Kwanini saba iwe moja kwenye masaa?

Mtoa mada kama nimekuelewa vizuri swali lako ni kwamba kinachoonekana katika saa ndio kitamkwe au wakati uliopo ndio uandikwe kwenye saa, badala ya hii "viceversa" tunayotumia, kwa maana ya kwamba saa 7 kutamka saa 1.
Kwa Tanzania tunatumia huo mfumo wa viceversa mfano sasa hivi ni saa kumi na moja kamili jioni lakini kwenye saa yako ukiangalia ipo 5:00pm.
Kwa nchi za ulaya kilichopo kwenye saa yako ndio kinachotamkwa kwa maana ya kwamba, tukirudi katika mfano wetu wa saa kumi na moja kamili jioni wao wanasema ni saa tano kamili jioni kama ilivyo kwenye saa.
Kwa nchi za kiarabu, tukirudi kwenye mfano uleule wa saa kumi na moja jioni wao wanasema ni saa kumi na moja hivyo hivyo na saa zao zinaonesha hivyo hivyo Saa 11.

Swali la kujiuliza sisi Watanzania utaratibu huu wa kutamka viceversa tumeupata wapi?

Kwa mtazamo wangu hii imetokana na kuchanganya tamaduni tofauti za mataifa ya nje hasa waarabu (waislamu) na waingereza.
Kwanini?

1. Uarabuni siku inaisha saa kumi na mbili jioni. Kwahiyo saa moja jioni ndio saa la kwanza kwa siku mpya na tarehe mpya.
2. Waingereza siku inaisha saa sita usiku, hivyo ikiingia saa saba usiku kwao ndio saa la kwanza na tarehe mpya.

Sasa sisi baada ya utawala wa mwarabu, alipokuja mwingereza tumechukua utamaduni wa mwarabu tukachanganya na mwingereza tukapata kitu chetu "viceversa". Saa zetu tunaziweka zisome kingereza lakini kutamka, tunatamka kwa kiarabu. Matokeo yake ndio hivyo 5:00pm tunasema saa kumi na moja.
Nice answer
 
Inategemea anaongelea saa moja ya usiku au asubuhi ama zote. Kama ni zote basi ile ya asubuhi itabaki kuwa hivyo hivyo hata akitumia masaa 24. Halafu haiwezekani kuwa na saa 24 bali zinaishia 23 kwa sababu ya kwanza huwa ni saa sifuli.
Thanks
 
Habari zenu ndg WA jamii forum,,Mimi Nina swali/maswali ambayo nahitaji kujua kama ifuatavyo
Kwanini katika mzunguko WA dunia tunatumia masaa ambayo so sahihi?kwa maana ya kwamba tunatumia;

7kama SAA moja
8kama SAA mbili
9kama SAA tatu ,n.k..
nadhani hapo umenipata sasa swali langu la msingi kwanini tusitumie saa moja kama 1 badala ya 7,au saa mbili kama 2 badala ya 8 n.k
Msaada tafadhali
una miaka mingapi?
 
Cjakupata vzr kli anajua cku huanza SAA sitaUCk so bado nakuwa naswali kwan sa sits uck ikiandikwa 6 na sa saba ikaandikwa 7hatuwezi kutumia
Tutaweza sana tu.
Me maisha yote naseti sàa zangu namna hii. Wenyewe wanasema 'kiswahili '
Nikwambie kitu:
Mzungu akikwambia seven o'clock anamaanisha sàa saba kamili hamaanishi sàa moja kamili. Unajua hilo?
Sasa sie hicho kinyume nyume sijui tumekitoa wapi.
 
Standard ya muda duniani ni GMT ambayo kwayo siku inaanza 00.00 hrs (midnight ) hivyo baada ya lisaa limoja ni 01.00 na asubuhi ile ni 06.00. Likigonga utosini ni 12.00. Kama saa unayo tumia ina masaa 12 tu baadala ya 1300 hrs wewe unaingia 01.00pm. Kutokana na mahali ulipo una adjust muda wako kwa time zone yako. Sisi tz tuna add 3 hrs kupata local time with reference to gmt. Kwa huku kwetu asubuhi huanza saa 12.00 asubuhi ambayo ni sawa na saa 00.00 kwenye machine na tunaanza kuhesabu hapo kwenda mbele. Kama mtumia saa una option ya kuseti saa yako kiswahili au ki gmt. Option nyingine ni kuseti ki gmt lakini unasoma kiswahili na hapo ndio huo mkanganyiko wa 1 na 7 hutokea.
 
Kama mwenzetu mmoja alivyokueleza hapo mwanzoni, utaratibu wa muda unaotawala dunia ni wa wazungu. Tukichukulia kwa Kiswahili au kwa mazoea yetu, tuna ama saa moja asubuhi au usiku, na kwa saa saba ni hivyo hivyo. Kwa utaratibu wa dunia, siku inaanza usiku, pale sisi tunaposema ni saa 7 usiku, ndio mwanzo wa siku/tarehe mpya, ndio maana wao wanasema 1. Tofauti ni kuwa sisi tunatumia zaidi masaa 12, ila wao wanatumia masaa 12 pia na masaa 24 kwa mambo ya utaalamu zaidi.
Tofauti nyingine, ni pale sisi tunapoita ile saa 7 usiku ni usiku, wao wanaita ni 1 asubuhi (am). Saa 1 asubuhi yetu, wao ni mwendelezo wa walichoanza nacho tangu ile saa 7 ya usiku yetu, hivyo wao ni 7am. Saa 7 mchana ya kwetu, kwao (kwa masaa 12) ni saa 1 pm, (kwa masaa 24) ni saa 13, na jioni yao ndio inaanzia hapo.
 
g
Kwa mujibu wa calendar tunayo itumia sote duniani (The Gregorian calendar, an internationally and most widely used civil calendar. It is named after Pope Gregory XIII, who introduced it in October 1582) siku huanza saa sita na dakika moja usiku tofauti na mazoea yetu kuwa siku inaanza saa 12 asubuhi muda jua linapochomoza.
Good
 
Best answer?
 
