Single mother kampiga mwiko wa kichwa Baba wa kufikia

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,304
Jambo?

Hili tukio limetokea mtaani kwetu kuna jamaa ameoa Single mother, sasa usiku wakiwa sebuleni jamaa akasikia meseji imeingia kwenye simu ya Single mother.

Lahaullah ile kuangalia anakutana na meseji inayosema, "Mpenzi unakuja lini kwangu kunipikia, nimemisi mahanjumati yako mpenzi"

Jamaa baada kusoma ile meseji na kwakuwa anaijua namba ya jamaa aliezaa na mke wake ikabidi apaniki na amuulize mwanamke wake kwanini jamaa anamuita mpenzi.

Mwanamke katika kujitetea akasema eti itakuwa aliezaa nae amejisahau na kumuita mpenzi. Jamaa akapandwa na hasira na kumpiga kibao Single mother.

Aisee! Bado haijajulikana ule mwiko aliutoa wapi maana ni suala la sekunde kadhaa jamaa akawa kashapigwa na mwiko wa kichwa na kudondoka chini akiugulia maumivu.

Jamaa anasema laiti angejua asingemuoa yule bidada maana kwa anayomfanyia anajuta.
 
Back
Top Bottom