Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 39,741
- 92,197
Till now mitazamo ya watu imeshaanza kubadilika kama Nina kuoa hadhi ya kujilinda and still Nina shambuliwa wakati wewe mlinzi wangu upo so what do you expect!?? .
Wewe ulitegemea kuona kitu kama hicho !?
Well said 💯Nilitegemea kwa kiasi lakini sio kwa kiwango hiki.
Sasa akitaka amkomeshe Marekani atoe suprise ya karne. Sijui atatumia teknolojia gani ikitokea akashambulia Washington wengi watashangilia hata kama atapigwa.
Hata hivyo kwa kiwango alichofikia inatosha. Heshima ipo
Mtu akisha sema tu kuwa urusi ilifanya kosa kuvamia Ukraine basi namweka mtu huyo kwenye kundi la low IQ...pia urusi inapigana na nchi nyingi sana Ukraine ndiyo maana hata vifo vya majeshi kule ni kubwa sana.. vita vya urusi na Ukraine vilitengenezwa na kuanzishwa na Nchi za NATO siyo urussi lengo lilikuwa ni kuihujumu Urusi.Muda huwa ni mwalimu mzuri sana.
Nakumbuka mabazazi na madunya wa humu ndani mnamo tarehe 24 February 2022 siku ambayo Urusi alivamia Ukraine walinitafuta na kunisimanga sana. Wengine walidiriki hadi kukashifu taaluma yangu. Walishangaa kwamba kwanini Urusi ameshindwa kuivamia Ukraine na kuimaliza kwa haraka ilhali anajiita taifa kubwa (Super-Power). Niliwaambia vijana wa humu ndani kwamba Urusi alifanya makosa kuvamia jirani yake na kuna mambo alikosea, lakini kusema kwamba NATO+EU wataiangusha ni jambo lisilowezekana. Mataifa makubwa huwa yanafanya makosa pia (Political Blunders)
Mpaka 2026, Urusi na Ukraine wanapigana, huku Ukraine wakiwa wameumizwa zaidi. Urusi anatumia fedha nyingi sana kwenye vita na usalama, jambo ambalo siku vita ikiisha litazua matatizo makubwa mno kwasababu watu wengi watakosa ajira ambazo wanazifanya sasa. Pia kuna mambo kadha wa kadha. Sasa huu ni utangulizi tu:
Naomba niwaulize ninyi vijana wa humu ndani, kwanini Marekani (The Only Global Super-Power) ameshindwa kulimaliza taifa la Iran ndani ya wiki kama alivyofanya Afghanistani au Venezuela ??? Fahamuni tu kwamba hivi vita hapigani Marekani peke yake bali anasaidiwa na Israeli na washirika wengine kama Australia ambao imejulikana hivi karibuni kwamba walisaidia kuzamisha manowari za Iran. Hapo kuna Saudi Arabia, Jordan, Qatar, Bahrain, UAE, Azerbaijan na Mgambo wa kikurdi (kurdish Militia).
Donald J Trump alisema ni siku nne tu baada ya Ayatollah kulambishwa mchanga basi, Iran ingekuwa kaputi. Ila sasa yametokea tofauti. Marekani kweli kawatandika Iran, lakini nao wamemtandika vibaya mno. Mara ya mwisho kambi za kijeshi za Marekani zimelipuliwa hivi ilikuwa ni mwaka 1941 kule Pearl Harbour ambapo Japan aliua zaidi ya wanajeshi 2000. Jambo la kushangaza kulikuwa na silaha za ulinzi za kisasa kabisa kwenye hizo kambi kama THAAD na PATRIOT ambazo zilikuwa na mfumo bora kabisa wa rada duniani ambao umelipuliwa.
Mahoteli ambayo walikuwa wanakaa MAJASUSI na WANAJESHI wa Marekani yamelipuliwa. Mpaka sasa maswali ni mawili tu: Aidha Iran alikuwa amejipanga sana AU kuna mtu anamsaidia maana siyo jambo rahisi kufanya haya ambayo Iran amekuwa akifanya hasa kwenye kufanya mashambulio ya ulengaji bila kukosea (Precision Attack) ambayo hutegemea kwa sehemu kubwa mifumo ya satellite. Israeli nako yamewakuta, sehemu muhimu za kiusalama zinalipuliwa. Utapinga, utanuna, utabisha na kuleta hasara ila hii ndiyo hali ilivyo.
