Kwanini Ma IT bongo sio matajiri?

Kwanini Ma IT bongo sio matajiri?

Alifanyaje huyo jamaa nipe ubuyu

mgoogle satoshi nakamoto

mtu hewa huyo mmiliki wa bitcoin.. wataalamu wanahis amesoma havard ila hawamjui mpaka leo ni nani..

hela zote za upigaji malipo ni bitcoin huku mwenye bit coin hajulikani

m google utajua why havard hapafai...
 
Kuna fursa kubwa sana yani pesa mingi ya duniani ipo katika sekta ya teknolojia. Fursa inazidi kukua kila siku but why jamaa zetu bongo hapa hawana mpunga yani kuunga unga kwingi.

Personally am not an IT but i love this profession. Nchi kama bongo ipo nyuma sana lakini yenye matamanio makubwa yakufahamu teknolojia then whats pulling us back.?!

Mi ishu nimeona kwenye management ya hawa talented stars pia na wengi wao kuto fahamu marketing and advertisement.

Costech wanafeli na hubs zingine the push is not that hard. Hebu tuimarishe huu mfumo vijana wapige hela. Mifumo user friendly ambayo kila mwananchi hata mwenye elimu ndogo ya teknolojia anaweza master. Kwa research nliyofanya tech is not that expensive nkimaanisha kuna softwares, systems and tools zinawwza patikana in a cheaper way ughaibuni kwa njia tofauti(kijanja).

Na madini yote haya tufungue cyber mall moja kubwa sana, wajae wabongo humo, wachina na warusi wa kutosha. [HASHTAG]#YouthWeCan[/HASHTAG]
Tatizo hasa siyo wabongo IT ingekuwa inalipa bongo ma IT wa nje wangekuja kuvuna pesa. Tatizo ni gharama za matumizi ya internet inasababisha isiwafikie watu wengi wa vipato vya chini kwani it business mostly ni online services. Pili ni Benki kuu hadi sasa wameshindwa kuintergrate online payment system kwa banks so ni vigumu sana ku provide services on line halafu watu walipie manually. Kingine ni watu wenyewe kujifunza programming lakini hii itatrgemea sana hivyo vya juu.
 
mgoogle satoshi nakamoto

mtu hewa huyo mmiliki wa bitcoin.. wataalamu wanahis amesoma havard ila hawamjui mpaka leo ni nani..

hela zote za upigaji malipo ni bitcoin huku mwenye bit coin hajulikani

m google utajua why havard hapafai...
Duuuhh naisikia bitcoin ngoja nimuone, ila jana ITV malumbano ya hoja kuna mzee alisema amesoma Harvard ila Yupo tu bongo alikuwa anazungumzia resources zetu
 
Ndugu hapa kila kitu ni siasa, tena tunamalizwa na hizo kitu zinaitwa KAULI MBIU
 
Duuuhh naisikia bitcoin ngoja nimuone, ila jana ITV malumbano ya hoja kuna mzee alisema amesoma Harvard ila Yupo tu bongo alikuwa anazungumzia resources zetu
hata chenge mwenyewe kasoma Harvard
sema kila upigaji yupo
 
Naona ni zamu ya matajiri wa fani zingine kuwananga watu wa IT. Halafu hivi IT ndio fani gani? Na ninyi mmefanya nini cha maana Bongo ukiwemo mtoa mada? Kabla ya kibanzi kwa watu wa "IT" toa kwanza Boriti kwenye jicho lako

"And why worry about a speck in your friend's eye when you have a log in your own? " - Lord Jesus Christ

View attachment 525598

"Toa boriti kwanza kwenye jicho lako" Huu msemo nnao sana kichwani. Sijawasema kwa ubaya, im challenging you, you can also challenge others.
 
"Toa boriti kwanza kwenye jicho lako" Huu msemo nnao sana kichwani. Sijawasema kwa ubaya, im challenging you, you can also challenge other sector unayoona opportunity but watu hawachangamkii.
Kitanda usicholalia ni vigumu kujua kunguni wake. Sio rahisi kama wengi mnavyodhani.

Nika hamasisha vijana wenzangu nkaanzisha NGO, baada ya kupambana nayo mwaka to miwili hivii nkafanikiwa kupata fund from the US Embassy $47,000 after a year, baada ya kazi nzuri nkapata tena $50,000. Hiyo process ilichukua miaka 4. (Sijamtumia mtu ni ubishi tu na kukaza kama msuli pepa)
With all those money kwa umefanya nini cha maana na hizo opportunities unazoziona? Si ungeweza kufanya makubwa hata na ma "IT" wa nje ya nchi kama wa Bongo tunazingua? Ni kitu gani kikubwa ambacho hiyo NGO yenu imefanya na that bulky money?
 
Wewe kijana muda unao mwingi sana bado Inshallah jaribu kuunda team kutengeneza mambo na ku market kazi zenu kwa kujiamini and professionally. Tunawahitaji, tutawafata tutawasikiliza tutawawezesha. Am not rich but in a process counting blessings. Karibuni.
Hapo kwenye kuwawezesha ndipo Bongo taralila nyingi. Pia Sera zetu na baadhi ya sheria (au kukosekana kwazo) ni tatizo. Tunapigana na mengi sema basi tu tunavumilia...
 
