mkorinto
JF-Expert Member
- Jun 11, 2014
- 30,842
- 37,526
Wala hamna tatizo,ukisema utumie akili dkk 1 tu,hakuna kitu utakipokea ktk bible pale ni iman ndio inafanya kazi.Miswada sahihi
Wanazuoni wengi wa madhehebu na vikundi mbalimbali vya Kikristo wamethibitisha kuwa sehemu kubwa ya maandiko ya Biblia ina mashaka makubwa juu ya uhalisia wake.
Kwanza tukubaliane kitu,bible ina maandiko yenye wasifu wa aina mbali mbali,kuna historia za watu,manabii na mitume,hakuna sehem yeyote panapodai bible imeandikwa na Mungu.huu upuuzi unapatikana ktk Quran tu.Katika utangulizi wa Ngano za Mungu mwenye Mwili, Mtunzi ameandika yafuatayo:
"Katika karne ya kumi na tisa, Wakristo wa Kimagharibi walifanya marekebisho makubwa mawili ili kuitikia wito wa kupanuka kwa elimu ya wanadamu: imekubalika kuwa mwanadamu ni sehemu ya maumbile na ameibuka kuwa ni miongoni mwa wanamageuzi wa mfumo wa maisha duniani; imekubalika kuwa vitabu vya Biblia vimeandikwa na watu tofauti tofauti katika matukio tofauti tofauti na haviwezi kukubaliwa kuwa ni utunzi wa Mungu wa neno kwa neno.
Haya naomba msimamo wako sasa.rejea swali.Katika gazeti la kimataifa la, Newsweek2F3, lililobeba makala yenye kichwa 'Oo Bwana, Nani Aliyeandika Dua hii?'
kikosi cha wanatiolojia kutoka katika dhehebu kuu la kiporestanti, pamoja na Wasomi muhimu wa Biblia wa Kikatoliki nchini Marekani, baada ya ukaguzi wa kina wa miswada ya mwanzo kabisa ya Agano Jipya, wamehitimisha kuwa maneno pekee ya "Dua ya Bwana" ambayo yanaweza kunasibishwa barabara na Yesu Kristo ni "baba".
Na hilo, ni kwa mujibu wa wasomi hao wa kanisa, maneno yote yaliyokuja baada ya ibara ya kwanza, "Baba yetu", ambayo ni dua muhimu sana ya Kikristo, yaliongezwa karne nyingi na waandishi wa kanisa walionukuu miswada ya mwanzoni ya Injili.
Shirika la U.S News & World Report, linanukuu zaidi kuwa, kikundi cha wasomi kilisema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya maneno yaliyoandikwa katika Injili kumhusu Yesu huenda ni ya kubuniwa.
Miongoni mwa hayo likiwemo neno la Ekaristi ya Yesu ,katika Karamu ya Mwisho ("Chukua, kula. Huu ni mwili wangu…") na kila neno aliloambiwa kuwa amelitamka toka msalabani.