Nia ya hawa jamaa kuweka mambo kinyume na taratbu za dunia hii ndio imepelekea saa 7 kua sa 1 wao n Ant evrythng kwa maana ya new word order na kuitukuza 6 namba kila saa linabadilishwa na 6 na kuleta maana nyingne Mfano 12-6=6 sa13-6=7 mchana lkn wao wanaiweka 7 kua asubuh saa 8-6=2 saa nane bdl ya saa mbil
 
Sisi ndo tumebadilisha masaa mkuu! Waswahili ndo tunafikiria hivyo ila nchi zingine saba ni saba.
 
Kama mwenzetu mmoja alivyokueleza hapo mwanzoni, utaratibu wa muda unaotawala dunia ni wa wazungu. Tukichukulia kwa Kiswahili au kwa mazoea yetu, tuna ama saa moja asubuhi au usiku, na kwa saa saba ni hivyo hivyo. Kwa utaratibu wa dunia, siku inaanza usiku, pale sisi tunaposema ni saa 7 usiku, ndio mwanzo wa siku/tarehe mpya, ndio maana wao wanasema 1. Tofauti ni kuwa sisi tunatumia zaidi masaa 12, ila wao wanatumia masaa 12 pia na masaa 24 kwa mambo ya utaalamu zaidi.
Tofauti nyingine, ni pale sisi tunapoita ile saa 7 usiku ni usiku, wao wanaita ni 1 asubuhi (am). Saa 1 asubuhi yetu, wao ni mwendelezo wa walichoanza nacho tangu ile saa 7 ya usiku yetu, hivyo wao ni 7am. Saa 7 mchana ya kwetu, kwao (kwa masaa 12) ni saa 1 pm, (kwa masaa 24) ni saa 13, na jioni yao ndio inaanzia hapo.
Cha kushangaza tunajifanya kusoma saa tofauti lakini sijawai kutana na saa ya kiswahili ili inaposoma moja tuseme sa moja. Hizi saa za kizungu zinachanganya wasiojua kuzisoma.
 
Mtoa mada kama nimekuelewa vizuri swali lako ni kwamba kinachoonekana katika saa ndio kitamkwe au wakati uliopo ndio uandikwe kwenye saa, badala ya hii "viceversa" tunayotumia, kwa maana ya kwamba saa 7 kutamka saa 1.
Kwa Tanzania tunatumia huo mfumo wa viceversa mfano sasa hivi ni saa kumi na moja kamili jioni lakini kwenye saa yako ukiangalia ipo 5:00pm.
Kwa nchi za ulaya kilichopo kwenye saa yako ndio kinachotamkwa kwa maana ya kwamba, tukirudi katika mfano wetu wa saa kumi na moja kamili jioni wao wanasema ni saa tano kamili jioni kama ilivyo kwenye saa.
Kwa nchi za kiarabu, tukirudi kwenye mfano uleule wa saa kumi na moja jioni wao wanasema ni saa kumi na moja hivyo hivyo na saa zao zinaonesha hivyo hivyo Saa 11.

Swali la kujiuliza sisi Watanzania utaratibu huu wa kutamka viceversa tumeupata wapi?

Kwa mtazamo wangu hii imetokana na kuchanganya tamaduni tofauti za mataifa ya nje hasa waarabu (waislamu) na waingereza.
Kwanini?

1. Uarabuni siku inaisha saa kumi na mbili jioni. Kwahiyo saa moja jioni ndio saa la kwanza kwa siku mpya na tarehe mpya.
2. Waingereza siku inaisha saa sita usiku, hivyo ikiingia saa saba usiku kwao ndio saa la kwanza na tarehe mpya.

Sasa sisi baada ya utawala wa mwarabu, alipokuja mwingereza tumechukua utamaduni wa mwarabu tukachanganya na mwingereza tukapata kitu chetu "viceversa". Saa zetu tunaziweka zisome kingereza lakini kutamka, tunatamka kwa kiarabu. Matokeo yake ndio hivyo 5:00pm tunasema saa kumi na moja.
Umeelezea vizuri sana! Nimekuelewa mkuu
 
Tutaweza sana tu.
Me maisha yote naseti sàa zangu namna hii. Wenyewe wanasema 'kiswahili '
Nikwambie kitu:
Mzungu akikwambia seven o'clock anamaanisha sàa saba kamili hamaanishi sàa moja kamili. Unajua hilo?
Sasa sie hicho kinyume nyume sijui tumekitoa wapi.
Ila hii itafaa kwa zile saa zinazoonesha namba na sio za mishale.
 
Back
Top Bottom