Vita Kuu ya Tatu (WW3) ipo dhahiri mlangoni, Tuwe na akili ili tuishi

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,606
29,754
Urusi ilipovamia Ukraine kutokana na uchokozi (indirect) wa US akishirikiana na NATO ilikuwa ndiyo curtain-raiser, Baadaye tukaona Vita ya Sudan na Juba vimepambamoto huku taarifa za madhila zikidhibitiwa kwa kiwango kikubwa na vyombo vya kimataifa na serikali za Afrika... Tumeona Afrika Kaskazini na Magharibi kumekubwa na mapinduzi ya kijeshi yanayosemwa kuratibiwa na Urusi....

Israel imeendeleza unyama mkubwa ulioanza kwa uchokozi wa kigaidi kutoka kundi la HAMAS. unyama huo umeenda kuathiri maisha ya watu WOTE wa Gaza Strip. Vita imeanza kusambaa Lebanon na sehemu za Jordan huku Syria ikiendelea kupokea vipigo mfululizo...

Tumeona pale DRC Afrika ya Kusini imepeleka majeshi yake (kwa kivuli cha SADC) kujipanga kuishambulia Rwanda (mshirika wa US) na hili lipo wazi kabisa.

Kaskazini mwa Msumbiji jirani na mpaka wa Tanzania eneo la Cabo Delgado vita imechachamaa kupambana na majahili wanaofadhiliwa na mataifa makubwa, haya mambo yanafichwa na serikali zetu kwa nguvu kubwa sana.

Houth imejipanga kupigana na imeweza kushambulia kila meli inayokatiza bahari nyeusi kutoka nchi zinazoiunga mkono Israel....

Ndugu zangu wabongo wenzangu, Vita Kuu ya Tatu ya Dunia ipo mlangoni kwa sababu maandalizi yote yamekamilika na sasa mataifa makubwa yameshaweka vikosi vyao sawa. Ukiangalia mwenendo wa China, Korea Kaskazini, Iran, NATO na kwingineko ni mwendo wa mazoezi na majaribio ya kijeshi kila kona... Hivyo tujipange kama nchi tujue tunaishije katikati ya ulimwengu huu wa kitimtim.

Tusisahau kujiwekea akiba ya chakula kama nchi
 
MAGAIDI YA KIDINI NDIO WANALETA VURUGU KWENYE HII DUNIA LAKINI MATAIFA MAKUBWA YALIYO ENDELEA HAKUNA ANAYE TAKA VITA SHIDA NI MAGAIDI YENYE MLENGO WA KIDINI.
Ukifuatilia magaidi na wapiganaji karibia wote wa misituni wanapewa chapuo ya misaada ya zana na kimafunzo kutoka kwa hayo mataifa unayoyaona ndo mkombozi wa dunia hii
 
Urusi ilipovamia Ukraine kutokana na uchokozi (indirect) wa US akishirikiana na NATO ilikuwa ndiyo curtain-raiser, Baadaye tukaona Vita ya Sudan na Juba vimepambamoto huku taarifa za madhila zikidhibitiwa kwa kiwango kikubwa na vyombo vya kimataifa na serikali za Afrika... Tumeona Afrika Kaskazini na Magharibi kumekubwa na mapinduzi ya kijeshi yanayosemwa kuratibiwa na Urusi....

Israel imeendeleza unyama mkubwa ulioanza kwa uchokozi wa kigaidi kutoka kundi la HAMAS. unyama huo umeenda kuathiri maisha ya watu WOTE wa Gaza Strip. Vita imeanza kusambaa Lebanon na sehemu za Jordan huku Syria ikiendelea kupokea vipigo mfululizo...

Tumeona pale DRC Afrika ya Kusini imepeleka majeshi yake (kwa kivuli cha SADC) kujipanga kuishambulia Rwanda (mshirika wa US) na hili lipo wazi kabisa.

Kaskazini mwa Msumbiji jirani na mpaka wa Tanzania eneo la Cabo Delgado vita imechachamaa kupambana na majahili wanaofadhiliwa na mataifa makubwa, haya mambo yanafichwa na serikali zetu kwa nguvu kubwa sana.

Houth imejipanga kupigana na imeweza kushambulia kila meli inayokatiza bahari nyeusi kutoka nchi zinazoiunga mkono Israel....

Ndugu zangu wabongo wenzangu, Vita Kuu ya Tatu ya Dunia ipo mlangoni kwa sababu maandalizi yote yamekamilika na sasa mataifa makubwa yameshaweka vikosi vyao sawa. Ukiangalia mwenendo wa China, Korea Kaskazini, Iran, NATO na kwingineko ni mwendo wa mazoezi na majaribio ya kijeshi kila kona... Hivyo tujipange kama nchi tujue tunaishije katikati ya ulimwengu huu wa kitimtim.

