Kwanini Marekani ameshindwa kuimaliza Iran haraka?

Wewe kenge kula vichwa sio kufikiwa malengo haya nambie baada ya kula vichwa kimebadilika??Majirani wote wamekula kipigo mlango bahari umefungwa Iran regime bado ipo madarakani haya nambie kula vichwa kumesaidia nini??
Uniambie wewe Mkundugu hivi malengo ya kurusha kombora huwa ni nini km sio kuua adui vitani ? wenzio tayari wanafurahia Papuchi 72 mpya ambazo hajizatobolewa huko Peponi wewe umeng'ang'ania mwazi mpana wa mkeo km handaki la Hamas, unangoja nini kwenda vitani ukabutuliwe ufaidi toto'z za Allah kule peponi ?
 
Muda huwa ni mwalimu mzuri sana.

Nakumbuka mabazazi na madunya wa humu ndani mnamo tarehe 24 February 2022 siku ambayo Urusi alivamia Ukraine walinitafuta na kunisimanga sana. Wengine walidiriki hadi kukashifu taaluma yangu. Walishangaa kwamba kwanini Urusi ameshindwa kuivamia Ukraine na kuimaliza kwa haraka ilhali anajiita taifa kubwa (Super-Power). Niliwaambia vijana wa humu ndani kwamba Urusi alifanya makosa kuvamia jirani yake na kuna mambo alikosea, lakini kusema kwamba NATO+EU wataiangusha ni jambo lisilowezekana. Mataifa makubwa huwa yanafanya makosa pia (Political Blunders)

Mpaka 2026, Urusi na Ukraine wanapigana, huku Ukraine wakiwa wameumizwa zaidi. Urusi anatumia fedha nyingi sana kwenye vita na usalama, jambo ambalo siku vita ikiisha litazua matatizo makubwa mno kwasababu watu wengi watakosa ajira ambazo wanazifanya sasa. Pia kuna mambo kadha wa kadha. Sasa huu ni utangulizi tu:

Naomba niwaulize ninyi vijana wa humu ndani, kwanini Marekani (The Only Global Super-Power) ameshindwa kulimaliza taifa la Iran ndani ya wiki kama alivyofanya Afghanistani au Venezuela ??? Fahamuni tu kwamba hivi vita hapigani Marekani peke yake bali anasaidiwa na Israeli na washirika wengine kama Australia ambao imejulikana hivi karibuni kwamba walisaidia kuzamisha manowari za Iran. Hapo kuna Saudi Arabia, Jordan, Qatar, Bahrain, UAE, Azerbaijan na Mgambo wa kikurdi (kurdish Militia).

Donald J Trump alisema ni siku nne tu baada ya Ayatollah kulambishwa mchanga basi, Iran ingekuwa kaputi. Ila sasa yametokea tofauti. Marekani kweli kawatandika Iran, lakini nao wamemtandika vibaya mno. Mara ya mwisho kambi za kijeshi za Marekani zimelipuliwa hivi ilikuwa ni mwaka 1941 kule Pearl Harbour ambapo Japan aliua zaidi ya wanajeshi 2000. Jambo la kushangaza kulikuwa na silaha za ulinzi za kisasa kabisa kwenye hizo kambi kama THAAD na PATRIOT ambazo zilikuwa na mfumo bora kabisa wa rada duniani ambao umelipuliwa.

Mahoteli ambayo walikuwa wanakaa MAJASUSI na WANAJESHI wa Marekani yamelipuliwa. Mpaka sasa maswali ni mawili tu: Aidha Iran alikuwa amejipanga sana AU kuna mtu anamsaidia maana siyo jambo rahisi kufanya haya ambayo Iran amekuwa akifanya hasa kwenye kufanya mashambulio ya ulengaji bila kukosea (Precision Attack) ambayo hutegemea kwa sehemu kubwa mifumo ya satellite. Israeli nako yamewakuta, sehemu muhimu za kiusalama zinalipuliwa. Utapinga, utanuna, utabisha na kuleta hasara ila hii ndiyo hali ilivyo.