SASA IRAN ANAPAMBANAJE: Mwaka 2018 nakumbuka kuna uzi wangu nilifurumushiwa matusi na mabazazi na madunya wa humu ndani, nilioandika kuhusu dhana ya ASYMETRIC WARFARE. Dhana hii inafanya kazi pale ambapo taifa dogo au kikundi kidogo kinapambana na taifa kubwa. Lengo siyo kutaka kupambana CONVENTIONAL WARFARE, ila ni kumsababishia maumivu makubwa yule aliye mkubwa kiasi cha kufanya akimbie. Mfano halisi, ni USSR vs Mujahedeen au USA vs Vietcong.
Iran hana AIRFORCE kama USA na ISRAEL. Iran hana NAVY kama USA na ISRAEL. Iran alichokiamua ni kutengeneza FORMIDABLE ROCKET AND DRONE FORCE, ambalo lina uwezo wa kisasa kabisa kushambulia taifa lolote lile hapa duniani. Jambo ambalo wengi hatulifahamu ni kwamba Iran mbali na udhaifu wao mwingi, walianza kupambana na Marekani tokea mwaka 1979, na wameshuhudia USA akishambulia wenzake kama Iraq, Afghanistan, Libya na Venezuela. Unadhani ni wajinga ???
MADHARA ENDAPO VITA HAITAISHA MAPEMA:
Mosi, The Aura of American Invincibility has been shattered before the world. Zile propaganda za kusema hakuna wa kumgusa Marekani hazipo tena. Iran katuonesha kwamba Marekani na Israel wanagusika. Hebu sasa fikiria, endapo Uchina ataamua kuvamia Taiwani, nani anaamini kabisa kwamba kambi za Marekani zilizopo South-Korea, Philippines, Japan na Guam zitakuwa salama, kama tu kambi kubwa za Marekani barani Asia zimelipuliwa juzi na jana na Iran, taifa ambalo halina nguvu kama Uchina. Kiukweli, Marekani alizichanga karata vibaya na yanamtokea puani.
Pili, Urusi atapata nguvu kubwa kutokana na bei ya mafuta kupanda. Saudi Arabia, UAE, Oman, Qatar na Bahrain wanaogopa kupitisha mafuta Mfereji wa Hormuz, ambao kwa siku mapipa milioni 17 yanapita. Vita ikiendelea hivi na Iran akafanikiwa kufunga kabisa mfereji, basi mafuta ya Ulaya na Asia itabidi yapatikane Urusi ambako kuna vikwazo. Juzi Vladmir Putin kasema anafikiria kusitisha kabisa kuuza gesi Ulaya. Sasa USA na EU watabakiwa na maamuzi kama haya: Ondoa vikwazo ili tupate nishati kutoka Urusi. Bahati mbaya wakiondoa vikwazo Ukraine ndiyo kwaheri.
Tatu, Urusi atapenda kulipiza alichofanyiwa Ukraine. Hii ndiyo tabia kuu ya Urusi. Niguse-Ninuke. Marekani akitingwa kule Iran, basi lazima atapunguza kuangalia Ukraine. Sasa itabidi silaha zote zinazozalishwa zienda Persian Gulf (Ghuba ya Uajemi) siyo Ukraine. Urusi na Uchina wanaweza kuigeuza Iran, VIETNAM 2 endepo Marekani akiendelea hivi bila kuomba msamaha. Bahati mbaya sana kwa alichokifanya Donald Trump, Marekani ikirudi nyuma kama kipindi cha Twelve Days War mwaka 2024, basi ndiyo mwisho wa siasa za MAGA na Trump, na anaweza kufungwa kwasababu ameanzisha vita bila kibali cha Bunge.
