Kwanini NHIF huwa haiendi na wakati linapokuja suala la gharama za matibabu?

ZALEMDA

JF-Expert Member
Aug 15, 2017
1,647
1,885
Gharama za matibabu huwa zinabadirika mara kwa mara kulingana na gharama za maisha zinavyobadiriki na Kinachopandisha gharama za maisha ni bidhaa muhimu kupanda gharama hususani mafuta ya dizeli na petroli. Mfano ni hii ya sasa kabla ya 2021 lita ya mafuta ya petrol haikuzidi 2300-2600. Kwa leo lita moja ya dizeli ni inauzwa kwa shillingi 3131 na lita ya petroli inuzwa kwa shilling 2,994 kuanzia June 2022

Ukilinganisha na bei za june 2020 kipindi kile lita ya petroli iliuzwa kwa shilling 1,693 na lita ya dizeli iliuzwa kwa shilling 1,568

soma :REF: PPR/2020 - 07/1
PUBLIC NOTICE ON CAP PRICES FOR PETROLEUM PRODUCTS EFFECTIVE
WEDNESDAY, 1st JULY 2020

Ni dhahiri kwamba kulingana na gharama za mafuta kupanda , gharama za undeshashi wa makapuni ,vituo vya kutolea kuduma za afya zimepanda maradufu.gharama za dawa zimepanda,ghrama za vifaa tiba zimepanda .kila kitu ni shida.

Ukiangalia gharama za matibabu zinazolipiwa na mifuko ya afya wakati mwingi unakuta ziko statitic siyo dynamic. NHIF ndiyo inaongoza kwa kulipia gharama za chini ukilinganisha na bima za afya nyengine. Kama nakosea watanisamehe.gharama zao ziko static kwa muda mrefu sana.huwa wana review every three years.

Sasa tangia kipindi cha corona mpaka sasa maisha yamebadirika,gharama za uendeshaji zimepanda mara dufu ,

Hoja yangu ni kwani gharama wanazolipia makampuni ya bima ya afya hasa NHIF Ziko vile vile kwa muda mrefu hadi miaka 5? huku kupanda kwa gharama za maisha wao hawauoni?
 
Back
Top Bottom