SASA IRAN ANAPAMBANAJE: Mwaka 2018 nakumbuka kuna uzi wangu nilifurumushiwa matusi na mabazazi na madunya wa humu ndani, nilioandika kuhusu dhana ya ASYMETRIC WARFARE. Dhana hii inafanya kazi pale ambapo taifa dogo au kikundi kidogo kinapambana na taifa kubwa. Lengo siyo kutaka kupambana CONVENTIONAL WARFARE, ila ni kumsababishia maumivu makubwa yule aliye mkubwa kiasi cha kufanya akimbie. Mfano halisi, ni USSR vs Mujahedeen au USA vs Vietcong.

Iran hana AIRFORCE kama USA na ISRAEL. Iran hana NAVY kama USA na ISRAEL. Iran alichokiamua ni kutengeneza FORMIDABLE ROCKET AND DRONE FORCE, ambalo lina uwezo wa kisasa kabisa kushambulia taifa lolote lile hapa duniani. Jambo ambalo wengi hatulifahamu ni kwamba Iran mbali na udhaifu wao mwingi, walianza kupambana na Marekani tokea mwaka 1979, na wameshuhudia USA akishambulia wenzake kama Iraq, Afghanistan, Libya na Venezuela. Unadhani ni wajinga ???

MADHARA ENDAPO VITA HAITAISHA MAPEMA:

Mosi
, The Aura of American Invincibility has been shattered before the world. Zile propaganda za kusema hakuna wa kumgusa Marekani hazipo tena. Iran katuonesha kwamba Marekani na Israel wanagusika. Hebu sasa fikiria, endapo Uchina ataamua kuvamia Taiwani, nani anaamini kabisa kwamba kambi za Marekani zilizopo South-Korea, Philippines, Japan na Guam zitakuwa salama, kama tu kambi kubwa za Marekani barani Asia zimelipuliwa juzi na jana na Iran, taifa ambalo halina nguvu kama Uchina. Kiukweli, Marekani alizichanga karata vibaya na yanamtokea puani.

Pili, Urusi atapata nguvu kubwa kutokana na bei ya mafuta kupanda. Saudi Arabia, UAE, Oman, Qatar na Bahrain wanaogopa kupitisha mafuta Mfereji wa Hormuz, ambao kwa siku mapipa milioni 17 yanapita. Vita ikiendelea hivi na Iran akafanikiwa kufunga kabisa mfereji, basi mafuta ya Ulaya na Asia itabidi yapatikane Urusi ambako kuna vikwazo. Juzi Vladmir Putin kasema anafikiria kusitisha kabisa kuuza gesi Ulaya. Sasa USA na EU watabakiwa na maamuzi kama haya: Ondoa vikwazo ili tupate nishati kutoka Urusi. Bahati mbaya wakiondoa vikwazo Ukraine ndiyo kwaheri.

Tatu, Urusi atapenda kulipiza alichofanyiwa Ukraine. Hii ndiyo tabia kuu ya Urusi. Niguse-Ninuke. Marekani akitingwa kule Iran, basi lazima atapunguza kuangalia Ukraine. Sasa itabidi silaha zote zinazozalishwa zienda Persian Gulf (Ghuba ya Uajemi) siyo Ukraine. Urusi na Uchina wanaweza kuigeuza Iran, VIETNAM 2 endepo Marekani akiendelea hivi bila kuomba msamaha. Bahati mbaya sana kwa alichokifanya Donald Trump, Marekani ikirudi nyuma kama kipindi cha Twelve Days War mwaka 2024, basi ndiyo mwisho wa siasa za MAGA na Trump, na anaweza kufungwa kwasababu ameanzisha vita bila kibali cha Bunge.

Nne, mpaka sasa SECURITY DIPLOMACY ya Marekani imekufa. Ameingia makubaliano ya ulinzi na Saudi Arabia mwaka 1971, na mataifa kama UAE, Qatar na Bahrain kwamba wakitumia Dollar kuuza mafuta basi atawalinda. Bahati mbaya wanapigwa na Iran, wanaomba kuuziwa silaha na msaada wa kijeshi lakini bado hawajapata, kipaumbele chake ni Israel na kambi zake. Hii ndiyo vita kubwa ya kipropaganda ambayo Marekani hawezi kuishinda, endapo hatawalinda Saudi Arabia, UAE na Qatar dhidi ya Iran. Ujumbe utakuwa ni kwamba, kama Marekani ameshindwa kuwalinda UAE, Qatar na Saudi Arabia dhidi ya taifa dogo kama Iran, ataweza kweli kuwalinda Japan, South-Korea, Philippines na Australia dhidi ya taifa kubwa kama Uchina ???