Nne, mpaka sasa SECURITY DIPLOMACY ya Marekani imekufa. Ameingia makubaliano ya ulinzi na Saudi Arabia mwaka 1971, na mataifa kama UAE, Qatar na Bahrain kwamba wakitumia Dollar kuuza mafuta basi atawalinda. Bahati mbaya wanapigwa na Iran, wanaomba kuuziwa silaha na msaada wa kijeshi lakini bado hawajapata, kipaumbele chake ni Israel na kambi zake. Hii ndiyo vita kubwa ya kipropaganda ambayo Marekani hawezi kuishinda, endapo hatawalinda Saudi Arabia, UAE na Qatar dhidi ya Iran. Ujumbe utakuwa ni kwamba, kama Marekani ameshindwa kuwalinda UAE, Qatar na Saudi Arabia dhidi ya taifa dogo kama Iran, ataweza kweli kuwalinda Japan, South-Korea, Philippines na Australia dhidi ya taifa kubwa kama Uchina ???
Tano, THE COLLAPSE OF THE LAW OF NEUTRALITY. Katika sheria za kimataifa hasa wakati wa vita, The Law of Neutrality huyalinda mataifa ambayo hayapambani moja kwa moja, hata kama yanakuwa yanauza silaha kwa adui au kuwa na kambi za kijeshi ambazo hazitumiki kijeshi kushambulia adui. Kitendo cha Marekani kuvamia Iran bila sababu ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Hata Iran kuanza kuvamia Saudi-Arabia, UAE na Qatar ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Lakini Marekani hawezi kulalamika katika hili kwasababu yeye ndiye mvunjifu sugu wa sheria za kimataifa. Sheria za kimataifa ili zifuatwe na mataifa madogo, inategemea sana mataifa makubwa.
Hili lisipoangaliwa sana, tutaamka siku na kukuta Urusi kaanza kulipua Poland na Ujerumani kisa tu kuna kambi za jeshi za Marekani, hata kama hazitumiki kushambulia. Huku ndiko tunaelekea. Hivyo tukishafahamu haya, vitaifa masikini kama Tanzania vijiepushe na tabia za kupenda kujipendekeza kwa mataifa makubwa kama Uchina, Urusi na Marekani. Dunia inaelekea kubaya na kama tukitaka kuvuka itabidi kweli tusifungamane na upande wowote. Sasa wale wanopenda pesa za waarabu kisa ni wenzetu katika IMANI wakiendeleza tabia zao za kusajili manowari kule Zenji, wataliletea hili taifa matatizo makubwa mno. Tena kipindi hiki ukipigwa huna pakusemea maana kila mtu anapambana lwake.
==============================================================================
HALAFU KUNA MABAZAZI mengine yanasema INTERNATIONAL LAW IMEKUFA, haya nitayajibu baadaye.HAYANA AKILI
USA wamesema itawachukua 4-6 weeks kukamilisha objectives zao. Sidhani kama kuna mtu mwenye akili timamu alitegemea hii vita iishe ndani ya wiki.Tupo hapa,
Wiki ya kwanza ndiyo ishakata hivyo....
Wiki ingine ikiisha ntakuita hapa, lakini usikimbie.....
Asante sana kiongozi.Muda huwa ni mwalimu mzuri sana.

USA wamesema itawachukua 4-6 weeks kukamilisha objectives zao. Sidhani kama kuna mtu mwenye akili timamu alitegemea hii vita iishe ndani ya wiki.
Wewe jamaa tangu uandike uongo uongo kule kwenye uzi wa mgogoro wa Urusi na Ukraine, inahitaji kusoma mara mbili mbili unachoandika.
Kwa hiyo nyinyi mnafurahi taifa moja kuua political leadership ya taifa jingine kisa vita???Hiyo ni sign ya weakness sio nguvu.Nguvu inatambulika kwenye utiifu wa sheria za kimataifa, sio kulipua watu na nchi kisa una jeshi kubwa, nguvu kubwa etc.
Pili mlitaka Urus wamle kichwa Zelensky ili tu awafurahishe watu kama nyinyi et ndo nguvu hizo au sio???Umesahau Putin alimuhakikishia waziri mkuu wa Israel kipindi kile kuwa hatomgusa Zelensky???Uo ndo uongozi...
Vita sio betting, au Simba na Yanga, kwamba mna-prove ubishi wenu kwa kutembea na roho za watu.
