Kuna msichana mmoja tulisoma naye hata huko Primary alipofika alikuwa hana hiyana na wanaume, akapanchiwa kama "Hailali" wala hakubadilika alikuwa anatwanga tu. Baadaye alikuwa ni afisa mwandamizi sana hapo ARISA. Mwingine alilipanchiwa kama "Maasai Warior"- naye wala hakutishika kabisa akaendelea na mambo yake kama kawaida, baadaye akwa Mwanamuziki maarufu kidogo akiwa anajulikana kama Kalala Kinasha. mwingine naye alipanchiwa kama "Kuku wa Kishenzi" tena angali fresher kabisa, naye ile jeuri ya jeshi haikumtisha, baadaye aliendelea hadi kupata Masters. Kwa hiyo nakubalina nawe kuwa kutokwenda JKT kulichangia kutokuwa na uvimilivu dhidi ya matusi.