Tano, THE COLLAPSE OF THE LAW OF NEUTRALITY. Katika sheria za kimataifa hasa wakati wa vita, The Law of Neutrality huyalinda mataifa ambayo hayapambani moja kwa moja, hata kama yanakuwa yanauza silaha kwa adui au kuwa na kambi za kijeshi ambazo hazitumiki kijeshi kushambulia adui. Kitendo cha Marekani kuvamia Iran bila sababu ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Hata Iran kuanza kuvamia Saudi-Arabia, UAE na Qatar ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Lakini Marekani hawezi kulalamika katika hili kwasababu yeye ndiye mvunjifu sugu wa sheria za kimataifa. Sheria za kimataifa ili zifuatwe na mataifa madogo, inategemea sana mataifa makubwa.

Hili lisipoangaliwa sana, tutaamka siku na kukuta Urusi kaanza kulipua Poland na Ujerumani kisa tu kuna kambi za jeshi za Marekani, hata kama hazitumiki kushambulia. Huku ndiko tunaelekea. Hivyo tukishafahamu haya, vitaifa masikini kama Tanzania vijiepushe na tabia za kupenda kujipendekeza kwa mataifa makubwa kama Uchina, Urusi na Marekani. Dunia inaelekea kubaya na kama tukitaka kuvuka itabidi kweli tusifungamane na upande wowote. Sasa wale wanopenda pesa za waarabu kisa ni wenzetu katika IMANI wakiendeleza tabia zao za kusajili manowari kule Zenji, wataliletea hili taifa matatizo makubwa mno. Tena kipindi hiki ukipigwa huna pakusemea maana kila mtu anapambana lwake.

==============================================================================

HALAFU KUNA MABAZAZI mengine yanasema INTERNATIONAL LAW IMEKUFA, haya nitayajibu baadaye.HAYANA AKILI

Asante kwa udadavuzi mujarab mkuu. Humu ndani hata mm huwa nawaangalia watoto wa f2000 wanavyoishadadia Marekani, nawashangaa sana. Hii vita ukute Korea, Japan na Uchina wapo nyuma ya Iran. Ni zaidi ya vita ya dunia.
 
Uniambie wewe Mkundugu hivi malengo ya kurusha kombora huwa ni nini km sio kuua adui vitani ? wenzio tayari wanafurahia Papuchi 72 mpya ambazo hajizatobolewa huko Peponi wewe umeng'ang'ania mwazi mpana wa mkeo km handaki la Hamas, unangoja nini kwenda vitani ukabutuliwe ufaidi toto'z za Allah kule peponi ?
Haya wewe mkumajirani malengo ya vita yalikuwa ni regime change imefanikiwa???Ukibisha hapo labda unabishana na Trump and Netanyahu
 
Baadhi ya watu wanabisha vitu vya ajabu Malengo ya Marekani na Israil yalikuwa ni
1. Kubadili utawala wa Iran
2. Kuangamiza mpango wa nyuklia wa Iran n.k
Latin hawajatimiza hata Moja ya Malengo Yao leo hii mtu anakuja kusema wamemuua Khamenei, wamemuua Larijani je haya ndiyo Malengo Yao??
Walikuja na Kauli mbiu ya kuwakomboa raia wa Iran je, kulipua madaraja, viwanda, Shule na Kuua vitoto vya Shule ndiyo kuwakomboa raia wa Iran??
Vita ni Malengo!!
 
Walisema lengo ni regime change, waki andaa watu akiwemo mtoto wa Shah. Lengo ni kumaliza utawala wa dola ya Kiislam waweke watu wao. Malcolm Zheng usibishane na anayebisha! mpuuze

Wamebaini shambulio la June 25 haikuangamiza mitambo kama walivyokusudia. Israel ilijaribu haikufanikiwa. Marekani na B-Bomber hazikufanikiwa. Iran ilishaondoa enriched Uranium.

Lengo la kumuua Khamenei ilikuwa kuvuruga Utawala . Marekani na Israel waliamini Khamenei ndiye revolutionary council kwamba kutatokea power struggle within halafu wao waendelee kuchagiza uasi ''uprising'' kama walivyoanzisha wakidai ni wao.

