Ma-IT watanzania wako wengi. Check github ujionee mwenyewe kuwa wabongo wako wengi. Ila kwa kifupi shida ni moja; kama wewe ni software developer mzuri, hauna sababu ya kubaki bongo. Nchi kibao duniani zitakupigania na kukupa visa karibu bure.
Nikupe mfano. Nilirudi bongo baada ya kusoma nje kwa muda mrefu. Nilitaka kuanzisha kampuni ya software na kujitegemea. Nilianzisha kampuni na kuanza kuzunguka mtaani kuuza solution yangu. Tatizo kubwa nililiona ni kuwa wabongo hatuna uwezo wa kuona solution mpaka inapofika too late (hii ni shida kubwa duniani kote ila bongo nimeliona zaidi). Kwa maana nyingine, mpaka tuone wengine wanatumia kitu ndio tunaanza kudandia. Idea zetu za software ni za kizamani sana. Na software development ni eneo ambalo linakuwa na kubadilika haraka. Mfano ni baadhi ya kampuni na sekta kibao serikalini zinang'ang'ania kuwa na server kwenye ofisi zao. Mambo ya kuwa na cloud computing ni kitu kigeni. Wengi wanabaki kuhofia security ya cloud computing. Ukijaribu kuwaelewesha kuwa security ni balaa zaidi unapokuwa na server zako mwenyewe, wanabaki kufikiri kuwa mradi unaiona server kila siku basi hiyo ndio security (kana kwamba server ikiibiwa ndio security imefeli). Baada ya kusota miaka kadhaa kujaribu biashara bongo bila mafanikio nikaamua kupiga kazi na kampuni za nje ya nchi kama consultant nikiwa bado bongo (remote working). Mshahara wangu wa kwanza ulikuwa $3000 kwa mwezi. Kipindi nasota na wabongo, nikipata $800 kwa mwezi nilikuwa najiona mjanja. Huo mshahara wa kampuni za nje hata sikupigania na tayari nilikuwa napiga hela mara nne ya nilichozoea. Nilikuwa single, sina demu wala mtoto. Naomba niwaulizeni, utabaki kujaribu kupiga dili na wabongo baada ya hapo? Baada ya kama mwaka hivi nikaanza kudai hela ambayo ni halali kwa experience yangu. Bila mabishano mshahara ulipanda hadi $4800 kwa mwezi ($30/hr).
Unauliza ni kwanini hakuna matajiri wa IT bongo? Jibu hilo hapo juu 😀 Mpaka siku bongo tutapoanza kuona umuhimu wa IT, vijana wote wanaoweza hizi kazi tutabaki kupiga biashara na nchi ambazo zinafadhili kazi zetu.