Kitanda usicholalia ni vigumu kujua kunguni wake. Sio rahisi kama wengi mnavyodhani.

With all those money kwa umefanya nini cha maana na hizo opportunities unazoziona? Si ungeweza kufanya makubwa hata na ma "IT" wa nje ya nchi kama wa Bongo tunazingua? Ni kitu gani kikubwa ambacho hiyo NGO yenu imefanya na that bulky money?

1. Nime train Vijana zaidi ya 300 jinsi ya kuandika effective business plan na kuwaunganisha vijana zaidi ya 400 toka Iringa kwa financial providers zilizowawezesha kupata mikopo katika shughuli zao za kilimo.

2. Nime elimisha vijana 250 toka Bariadi/Simiyu juu ya maana halisi ya Ualbino kuwahamasisha watoe taarifa katika vyombo vya sheria iwapo watabaini uhalifu.

Nimetengeneza maigizo 6 yanayoelimisha jamii juu ya hizo changamoto tajwa hapo juu. Na mengine mengi sana katika jamii yangu.
 
Hongera sana.

Sasa fikiria kuwawezesha ma "IT" walioshindwa kwa sababu ya kukosa mitaji. wako wengi sana mtaani. Caution: Angalia sana matapeli maana siku hizi kila anayejua kubadilisha feni ya PC naye ni "IT" na kila anayeweza kuandika "Hello World" siku hizi ni "founder and CEO", so be careful!
 
BOT wanatubania PAYPAL tungeshakuwa mamilionea
Wala hilo sio tatizo kubwa kuna njia nyingi tu na salama kama Payoneer. Tatizo IT wa Tanzania sio wabunifu wao ni theory nyingi kichwani. Nina amini kama IT unaweza kupata pesa nyingi sana online kama ukiwa mjanja na mbunifu. Kuna rafiki zangu ambao ni IT nilikua nawashangaa sana kukuta wanachart facebook au insta badala ya kuzitumia hizo social network kupata angala 5$ kwa siku.
 
Kweli mkuu hata ubunifu pia ni changamoto kwa maIT wa bongo,
ila Mimi binafsi nimetuma maombi mara kadhaa kuomba hiyo card ya payoneer ila mpaka tarehe ya kuarrive hiyo card inafika lakini hola
hata sijui nakosea nini?
 
Kwa haraka nimeona shida mbili za fasta kwa IT's wetu.
Kwanza wengi hawapendi code. Ingawa nahisi IT sio code peke ake but naona code ni kama lugha muhimu. So kama mtu hapendi code means automatic hataweza kuexpress idea yake fast katika computer
Pili ubunifu ni mdogo na hata ukitoa idea unaonekana chai.

Kwa IT's mliomo humu ndani naomba niwape task ambazo zinaweza kuwa good business ideas mbeleni. Mkifanya research naombeni mrejesho.

1: jaribu kufikiri kuhusu kuunganisha maduka au biashara zozote kwa magroup kupitia website na smartphone app. Hapo unatengeneza website yenye kuonesha maduka na bidhaa zilizopo au coffee shops zilizopo kwa mfano unaweza kuichambua kariakoo na maduka yake na coffee shops zilizopo mjini na hata hotels au logdes kubwa pia. Unaweza kucharge kidogo kidogo kwa matangazo kwa mwezi but as time goes unaongeza charge. Ifike mahali ukiwa dar au mkoa wowote unaangalia ktk app yako sehemu ya kula, kunywa, kulala na kufanya shopping.
Hii idea nilikuwa nayo mwaka 2008 nilipokuwa A level ilianza kwa kutaka kuanzisha blogu itakayokuwa inaunganisha past papers za shule zote Tanzania. But sikusoma computer so nilipiga chini but bahati nzuri nikakuta inafanywa na website moja inaitwa karakoo digital hapo posta. But nahisi huyu mtu bado hajafanikiwa sana ktk hiyo idea... kama kafanikiwa mnijuze.

2: nilikuwa nafikiri kuhusu business cards. Kuna muda nilikuwa natafuta kazi nikawa na mzigo wa business cards ktk wallet. Nikafikiri how IT guys wanaweza kutransform na kutengeneza app itayoweza kutunza hizi cards. Hiyo sikufiria sana but nilitoa idea kwa IT mmoja akasema hiyo inatatuliwa na linkedin. I dont think so. Na nyie mnaweza kufikiri zaidi kuhusu hiyo idea.

Kwa leo ni hizo tu. Idea nyingine kubwa sana kuhusu umeme bado ninayo kapuni hiyo nitaifanya mwenyewe na kuwapa mrejesho ingawa sijasoma electrical engineering.
So jaribuni research ya hizo idea kwanza wakuu then tupeane mrejesho. May be ni idea za kijinga but i think zina matter.
 
Kweli mkuu hata ubunifu pia ni changamoto kwa maIT wa bongo,
ila Mimi binafsi nimetuma maombi mara kadhaa kuomba hiyo card ya payoneer ila mpaka tarehe ya kuarrive hiyo card inafika lakini hola
hata sijui nakosea nini?
Labda unakosea kwenye postal address unayotumia. Mm ilifika na kuna watu niliwasaidia na zimefika pia.
 
Back
Top Bottom