Kwanini Ma IT bongo sio matajiri?

Kwanini Ma IT bongo sio matajiri?

They are not creative, cheti hakikupi utajiri isipokuwa hardwork and creativity, unless kwa kuiba.
 
Mimi nazan ni mfumo wa elimu. Mtu anasoma darasa la kwanza mpaka advance haifaham hata computer. Hapo akifaulu anachagua IT, anaenda chuo na kusoma miaka 3 then anagraduate na kurudi mtaani. Wenzetu wamekeza hayo mambo kweny elimu, mtoto anakua akijua hzo mambo ndio maana utaskika kijana wa miaka 14 afanya hiki, huku bongo kijana wa miaka 14 anajifunza kusoma, kukalili na kuandika,
Kweli mkuu unapata PC ukiingia first year tena ela ya boom at 20' age
 
Jamaa angu tupo nae kitaa ana degree ya it ana library yake ya kuweka nyimbo Kuban CDs kupiga window .....alinifundishaga Ku hack fb account kipindi hichoooo ....ni bonge la it kwa mtaani kwetu
 
Kwa Tz mambo mengi hayaendi kwa kasi au mwelekeo wa kidunia. Wanataaluma wa IT, madaktari na hata wakunga(manesi), wanasheria, wahandisi n.k, kwenye ulimwengu wa kwanza(nchi za viwanda, zilizoendelea), huwa na hali nzuri sana kifedha, na taaluma zao zimeendelea kwa vifaa na ujuzi wa kisasa wa kiteknolojia. Huku kwetu ni kama tumegeuka na kuurudia ujima. Kila kitu kinazidi kuwa na hali mbaya.
 
Kwa upeo wangu ma IT wapo wengi fursa wanazo, elimu ipo ila tuangalie na suala la capital. Utafanya kitu gani kinachohusu computer kikubwa chenye hela bila hela ya kutosha...tuangalie nchi yetu... Kuna hawa ISP wanakaba hadi penati, umeme wa kazi sio uhakika sana...japo miezi hii angalau... Njoo kwenye kazi yenyewe hutaweza peke yako itabidi upate crew angalau wawili watatu,, kwa gharama za nani??;; hapo serikali haijatoa sapoti Kwa lolote... Maana utafanya mwishowe utaeka mtandaoni (youtube) hadi ilegharama yako irudi kipitia mtandaoni...ni msoto.. Ndio maana hakuna mwana IT anakubali kupoteza gharama na muda wakekwa ishu ambayo itamchukua muda kumlipa..


Nina mengi ndio maana hii IT yangu ya darasani naitafutia mtaji nianzishe computer center uku nilipo maana nimeona ni fursa
 
Ma IT wengi wa Bongo ni vilaza. Wangekuwa smart, wangeweza kuutumia ujuzi wao kupanga mikeka ya ku BET na wangeshatoka kimaisha...
 
Kwa Tz mambo mengi hayaendi kwa kasi au mwelekeo wa kidunia. Wanataaluma wa IT, madaktari na hata wakunga(manesi), wanasheria, wahandisi n.k, kwenye ulimwengu wa kwanza(nchi za viwanda, zilizoendelea), huwa na hali nzuri sana kifedha, na taaluma zao zimeendelea kwa vifaa na ujuzi wa kisasa wa kiteknolojia. Huku kwetu ni kama tumegeuka na kuurudia ujima. Kila kitu kinazidi kuwa na hali mbaya.
Ndio... Yaani taabu tupu
 
Ma IT wengi wa Bongo ni vilaza. Wangekuwa smart, wangeweza kuutumia ujuzi wao kupanga mikeka ya ku BET na wangeshatoka kimaisha...
Unawaza kinyume nyume sasa mkuu.. Kubet kwenyewe hela .... Unaitafuta alafu unaipoteza kwa bahati nasibu... Think twice
 
Wengi sio wabunifu mkuu, wakisomea na kujua kidogo tu wanafungua ufundi simu sijui, baada ya hapo wanajisahau kutafuta maarifa zaidi. Wanasahau kuwa LIFE IS A TEACHER THE MORE WE LIVE THE MORE WE LEARN. Elimu haina mwisho wanafikiri kuwa na IT certificate au Diploma ndio washamaliza kila kitu.
 
Naona ni zamu ya matajiri wa fani zingine kuwananga watu wa IT. Halafu hivi IT ndio fani gani? Na ninyi mmefanya nini cha maana Bongo ukiwemo mtoa mada? Kabla ya kibanzi kwa watu wa "IT" toa kwanza Boriti kwenye jicho lako

"And why worry about a speck in your friend's eye when you have a log in your own? " - Lord Jesus Christ

log-in-eye.jpg
 
Hakuna tajiri ali invest na Shule muda mwingi au aliumiza Mno kichwa Juu ya Gunduzi ,Ukiona mtu ametajirika Jua ametumia wasomi Vichwa Kujinufaisha kwa kuwalipa ujira, Bill gate anasema Wakati yupo Chuo yule kipanga kabisa Sasa amemuajiri Microsoft Pesa inaletwa na Ujasiliamali ukiwafatilia watu kama Thomas Edison, George wesgthouse,J.P Morgan or Rockfeller ndio utajua Dunia Iko tofauti na Shule au elimu tunayopewa kwenye Makaratasi, Ujanja Ujanja tu nakumudu kupambana na Mazingira ndio unaeza tawala wenzio
 
Kwanza kabisa ubinafsi mtu anataka kufanya kila kitu mwenyewe. Mfano unaweza kuwa IT mzuri lakini kuongea na investors ukashindwa. Kuna tv series inatwa silicon valley inaonyesha ushirikiano na mgawanyo wa majukumu kwenye hii sector
 
Back
Top Bottom