Kosa lao ni kutoelewa Khamenei ni kiongozi wa Dini ''spiritual leader'' hata wanaopinga serikali walimkubali kama kiongozi wa kidini. Kumuua Khamenei kulipunguza kundi linaloasi kwani ilikuwa kama kuitosha Dini. Ndio maana hadi sasa hakuna uprising na kila inapoanza inakufa kwa upinzani wa Wananchi

Wameupiga vyuo vikuu 25, mashule zaidi ya 600 na Hospitali 200. Wameua wanafunzi na wanavunja madaraja. Wamevunja mitambo ya kusafisha mafuta n.k. Marekani inasema lengo ni Wananchi wateseke ili kuichukia serikali yao. Kinyume chake Uzalendo unaonekana kutawala zaidi

Moja ya madai yao ni Wanawake kutoruhusiwa kuvaa vimini. Takwimu zinaonyesha nchini Iran Wanawale ni 60% ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu. Hili haisemwi bali wanataka kumkomboa Mwanamke avae kimini.
Wameua Wasichana 175 dakika ya kwanza ya mashambulizi. Je ndio ukombozi huo?
 
Ulitaka aimalizaje kwa mfano? Mbona watu mnaroho mbaya hivyo? Embu vaa viatu vya Iran na vya wa Iran na viongozi wao. Mafuta yamepanda bei tu kidogo kelele nchi nzima sasa hao wa Iran kwao hali ya maisha unadhan ipoje?
 
Baadhi ya watu wanabisha vitu vya ajabu Malengo ya Marekani na Israil yalikuwa ni
1. Kubadili utawala wa Iran
2. Kuangamiza mpango wa nyuklia wa Iran n.k
Latin hawajatimiza hata Moja ya Malengo Yao leo hii mtu anakuja kusema wamemuua Khamenei, wamemuua Larijani je haya ndiyo Malengo Yao??
Walikuja na Kauli mbiu ya kuwakomboa raia wa Iran je, kulipua madaraja, viwanda, Shule na Kuua vitoto vya Shule ndiyo kuwakomboa raia wa Iran??
Vita ni Malengo!!
Weka speech ya Trump kiongozi yeyote akisema hivyo vinginevyo ni porojo tu.
 
Sa
Actually, I have a side: I side with the Victims of Imperialism.

I hate Fascism, I hate Imperialism and I can't stand Fanatical Nationalism.

If the evil things done by Americans were to be done by Tanzanians I would hate Tanzania as well.
sasa uchambuzi pia utakuwa biased
 
Walisema lengo ni regime change, waki andaa watu akiwemo mtoto wa Shah. Lengo ni kumaliza utawala wa dola ya Kiislam waweke watu wao. Malcolm Zheng usibishane na anayebisha! mpuuze

Wamebaini shambulio la June 25 haikuangamiza mitambo kama walivyokusudia. Israel ilijaribu haikufanikiwa. Marekani na B-Bomber hazikufanikiwa. Iran ilishaondoa enriched Uranium.

Lengo la kumuua Khamenei ilikuwa kuvuruga Utawala . Marekani na Israel waliamini Khamenei ndiye revolutionary council kwamba kutatokea power struggle within halafu wao waendelee kuchagiza uasi ''uprising'' kama walivyoanzisha wakidai ni wao.

Kosa lao ni kutoelewa Khamenei ni kiongozi wa Dini ''spiritual leader'' hata wanaopinga serikali walimkubali kama kiongozi wa kidini. Kumuua Khamenei kulipunguza kundi linaloasi kwani ilikuwa kama kuitosha Dini. Ndio maana hadi sasa hakuna uprising na kila inapoanza inakufa kwa upinzani wa Wananchi

Wameupiga vyuo vikuu 25, mashule zaidi ya 600 na Hospitali 200. Wameua wanafunzi na wanavunja madaraja. Wamevunja mitambo ya kusafisha mafuta n.k. Marekani inasema lengo ni Wananchi wateseke ili kuichukia serikali yao. Kinyume chake Uzalendo unaonekana kutawala zaidi

Moja ya madai yao ni Wanawake kutoruhusiwa kuvaa vimini. Takwimu zinaonyesha nchini Iran Wanawale ni 60% ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu. Hili haisemwi bali wanataka kumkomboa Mwanamke avae kimini.
Wameua Wasichana 175 dakika ya kwanza ya mashambulizi. Je ndio ukombozi huo?
Hoja makini sana!
 
Muda huwa ni mwalimu mzuri sana.

Nakumbuka mabazazi na madunya wa humu ndani mnamo tarehe 24 February 2022 siku ambayo Urusi alivamia Ukraine walinitafuta na kunisimanga sana. Wengine walidiriki hadi kukashifu taaluma yangu. Walishangaa kwamba kwanini Urusi ameshindwa kuivamia Ukraine na kuimaliza kwa haraka ilhali anajiita taifa kubwa (Super-Power). Niliwaambia vijana wa humu ndani kwamba Urusi alifanya makosa kuvamia jirani yake na kuna mambo alikosea, lakini kusema kwamba NATO+EU wataiangusha ni jambo lisilowezekana. Mataifa makubwa huwa yanafanya makosa pia (Political Blunders)

Mpaka 2026, Urusi na Ukraine wanapigana, huku Ukraine wakiwa wameumizwa zaidi. Urusi anatumia fedha nyingi sana kwenye vita na usalama, jambo ambalo siku vita ikiisha litazua matatizo makubwa mno kwasababu watu wengi watakosa ajira ambazo wanazifanya sasa. Pia kuna mambo kadha wa kadha. Sasa huu ni utangulizi tu:

Naomba niwaulize ninyi vijana wa humu ndani, kwanini Marekani (The Only Global Super-Power) ameshindwa kulimaliza taifa la Iran ndani ya wiki kama alivyofanya Afghanistani au Venezuela ??? Fahamuni tu kwamba hivi vita hapigani Marekani peke yake bali anasaidiwa na Israeli na washirika wengine kama Australia ambao imejulikana hivi karibuni kwamba walisaidia kuzamisha manowari za Iran. Hapo kuna Saudi Arabia, Jordan, Qatar, Bahrain, UAE, Azerbaijan na Mgambo wa kikurdi (kurdish Militia).

Donald J Trump alisema ni siku nne tu baada ya Ayatollah kulambishwa mchanga basi, Iran ingekuwa kaputi. Ila sasa yametokea tofauti. Marekani kweli kawatandika Iran, lakini nao wamemtandika vibaya mno. Mara ya mwisho kambi za kijeshi za Marekani zimelipuliwa hivi ilikuwa ni mwaka 1941 kule Pearl Harbour ambapo Japan aliua zaidi ya wanajeshi 2000. Jambo la kushangaza kulikuwa na silaha za ulinzi za kisasa kabisa kwenye hizo kambi kama THAAD na PATRIOT ambazo zilikuwa na mfumo bora kabisa wa rada duniani ambao umelipuliwa.

Mahoteli ambayo walikuwa wanakaa MAJASUSI na WANAJESHI wa Marekani yamelipuliwa. Mpaka sasa maswali ni mawili tu: Aidha Iran alikuwa amejipanga sana AU kuna mtu anamsaidia maana siyo jambo rahisi kufanya haya ambayo Iran amekuwa akifanya hasa kwenye kufanya mashambulio ya ulengaji bila kukosea (Precision Attack) ambayo hutegemea kwa sehemu kubwa mifumo ya satellite. Israeli nako yamewakuta, sehemu muhimu za kiusalama zinalipuliwa. Utapinga, utanuna, utabisha na kuleta hasara ila hii ndiyo hali ilivyo.

SASA IRAN ANAPAMBANAJE: Mwaka 2018 nakumbuka kuna uzi wangu nilifurumushiwa matusi na mabazazi na madunya wa humu ndani, nilioandika kuhusu dhana ya ASYMETRIC WARFARE. Dhana hii inafanya kazi pale ambapo taifa dogo au kikundi kidogo kinapambana na taifa kubwa. Lengo siyo kutaka kupambana CONVENTIONAL WARFARE, ila ni kumsababishia maumivu makubwa yule aliye mkubwa kiasi cha kufanya akimbie. Mfano halisi, ni USSR vs Mujahedeen au USA vs Vietcong.

Iran hana AIRFORCE kama USA na ISRAEL. Iran hana NAVY kama USA na ISRAEL. Iran alichokiamua ni kutengeneza FORMIDABLE ROCKET AND DRONE FORCE, ambalo lina uwezo wa kisasa kabisa kushambulia taifa lolote lile hapa duniani. Jambo ambalo wengi hatulifahamu ni kwamba Iran mbali na udhaifu wao mwingi, walianza kupambana na Marekani tokea mwaka 1979, na wameshuhudia USA akishambulia wenzake kama Iraq, Afghanistan, Libya na Venezuela. Unadhani ni wajinga ???

MADHARA ENDAPO VITA HAITAISHA MAPEMA:

Mosi
, The Aura of American Invincibility has been shattered before the world. Zile propaganda za kusema hakuna wa kumgusa Marekani hazipo tena. Iran katuonesha kwamba Marekani na Israel wanagusika. Hebu sasa fikiria, endapo Uchina ataamua kuvamia Taiwani, nani anaamini kabisa kwamba kambi za Marekani zilizopo South-Korea, Philippines, Japan na Guam zitakuwa salama, kama tu kambi kubwa za Marekani barani Asia zimelipuliwa juzi na jana na Iran, taifa ambalo halina nguvu kama Uchina. Kiukweli, Marekani alizichanga karata vibaya na yanamtokea puani.

Pili, Urusi atapata nguvu kubwa kutokana na bei ya mafuta kupanda. Saudi Arabia, UAE, Oman, Qatar na Bahrain wanaogopa kupitisha mafuta Mfereji wa Hormuz, ambao kwa siku mapipa milioni 17 yanapita. Vita ikiendelea hivi na Iran akafanikiwa kufunga kabisa mfereji, basi mafuta ya Ulaya na Asia itabidi yapatikane Urusi ambako kuna vikwazo. Juzi Vladmir Putin kasema anafikiria kusitisha kabisa kuuza gesi Ulaya. Sasa USA na EU watabakiwa na maamuzi kama haya: Ondoa vikwazo ili tupate nishati kutoka Urusi. Bahati mbaya wakiondoa vikwazo Ukraine ndiyo kwaheri.

Tatu, Urusi atapenda kulipiza alichofanyiwa Ukraine. Hii ndiyo tabia kuu ya Urusi. Niguse-Ninuke. Marekani akitingwa kule Iran, basi lazima atapunguza kuangalia Ukraine. Sasa itabidi silaha zote zinazozalishwa zienda Persian Gulf (Ghuba ya Uajemi) siyo Ukraine. Urusi na Uchina wanaweza kuigeuza Iran, VIETNAM 2 endepo Marekani akiendelea hivi bila kuomba msamaha. Bahati mbaya sana kwa alichokifanya Donald Trump, Marekani ikirudi nyuma kama kipindi cha Twelve Days War mwaka 2024, basi ndiyo mwisho wa siasa za MAGA na Trump, na anaweza kufungwa kwasababu ameanzisha vita bila kibali cha Bunge.

Nne, mpaka sasa SECURITY DIPLOMACY ya Marekani imekufa. Ameingia makubaliano ya ulinzi na Saudi Arabia mwaka 1971, na mataifa kama UAE, Qatar na Bahrain kwamba wakitumia Dollar kuuza mafuta basi atawalinda. Bahati mbaya wanapigwa na Iran, wanaomba kuuziwa silaha na msaada wa kijeshi lakini bado hawajapata, kipaumbele chake ni Israel na kambi zake. Hii ndiyo vita kubwa ya kipropaganda ambayo Marekani hawezi kuishinda, endapo hatawalinda Saudi Arabia, UAE na Qatar dhidi ya Iran. Ujumbe utakuwa ni kwamba, kama Marekani ameshindwa kuwalinda UAE, Qatar na Saudi Arabia dhidi ya taifa dogo kama Iran, ataweza kweli kuwalinda Japan, South-Korea, Philippines na Australia dhidi ya taifa kubwa kama Uchina ???

Tano, THE COLLAPSE OF THE LAW OF NEUTRALITY. Katika sheria za kimataifa hasa wakati wa vita, The Law of Neutrality huyalinda mataifa ambayo hayapambani moja kwa moja, hata kama yanakuwa yanauza silaha kwa adui au kuwa na kambi za kijeshi ambazo hazitumiki kijeshi kushambulia adui. Kitendo cha Marekani kuvamia Iran bila sababu ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Hata Iran kuanza kuvamia Saudi-Arabia, UAE na Qatar ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Lakini Marekani hawezi kulalamika katika hili kwasababu yeye ndiye mvunjifu sugu wa sheria za kimataifa. Sheria za kimataifa ili zifuatwe na mataifa madogo, inategemea sana mataifa makubwa.

Hili lisipoangaliwa sana, tutaamka siku na kukuta Urusi kaanza kulipua Poland na Ujerumani kisa tu kuna kambi za jeshi za Marekani, hata kama hazitumiki kushambulia. Huku ndiko tunaelekea. Hivyo tukishafahamu haya, vitaifa masikini kama Tanzania vijiepushe na tabia za kupenda kujipendekeza kwa mataifa makubwa kama Uchina, Urusi na Marekani. Dunia inaelekea kubaya na kama tukitaka kuvuka itabidi kweli tusifungamane na upande wowote. Sasa wale wanopenda pesa za waarabu kisa ni wenzetu katika IMANI wakiendeleza tabia zao za kusajili manowari kule Zenji, wataliletea hili taifa matatizo makubwa mno. Tena kipindi hiki ukipigwa huna pakusemea maana kila mtu anapambana lwake.

==============================================================================

HALAFU KUNA MABAZAZI mengine yanasema INTERNATIONAL LAW IMEKUFA, haya nitayajibu baadaye.HAYANA AKILI

Iran yenyewe imeshatepeta, unataka imalizwe mara mbili. Teke la pundamilia linalorushwa katika hali ya kujitetea anapodhibitiwa sio kwamba halimuumizi simba, linamuumiza, lakini hiyo haina maana kwamba hatiishia kuwa kitoweo cha mfalme wa nyika.
 
Wewe Nguruvi3: na Malcolm Lumumba msiwe mnakuja wote kwa pamoja,mkubaliane muwe mnakuja mmoja mmoja,yaani baada ya wiki anakuja mmoja.
Sababu ni kwamba hawa vijana wa bongo uwezo wa kupokea mambo makubwa kama haya hawana ,hivyo badala ya kuwasaidia ndio mtawaondolea kabisa hata hicho kidogo walichonacho vichwani,wengi wameharibiwa akili na Hollywood movies,amini nakuambia.

... naongeza na betting
 
Walisema lengo ni regime change, waki andaa watu akiwemo mtoto wa Shah. Lengo ni kumaliza utawala wa dola ya Kiislam waweke watu wao. Malcolm Zheng usibishane na anayebisha! mpuuze

Wamebaini shambulio la June 25 haikuangamiza mitambo kama walivyokusudia. Israel ilijaribu haikufanikiwa. Marekani na B-Bomber hazikufanikiwa. Iran ilishaondoa enriched Uranium.

Lengo la kumuua Khamenei ilikuwa kuvuruga Utawala . Marekani na Israel waliamini Khamenei ndiye revolutionary council kwamba kutatokea power struggle within halafu wao waendelee kuchagiza uasi ''uprising'' kama walivyoanzisha wakidai ni wao.

Kosa lao ni kutoelewa Khamenei ni kiongozi wa Dini ''spiritual leader'' hata wanaopinga serikali walimkubali kama kiongozi wa kidini. Kumuua Khamenei kulipunguza kundi linaloasi kwani ilikuwa kama kuitosha Dini. Ndio maana hadi sasa hakuna uprising na kila inapoanza inakufa kwa upinzani wa Wananchi

Wameupiga vyuo vikuu 25, mashule zaidi ya 600 na Hospitali 200. Wameua wanafunzi na wanavunja madaraja. Wamevunja mitambo ya kusafisha mafuta n.k. Marekani inasema lengo ni Wananchi wateseke ili kuichukia serikali yao. Kinyume chake Uzalendo unaonekana kutawala zaidi

Moja ya madai yao ni Wanawake kutoruhusiwa kuvaa vimini. Takwimu zinaonyesha nchini Iran Wanawale ni 60% ya Wanafunzi wa Vyuo vikuu. Hili haisemwi bali wanataka kumkomboa Mwanamke avae kimini.
Wameua Wasichana 175 dakika ya kwanza ya mashambulizi. Je ndio ukombozi huo?
Ebana ehh
 
Inshengoma is just a Russia- Obsessed Mofo.
He supports anything that opposes the West.
If Sheitwan comes out today and stand against the west,Inshengoma would definitely appoint himself as his favorite demon.
in other hand;
A Muslim is some that reads the Quran,An ex Muslim is some that understands the Quran.
Hata PAPA Leo anazipinga Marekani na Israeli.

Vipi utahama Kanisa au utakubaliana na balozi wa MUNGU duniani ???
 
Natumai ndugu zangu WASTAHIKI mtakuwa mshajifunza somo la msingi sana katika hili:

1. Nguvu ya kijeshi ina mipaka yake (THERE ARE LIMITS TO MILITARY POWER).

2. Dunia ya mwaka 2000 siyo dunia ya mwaka 2026, Marekani hakusoma alama za nyakati.

3. Marekani na Israel wamesababisha madhara makubwa lakini ushindi wa kisiasa kaupata Iran.

4. Baada ya hii vita Iran ndiyo litakuwa taifa lenye nguvu sana pale Middle-East/The Levant.

5. Mfereji wa Hormuz umempa Iran karata turufu ya kidiplomasia itakayotumika dhidi ya Europe na Asia.

6. Miaka michache ijayo dhehebu la Kishia ndiyo litakuwa na ushawishi mkubwa kwenye ulimwengu wa kiislamu.

7. Barack Obama alivyosaini JCPOA alikuwa mbele ya muda ila alipuuzwa kwasababu za kibaguzi.

8. CIA+MOSSAD+THE FIVE EYES wameshindwa kufanya mapinduzi ya kisiasa nchini Iran. UJASUSI kama taaluma huwa na mipaka yake pia.

Taifa kubwa kama Marekani kukubali kukaa meza moja na taifa ambalo kwanza ni la KIISLAMU, WANASEMA LINAONGOZWA NA MAGAIDI, LINAUNGA MKONO UGAIDI DUNIANI na LINAVUNJA HAKI ZA BINADAMU, ni jambo ambalo lazima wewe ukae ufikiri. Marekani huwa hanaga mazungumzo na taifa au kundi ambalo linawachukulia wako chini yao, lakini katika hili la Iran Marekani ni dhahiri ameshindwa.

===================================================================================
Marekani na Israel wamepatwa na changamoto kubwa mno. Middle-East mataifa yenye nguvu kijeshi mpaka sasa ni matatu: Israel, Uturuki na Iran. Haya mataifa mawili ya Uturuki na Iran hayana historia nzuri kabisa na Israeli, na lengo kuu la Israel ni kuhakikisha anamtumia Marekani kuzorotesha Iran na Uturuki. Jambo ambalo ni baya mno (A worse-case scenario) kwa Israeli ni kuwa na maadui wenye nguvu kama Uturuki na Iran kwa pamoja wakishirikiana kupambana naye.

Hivyo Marekani inabidi aendelee kutumia NATO kumuweka uturuki karibu, na kucheza karata zake vizuri nchini Syria. Uturuki hawataki kabisa Wakurdi, ambao pia wako Iran kwa wingi. Bahati mbaya sana Israel inataka kuwatumia Wakurdi kuzorotesha Iran na Uturuki kwa pamoja, jambo ambalo lina hatari ya kuwaunganisha Wairani na Waturuki. Kikawaida, Iran na Uturuki siyo marafiki hata kidogo, lakini Marekani akicheza vibaya tu kipindi hiki basi Israel atakuwa na hali mbaya mno.
======================================================================================

ENIWEI maisha ndivyo yalivyo, kila siku unajifunza mambo mapya na kubadilisha mtazamo.

Mkiendelea kukomaa kwamba dunia hii yetu ya mwaka 2026 ni dunia ambayo mataifa makubwa yanaweza kuamka tu na kuvamia taifa jingine halafu kusiwe na madhara yoyote. Kalaghabaooo.

Kilichotokea, Ukraine na Iran, ni funzo kubwa hata kwa Uchina kuhusu Taiwan, kwamba akijifanya kijogoo aingie kichwa-kichwa kulazimisha kutaka kuwatala ndugu zake hata kwa kumwaga damu kisa UNAZI (ULTRA-NATIONALISM/CHINESE CHAUVINISM) itakula kwake.
 
Madunya na Mababazi sijui wapo hali gani sasa .

Sikutarajia Jana kumuona Trump akiwa kwenye low mood anatangaza mambo ya makubaliano bila ego na matambo yake huku akikosoa Israel hadharani .

US imekuwa waoga kutoa maelezo full kuhusu makubaliano.

Wataalamu wengi wabobezi na majasusi wanasema Iran amepata nguvu na karata ya kuzitumia kwa baadae kutikisa mataifa makubwa
 
Back
Top Bottom