Kwanini Ma IT bongo sio matajiri?

Mkuu Mfumo wa Elimu nchini unapumulia mipira yani Curriculum ni Outdated kabisa na vyuo havina muda wa Research na kuandaa mitaala iliyopo sokoni Wao wanajali kukusanya Fees na Kutuswaga kama ngombe mpaka tu graduate
 
ngoja Mimi nichangamkie fursa ya kuunda "kiwanda cha ma-IT",halafu nitamuomba waziri mwenye dhamana ya masula ya viwanda na biashara aje afanye ufunguzi,bila shaka atakuwa Charles Mwijage.

hakuna namna,lazima tuongeze idadi ya viwanda.
 
kwani mmiliki wa jf sio tajiri? wapo ma IT matajiri pia Tanzania, kama vile ambavyo kuna Ma IT masikini huko Duniani ambao wanaishia tu kuwa wauzaji/wazungumzaji kwenye show room.

Bado hajawa tajiri bro, kuna vitu vingi anamiss. Kwa hii network aliyonayo naona kama haitumii effectively, he can do better na kufikia levels za private jet, mansions, fancy cars n.k Wafanyabiashara bongo ndo wanatisha walio kwenye products na service wanakuja kwa kasi.

Kama JF founder akatuliza akili zaidi na kuitanua hii network yake ki biashara as in deep kiasi cha kupenetrate katika international markets na kushiriki events za kutosha silicon valley huko basi atatoboa sana na si yeye tu bali wengi sana waliomiss management na marketing skills. Exploration muhimu sana.

Waduniani hao uzembe tu na kutokujitambua. Kukulia mazingira ya kuchi kinachangia kwa hao watu.

Ukitaka amini kama hii sekta ni hatari angalia top 10 ya world's richest. Wakiongozwa na gates, kuna kina zuck wakali wa google n.k

Its a dream that can be fulfilled, we shouldn't settle for less.
 
Ma IT sio matajiri karibu dunia nzima, kuna wachache tu hasa silicon valley wamekuwa matajiri na tena hao kuwaita ma IT ni kosa, kilichowapa utajiri ni biashara/entrepreneurship.

Hii ndio akili na ndio jambo nalotaka nlifanyiwe kazi... Kutambua why IT wa silicon wanatoboa kuliko wengine simply ni koz wamechukua ile IT yao na kuitengenezea mfumo wa kibiashara na kufata principles za entrepreneurship na marketing.

Inatakiwa kuuza ujuzi, na ili huo ujuzi ununuliwe na kukubalika lazma uutangaze na kabla ya kuutangaza lazma ubrand kazi yako. Simple strategies hizo. Advertising is expensive but pays back big time. Dunia nzima but watanzania hakuna kabisa kinachoniuma sio kwamba hawana uwezo but wengi wanakosa mentors wa kuwafikisha pale dream ilipo.
 
Mimi nazan ni mfumo wa elimu. Mtu anasoma darasa la kwanza mpaka advance haifaham hata computer. Hapo akifaulu anachagua IT, anaenda chuo na kusoma miaka 3 then anagraduate na kurudi mtaani. Wenzetu wamekeza hayo mambo kweny elimu, mtoto anakua akijua hzo mambo ndio maana utaskika kijana wa miaka 14 afanya hiki, huku bongo kijana wa miaka 14 anajifunza kusoma, kukalili na kuandika,

Ni kweli but tukiongelea mfumo wa elimu kwa style hii hapa kila sekta imeumia kinachotakiwa ni kupambana na tatizo lililotokea. Siri ya kuwa tajiri ni marketing. Unaweza ukawa naquality good but bila marketing ni bure. So kuna ITs wanatengeneza systems kali sana but zinaishiwa kwenye harddisks tu na apps kuna watu naamini wana appz matata ambazo ni solutions nzuri but zinaishia kuwa kwwny store huku.

Demand ya teknolojia ni kubwa sana and this ukiweza ichangamkia vema lazma iwatoe hawa jamaa...
 
Nazani Tatizo lipo katika mfumo mzima wa Elimu, Mwanafunzi Anaifahamu Laptop Akifika Chuo, Unategemea nini??

Wakati ni vitu Ambavyo ilitakiwa Mwanafunzi ajue Toka Akiwa Shule ya msingi.
 
Not so easy.
Urasimu umejaa Tanzania.ao
Costech wenyewe ni wapiga dealz akuna kitu pale! Wanaa cha wagunduzi wa kweli wanapiga hela na makanjanja!
Pia serikali na idara usika azipo kusaidia hilo! South Africa walivyoanzisha Black empower ment ilikuwa kwenye tender ukiwa black tayari ni marks 20! Na serikali ilikuwa analisimamia hilo.

