hata akitumia masaa 24. Halafu haiwezekani kuwa na saa 24 bali zinaishia 23 kwa sababu ya kwanza huwa ni saa sifuli.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom