Kwanini Levina Mukasa alijiua UDSM?

Kwanini Levina Mukasa alijiua UDSM?

Kuna kabinti fulani ka Njau kalikuwa kanasoma Kiraeni, nilikapendaga na ilikuwa nioe KV, tatizo likawa vitoto vya KV vimefunzwa mambo fulani ni mpaka baada ya ndoa, sisi watu wa mjini, unataka kufanya kwanza test drive ndipo, ulipende gari ndipo ulinunue, wenyewe wanataka ulitazame tuu ulinunue kwanza ndipo uliendesha, hakuna test drive, hiyo tukashindwana.
Kiukweli mabinti wa KV wa enzi hizo, ilikuwa ni bila bila mpaka kieleweka, hakuna test drive!.
P
Hahaaa nimecheka sana, ulitaka kumla dada yangu kimasihara hivyo! hawapogo hivyo tunda linatunzwa mpaka wakati ulioamuriwa hata kama ungetumia mbinu kama za PUNCH angewapa taarifa kaka zake taarifa basi ingekuwa balaa kweli kweli ungeacha vitendea kazi vya Umma.
 
Hahaaa nimecheka sana, ulitaka kumla dada yangu kimasihara hivyo! hawapogo hivyo tunda linatunzwa mpaka wakati ulioamuriwa hata kama ungetumia mbinu kama za PUNCH angewapa taarifa kaka zake taarifa basi ingekuwa balaa kweli kweli ungeacha vitendea kazi vya Umma.
Kweli Wachagga wagumu.
P
 
Hao Saloti na Victor sijui wanajisikiaje sasa!!?? Hivi familia haiwezi kufungua kesi ya madai Chuo Kikuu au against these people??
Pumbavu sana, nadhai familia inapaswa kupewa msaaa wa kisheria hapa. Wote walioshiriki kuweza kuchukuliwa hatua, kwani "Jinai" huwa hai-expire. Lakini zaidi ya hapo, most guys hapo UDSM never been gentlemen...Kuna mmoja anadai alishuhudia Binti akimeza vidonge vile na hakuchukua hatua kisa yupo na ka-malaya kake kutoka mtaani. Elimu yako haikuwa na msaada, your manhood never exercised to save life...Pumbavu sana. I am always against injsutice at whatever cost.
 
Nimesoma uzi wote kwa masikitiko but niliposoma comment kua levina alichanganya wakaka wawili ata once na masikitiko yangu yakaishia hapo
Wewe unamuaminije huyo bwana? Mimi nilikuwa namfahamu marehemu personally hakuwa mtu wa tabia hizo!!! Huyo ni muongo
 
Inasikitisha sana. Wapi Omar Saloti na Mark Victor, wanawaambia nini watoto wao sasa hivi?
 
Haya makundi yanaanzaga mbali sana,nakumbuka nikiwa o level japo ni miaka ya juzi juzi shule moja ipo Tanga inaitwa GALANOS acha bhana kulikua kina watu ni vichaa wakuotea mbali,walikua wana uwezo wakuweka vipeperushi vyao na machata yao mahali popote pale ndani au nje ya shule yani sehemu yoyote iwe chumban kwa headmaster,iwe ofisin kwa kwake iweofisin kwa mkuu wa wilaya na hata ofisi za jeshi la police,yani kuna chata zilikua zinapigwa mahali popote pale sijui hawa jamaa huwa wanatokea wapi na ujasiri wao wa ajabu kiasi hiki,na walikua wakianzisha mgomo hakuna ambae hatashiriki wataka hutaki lazima uingie na uwe active members,kilikua kuna mabweni yanaongoza kwa bangi ambayo ni kahawa na chai huko kulikua kuna vutwa bangi mpaka waalimu wanaogopa kuingia,hawa jamaa walikua hawavai sare wakitoka nje ya shule sasa konda wa daladala jifanye humjui kwamba ni mwanafunz uone mziki wake,kuna mwaka tulipiga kijiji kizima cha majani mapana na nguvumali yani tulitembeza kichapo chakufa mtu,mwisho wa siku uongozi wa kijiji ulikuja shule kuomba msamaha utadhani wana kosa,na kwa amri sisi ndio tuliwapangia kima cha nauli nakuweka sheria zetu kibabe,kwakweli nikikumbuka haya mambo napata kitu hawa watu huwa ni natural created yani kuna majamaa yalikua yanapiga bangee ile kisenge lakini yaametoka na single digit o level na a level,ilikua mgomo ukitokea pale skuli hakuna aneweza kuustopisha labda kamanda wa jeshi pale kange na ocd na rpc ndio walikua wakija tena kwa mashart magumu kutoka kwa wanafunzi.
 
Heeee haya yalitokea hapahapa tanzania mkuu?

Dizaini zamani wanafunzi wa kiume walikua wanaume hasa sio vishalobalo vya siku hizi hata ngumi havijui kuikunja
Hawa wahusika wakufanya haya huwa wapo kila kona kwenye mashule makubwa tanzania na ndio wanaokuja kua hatari sana baadae wanapokuja kukutana vyuo vikuu,nakumbuka matukio mengi sana yakutisha ambayo niliyapitia pale GALANOS enzi za kinala,wanafunzi waliokua wanasoma pale wengi walitokea mikoa ya bara sio pwani na kama ukimkuta mtoto wa pwani anasoma hapo muangalie mara mbili lazima atakua nae anapiga bangee tena yuko vizuri sana nakumbuka tumesoma na watoto wa jaji mkwawa akina joseph dah jamaa nae alikua amepindaga sana,alikua anaonhoza kwakuongoza migomo kama hana akili alafu hakuna yeyote anaeweza kumfanya kitu,siku moja mwalimu alimchapa mwanafunz ambae alikua ana kibali chakutokuadhibiwa,alivyomchapa yule mwanafunzi akaanguka chini kumbe na kifafa mwalimu alivyokua mjinga anamwambia joseph mkwawa muamshe mwenzako,joseph akamwambia"wewe mjinga kweli wewe uliyempiga ndio umuamshe"ticha akaamuru wanafunzi wengine wamuamshe yule jamaa pale chini hapo ndipo moto ulipowaka,yule mwalimu alichezeshewa kichapo chakufa mtu wanafunzi wakaenda nyumbani kwa mwalimu wakakuta amepika wali wakaumwaga wakavunja samani za ndani wakambaka binti amabae alikua mdogo ake na yule mwalimu na hapo ndipo vurugu zilipoanza ilikua jioni muda wa parade au rolcal,walimu walichezea kichapo chakufa mtu na shule iliharibiwa vibaya mno gari za police zilivunjwa vioo nakutobolewa matairi hakuna cha field force wala nini,kikosi cha wana GALAXY kilikua na nguvu sana yani kilikua ni cha ajabu mno,kwakweli tunatoka mbali sana na haya majitu mengi yao yamefanikiwa kimaisha yani yapo kwenye system,wengine ni maafisa usalama wa taifa ba wengine wapo kwenye sekta mbali mbali na kaa ukijua hizi shule kubwa tanzania sio wote wanakua ni wanafunzi wengine ni watumishi wamekuja kikazi pale.
 
JIULIZE KWENYE KITI CHA MKUU WA MKOA AU MKUU WA WILAYA WALIWEZAJE KUWEKA CHATA NA VIPEPERUSHI?CHUMBAN KWA HEADMASTER AU OFISIN KWAKE WANAWEKA CHATA JIULIZE WANAWEZAJE?ACHANA NA HAWA WATU.SHULE KAMA MAGAMBA,KIBITI,MAZENGO ZILIKUA HATARI SANA NA NDIO AMBAZO WANAFUNZI WAKE WALIHAMISHIWA GALANOS MIAKA AMBAYO ZILIBADILISHWA.KULIKUA KUNA VICHWA HUKO NI BALAA.
 
Wanafalsafa wanasema.
Ukifanya mambo mema wakati wa uhai wako, japo kuwa utakuwa umekufa lakini utakuwa u hai.
Ukifanya mambo mabaya wakati unaishi, japo kuwa utakuwa unaishi lakini utakuwa umekufa.
Hawa wanyanyasi wa kijinsia waliokuwa wanajiita punch kama bado wanaishi ni wazee na ni wanafamilia wanaendelea kuteseka kwa haya waliyokuwa wanayafanya wakati wao wa wa Foolish age.
 