Costech na TCRA wanazingua tu. Inabidi ije regulatory body nyingine pia kitu kama IT marketing Hub kinahitajika. Platform trusted itakyowasaidia kukutanisha IT programmers na investors. Kuna investors wanahitaj some systems ambapo wako willing to pay the price but unakuta hawajui kwa kuanzia tena kama bongo tech ndo miaka mitano hii imekua ndo ishu kabisaaaa. All in all fursa ni kubwa sana bado. Something big can still be done
 
wapi ambako ni matajiri

10 hawafiki kwanza hakuna kwa utajiri nnao uongelea mimi level zile yani. Unajua a single program inaweza ikakupa hela ndefu sana kama utaichukulia as a real business(serious) and promote it. Nnapoongelea marketing ni swala muhimu sana aiseee very deep crucial yani.
 
wengi wao ni waoga, wanaogopa shortcuts , wanaogopa kutoa solution tofauti na walivyo fundishwa, ni wavivu wa kufikiri na hii ni kutokana na mazingira magumu yaliyowakuta kipindi wakiwa masomoni, wengi wao reseach zao ni za kukopi, kingine kikubwa ni katika au sheria zina wabana wazivuke mipaka wakiogopa kupelekwa ostabey, wengine wanadanganywa na vi overtime na vijipesa na vi access na mabosi wao huku wataalamu wakiendelea kuvuta mpunga...

kwa kumalizia , wana ma kumpyuta wajifunze kuwa na lugha inayoeleweka kwa wateja, wawe ni watatuzi wa matatizo ya jamii kwa kutumia computer bila kujigamba...nk
 
Kweli mfano king kapita hana lolote mjini

Ahah ndo hapo sasa tatizo nini. Strategies kushnei huu mchezo hautaji hasira hafu uvumilivu, persistence na hardworking ni vitu muhimu sana. Dah yani nna uchungu hivi ma cheats na tricks zooote zilizojaa online mtu wa IT unashindwaje kutoboa asee. Hapana we need to push it bongo. Wazee wa IT kazeni buti kama vp game likizidi kuwa tight mkishindwa kabisa kupata marketing management kwa kasi ya tech bongo bora mpige kinaigeria tu. Maana IT wa nigeria na ghana na senegal ni balaa hafu wanakula maisha. Hapo south napo wazee wa makompyuta madogo tu wanapiga hela ndefu.
 
ngoja Mimi nichangamkie fursa ya kuunda "kiwanda cha ma-IT",halafu nitamuomba waziri mwenye dhamana ya masula ya viwanda na biashara aje afanye ufunguzi,bila shaka atakuwa Charles Mwijage.

hakuna namna,lazima tuongeze idadi ya viwanda.

Nafkiria kufanya hii kitu. Na week ijayo Inshallah naingia China kukutana na couple of investors ku discuss hili. Fanya hivo kaka watatusua wengi sana ukiwemo we mwenyewe.

Tanzania ya viwanda, tusisahau na viwanda vya teknolojia. Hafu kilimo huko sijui nini kuna digital machines nyingi tu ambazo zinaweza kuja fanyiwa assemle bongo na vijana wetu wakajifunza wakaanzisha vyao.
 
They ain't creative to that extent

Wanajitahidi bwana tena siku hizi creation imekua chache sana maana kila kitu almost already predicted or imagined ni magenius tu wa kuimplement ambao wengine bongo humu wamo na solutions zao kwenye laptops tu hawajui pakuanzia au wanachukulia poa mautajiri wanayokalia. They marketing skills
 
Nazani Tatizo lipo katika mfumo mzima wa Elimu, Mwanafunzi Anaifahamu Laptop Akifika Chuo, Unategemea nini??

Wakati ni vitu Ambavyo ilitakiwa Mwanafunzi ajue Toka Akiwa Shule ya msingi.

Binadamu tunajifunza na ku adapt, ni kukomaa tu kama mfumo ndo tayari ushakua hivo kulalamikia si kutatua. Kujua laptop siku nyingi na juzi utofauti unakuja kwenye experience na sio kuitumia so i dont take this as an excuse.

Kuna mtu anajua computer toka 98 but hadi leo hajui ku run au ye anajua basics tu.

Vijana wadiriki na kujifunza jinsi ya kujitangaza. Wajifunze the meaning of Branding and Marketing
 
wengi wao ni waoga, wanaogopa shortcuts , wanaogopa kutoa solution tofauti na walivyo fundishwa, ni wavivu wa kufikiri na hii ni kutokana na mazingira magumu yaliyowakuta kipindi wakiwa masomoni, wengi wao reseach zao ni za kukopi, kingine kikubwa ni katika au sheria zina wabana wazivuke mipaka wakiogopa kupelekwa ostabey, wengine wanadanganywa na vi overtime na vijipesa na vi access na mabosi wao huku wataalamu wakiendelea kuvuta mpunga...

kwa kumalizia , wana ma kumpyuta wajifunze kuwa na lugha inayoeleweka kwa wateja, wawe ni watatuzi wa matatizo ya jamii kwa kutumia computer bila kujigamba...nk

Sure. Well said. Matatizo mengi haya yanayotuzunguka katika jamii yanaweza kuwa solved digitally ni tu kufikiria tatizo gani and how. Kazi kwao but fursa hii.
 
Lack of creativity! Nilikuwa na idea moja ambayo ningekuwa Proffessional developer ningekuwa mbali sana. Nikajaribu kumshirikisha jamaa mmoja anaitwa matthew humu lakini kumbe nae ni tapeli. Bora nife nayo idea yangu

Leta idea hiyo tuifanyie kazi tupate hela, mi sio IT but nna uwezo wangu binafsi katika uhandishi wa miradi ya fedha ambayo itasaidia kuwafikia investors kirahisi au kutupa muongozo wa project. Ma IT wabongo ndo hivo kazi kweli kweli. Customer service 0 kwa hata hao few customers wanaopata sa kutusua kwa style hiyo itaendelea kuwa dream.
 
Back
Top Bottom