Tusisahau kujiwekea akiba ya chakula kama nchi
Vita ya tatu hapana mzungu hakuna kitu anaogopa kama nyuklia. Ila vita vya maeneo maeneo vitakuwepo
 
Labda niseme tu uelewe...
Ninapata vijitaarifa vya intel kutoka huko ndani ndani kwa marafiki. Wapo wanaotupenda na kusema wazi kabisaa kuwa haya yanayoendelea ni maandalizi ya Vita..

Marekani kinachoendelea sasa ni mashinikizo ya wananchi kuitaka nchi yao ijiondoe kwenye mizozo ya kimataifa na ipunguze bajeti yake ya Ulinzi ambayo imeongezeka ghafla mno hivi karibuni...

Mkuu kuna mambo ni nyeti, ukiyajua unaweza kulazwa kwa kuumwa kichwa
 
Pamoja na hayo bado mkuu. Vita ya dunia ya leo sio ile ya miaka ile ya bunduki. Ni ya nyuklia na maandalizi ni kawaida wala yasikutishe.
 
Ndio tatizo la kuwakubali makafiri kwa namna yoyote ila ,hayo ndio mambo yanakatazwa daima .

Walipigana vita ya kwanza ya dunia wao kwa wao ,kila nchi wakifika tu basi wanaanzisha vita mfano kule mashariki ya kati.

Mtu na akili timamu uwamalize watoto na watu wasiokuwa na hatia eti unalinda maslahi ,ni ujing mtu kutoka bara moja kwenda kusababisha vita bara lingine kwa ujinga eti superpower.

Binadamu wamechoka ,hii ndio maana Qur an inasema hawa makafiri ni maadui wakubwa sana... Sabab kubwa ya vita ni kuingilia katika mambo ndani ya nchi za watu .

Chukulia mfano kweny nchi wananchi wanapata tabu sana wewe unapeleka mpaka Tillion ili kuchochea vita iendelee, huku maisha ya wananchi wako bado baadhi ni mabaya.

View: https://twitter.com/GlobeEyeNews/status/1761475227395969391?s=19

View: https://twitter.com/GlobeEyeNews/status/1761006868418252878?s=19
 
Urusi ilipovamia Ukraine kutokana na uchokozi (indirect) wa US akishirikiana na NATO ilikuwa ndiyo curtain-raiser, Baadaye tukaona Vita ya Sudan na Juba vimepambamoto huku taarifa za madhila zikidhibitiwa kwa kiwango kikubwa na vyombo vya kimataifa na serikali za Afrika... Tumeona Afrika Kaskazini na Magharibi kumekubwa na mapinduzi ya kijeshi yanayosemwa kuratibiwa na Urusi....

Israel imeendeleza unyama mkubwa ulioanza kwa uchokozi wa kigaidi kutoka kundi la HAMAS. unyama huo umeenda kuathiri maisha ya watu WOTE wa Gaza Strip. Vita imeanza kusambaa Lebanon na sehemu za Jordan huku Syria ikiendelea kupokea vipigo mfululizo...

Tumeona pale DRC Afrika ya Kusini imepeleka majeshi yake (kwa kivuli cha SADC) kujipanga kuishambulia Rwanda (mshirika wa US) na hili lipo wazi kabisa.

Kaskazini mwa Msumbiji jirani na mpaka wa Tanzania eneo la Cabo Delgado vita imechachamaa kupambana na majahili wanaofadhiliwa na mataifa makubwa, haya mambo yanafichwa na serikali zetu kwa nguvu kubwa sana.

Houth imejipanga kupigana na imeweza kushambulia kila meli inayokatiza bahari nyeusi kutoka nchi zinazoiunga mkono Israel....

Ndugu zangu wabongo wenzangu, Vita Kuu ya Tatu ya Dunia ipo mlangoni kwa sababu maandalizi yote yamekamilika na sasa mataifa makubwa yameshaweka vikosi vyao sawa. Ukiangalia mwenendo wa China, Korea Kaskazini, Iran, NATO na kwingineko ni mwendo wa mazoezi na majaribio ya kijeshi kila kona... Hivyo tujipange kama nchi tujue tunaishije katikati ya ulimwengu huu wa kitimtim.

Tusisahau kujiwekea akiba ya chakula kama nchi
vita ya tatu ya dunia, hivi ni lazima iwepo hiyo vita
 
Duh...vip US ataendelea kushika ukiranja mkuu au utaamia far east.
Kama ulivyosema uko karibu nao ivyo na matokeo utakua nayo.
 
Back
Top Bottom