Et Urusi hatawali anga, mosi hujui kuwa kuna vijeba vimejichimbia pale -NATO na air defenses za Kutosha, utalinganisha na Iran??
Pili Urusi anawezapiga popote kwa missiles akitokea kwake, kwa nini ahangaike kuweka rehani maisha ya airforce yake wakati ana alternative??Makombora tu na drones zinagusa kila kona..
US atashinda pambano pale Iran lakini hatshinda vita...BATTLES yes, atawatwanga kwelikweli lkn kushinda vita sio rahisi pale, nchi kubwa ile, milima na mapango kama yote
Sio manowali ya Marekani Bali ni ya Iran.rekebisha.

You constantly shy away from speaking the truth. If you can not speak honesty due to your " Mahaba" it would be better to remain silent than to mislead people. As one of the Most prominent JF Speakers, Many may assume you hold the monopoly on Truth.Kuna hili lifala linaitwa let the caged bird sings ni moja kati ya Mabazazi na Madunya ya humu ndani. Limetoka shimoni baada ya maumivu makali ya moyo, likaharisha ujinga halafu likaenda kuvimbiwa futari ya Kwaresma.
Lenyewe na wenzake wengi humu ndani niliwahi kuwaambia mwaka 2022 kwamba muda ni mwalimu mzuri sana, wekeni akiba ya maneno. Katika wooote ambaye huwa hajawahi kunivunjia heshima kwenye mijadala ni mdogo wangu T14 Armata , atabishana na mimi vikali ila hajawahi kubisha kitu bila walau kuweka hoja. Katika hili namheshimu sana sanaaa.
Mengine sasa hivi yanachungulia yanapita kimyakimya kama mapepo yakitegemea walau CNN watangaze chochote kibaya kilichowakuta Iran ili wakilete hapa, lakini wapiiiiii. Mimi niko nao tu hawaa Weekend yote hiiiii
Ukishachagua TU upande
Uchambuzi wako unakosa mantiki na credibility
Unalinganisha vita ya Marekani aliyepigana chini ya wiki mbili na Urusi ambaye anapigana miaka mitatu Hadi sasa na taifa jirani hapo
Kuna watu niwapuuzi sana kuvamiwa Irani ni sawa ila kuvamiwa ukrein si sawa hayo ni mahaba ya kishetani
Iran ni taifa dogo kushinda marekani lakini USA ain't having an easy way.
Marekani hawezi kupigana vita bila kuwa na allies ambae kwa sasa ni waarab(wote wamechezea) na Israel.
Iran anasurvive peke yake, pamoja na kwamba amekuwa kwenye economic sanctions kwa miaka zaidi ya 40 sasa.
Waajemi sio wamatumbi kwamba you can have an easy route.
Pamoja na kukua kwa teknolojia?
Nilitegemea kwa kiasi lakini sio kwa kiwango hiki.
Sasa akitaka amkomeshe Marekani atoe suprise ya karne. Sijui atatumia teknolojia gani ikitokea akashambulia Washington wengi watashangilia hata kama atapigwa.
Hata hivyo kwa kiwango alichofikia inatosha. Heshima ipo
Hahahaaa!Kama ilivyokuwa mbaya kwa Cuba kule The Bay of Pigs mwaka 1961 eti ???
Mfano wa jirani wa US tumemuona, kalala Venezuela kaamkia USA na night dress yake.Kwa kuongezea kwa uchache ni kwamba, kama Iran ingepakana na US kama Russia na Ukraine, yamkini hadi sasa hali kwa Iran ingekuwa ni mbaya mbaya zaidi.
Mkuu changia hoja mbona kama uwezo wako imejaa kwenye Matusi tu kama hujui Geopolitics tulia usome tu ,Tutaamini vipi kama ni typing error au ni IQ yako ndogo??
Waliokubeza wapo sahihi aisee..!
Pol Pot alidumu miaka minne tu madarakani, vipi naye ulitaka afukuzwe madarakani na Marekani?Sawa!
Vipi kuhusu Pol Pot wa Cambodia sasa ???
Jirani kabisa na Vietnam.....
Weka na source mkuuNdani ya siku nne Iran destroyed Five radar system worth approximately USD five billion.