Pascal Mayalla,

Mkuu Bangi haiachwi, wapo watu wazee na wakubw atu bado wanavuta mpaka kesho.
Ukishatumia BANGE inakua ngumu sana kuacha,ila kila mtu ana matumiz yake kulingana na aina ya ubongo na uwezo wake waku handle,kuna mchiz wangu alikua hawezi kufanya pepa bila ya bange,jamaa alikua tishio kwenye hesabu na o level alipiga one akachukua pcm akapangwa ifunda tech huko ndio akawa kichaa,sasaivi yupo kwenye systm za serikali ameajiriwa na ana maisha safi tu ila bange kama kawaida.
 
Umenikumbusha mbali sana Mkuu.

Huyu dada moja ya sababu iliyofanya ajiuwe inasemekana ni kukosa uvumilivu kulikochangiwa na kutokwenda JKT.

Wengi wanasema kama angelikwenda JKT, basi matusi ya PUNCH yasingelimtisha kabisa maana JKT, wale ma-Coplo Magwegwa, Gumo, Wawa, Wera, Manyilizu, Mandevu, Chacha, Matron Makunyanzi nk kwa kweli walikuwa wanajua kutukana na kunyanyasa.

Kuna Madada wawili sikumbuki walisoma miaka gani, ambao nasikia Mzee Punch alishindwa kabisa kuwanyoosha. Walikuwa wakiwahi kula kama Wanaume na kuvaa suruali, tabia ambayo Punch hawakuipenda. Basi wakaanza kuwashughulikia. Na wao wakaanza ukorofi wa kwenda mapema Cafeteria kuangalia wamechorwa na nguo gani, basi wanarudi chumbani na kuvaa kama walivyochorwa ili kila mtu awafahamu.

Walisumbuana na Punch hadi mwisho jamaa hawa wakakosa nguvu na kuwaacha. Walipowaacha na wao kweli ndipo wakatulia kabisa na kuacha ukorofi wao. Ila hii kama sikosei inaweza kuwa ilitokea miaka ya 70 kwa sababu zote ni story ambazo mie nilisikia na kwa bahati mbaya, sikusoma UDSM.

Halafu kweli dunia imebadilika Bandugu. Siku hizi wanafunzi wanajibandika wenyewe picha za uchi wa Mnyama na siyo za kuchorwa tena. Wengine walienda kabisa na kuanza kujieleza "nimebakwa Meen" na bila wasiwasi wowote huku TV Camera na Radio zinawarekodi. Mzee Puch angelikuwepo basi watu wangelilipa ili wawekwe pale na wajiongezee umaarufu.

Kufa kwa Punch ilikuwa ni lazima hata kama Levina asingelijiuwa. RIP LEVINA.

Kuna msichana mmoja tulisoma naye hata huko Primary alipofika alikuwa hana hiyana na wanaume, akapanchiwa kama "Hailali" wala hakubadilika alikuwa anatwanga tu. Baadaye alikuwa ni afisa mwandamizi sana hapo ARISA. Mwingine alilipanchiwa kama "Maasai Warior"- naye wala hakutishika kabisa akaendelea na mambo yake kama kawaida, baadaye akwa Mwanamuziki maarufu kidogo akiwa anajulikana kama Kalala Kinasha. mwingine naye alipanchiwa kama "Kuku wa Kishenzi" tena angali fresher kabisa, naye ile jeuri ya jeshi haikumtisha, baadaye aliendelea hadi kupata Masters. Kwa hiyo nakubalina nawe kuwa kutokwenda JKT kulichangia kutokuwa na uvimilivu dhidi ya matusi.
 
Ukishatumia BANGE inakua ngumu sana kuacha,ila kila mtu ana matumiz yake kulingana na aina ya ubongo na uwezo wake waku handle,kuna mchiz wangu alikua hawezi kufanya pepa bila ya bange,jamaa alikua tishio kwenye hesabu na o level alipiga one akachukua pcm akapangwa ifunda tech huko ndio akawa kichaa,sasaivi yupo kwenye systm za serikali ameajiriwa na ana maisha safi tu ila bange kama kawaida.
Siyo kweli mzee, mbona mimi nilitumia sana lakini baadaye nikaacha.
 
Kama miaka hiyo tuliweza kutoia wataalamu,basi tujitafakari sana.
 
Back
Top Bottom