Kwanini kujenga nyumba imekuwa ni fashion kwa Watanzania?

Gulio Tanzania

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
2,160
4,543
Imekuwa ni jambo la kushangaza kwa watanzania wengi kuamua kujenga na kuendelea kuishi maisha yale yale.

Unakutana fundi fenicha aliyefanya kazi miaka 15 anakuambia anamalizia ujenzi ukiangalia ufanyaji kazi bado wa kusubiri hela advance kwa mteja hafikirii kabisa kuwa na store kubwa utakayotoa faida kubwa zaidi kwa haraka zaidi kutokana na uzoefu wake.

Unakutana na dereva yeye miaka na miaka anaendesha gari za watu anakuja na habari njema amejenga ni vyema lakini kwanini asikilie kumiliki gari yake.

Unakutana na kijana kinyozi ana uzoefu wa miaka saba anakuambia nimejenga vyumba vitatu nataka nihamie kwangu ni jambo jema lakini hafikirii kama pesa hizo kama angetumia kufungua barbershop kubwa ambayo ingempa faida maradufu.
 
😂 kijana inaonekana huna future na maisha yako, inaonekana umekata tamaa kabisa... Yaani mtu kujenga makazi yake ya kudumu wewe unaona si muhimu bali ni fashion..? Hata kama ni fashion basi ni nzuri maana inakuhakikishia maisha bora marefu yenye utulivu...
Mmekuja na mihemko lakini point yangu ya msingi ilikuwa ni kwamba kwanini watu wanawaza kuanza kujenga kabla hawajamiliki uchumi mkubwa
unakaa bure na unakula bure mkuu....?
samahani kwa swali langu nataka nijue kwanza apo
 
Mmekuja na mihemko lakini point yangu ya msingi ilikuwa ni kwamba kwanini watu wanawaza kuanza kujenga kabla hawajamiliki uchumi mkubwa
😂 Kumbe tunahangaika kujadili na kitoto kisichojua maisha... Uchumi Mkubwa ni upi huo??? Unakula bure unalala bure unakunya bure, basi ukiona wanaume wanajenga nyumba unadhan ni kazi rahisi ambayo na wewe uliyetoka shule juzi umeahidiwa kutafutiwa kazi utaweza kujenga ukishika mamilioni...
 
Watanzania wasipotumia hii neema tuliyo nayo ya kumiliki ardhi watakuja kujuta. Kujenga ni kuipa thamani ardhi. Kwa mfanyabiashara makini lazima ajue umuhimu wa kuwa na nyumba. Tena sio nyumba tu bali yenye furnitures na vitu vyote muhimu vya ndani.

Inapunguza sana gharama za maisha. Mleta uzi ni miongoni mwa watu wajinga kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya binadamu. APUUZWE.
 
Wabongo wanapenda sana kujenga, kwao kujenga ndo mafanikio...kuna ndugu yangu majuzi ananishauri nijenge hata chumba na sebule, nikajisemea huyu mzima kweli ..sina kitega uchumi chochote cha maana naanzaje kujenga?
Majuzi zaidi ya 20m nimewekeza kwenye buashara ila ndo hivyo hata kiwanja sina .

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
Hata kama unafanya biashara jiwekee mikakati ya kujenga nyumba ya ndoto zako mapema.
 
Inaonekana mleta mada huna familia

Kwa sisi tulio na familia na watoto tena unakuta jinsia tofauti inabidi ufanye maamuzi ya kujenga ili familia ipate kwanza sehemu ya kulala..

Kuna biashara nyingine kama ulivyosema haziwez kukua mara nyingi zina vikomo. Mfano barber shop, dereva nk

Ila mawazo yako yapo limited sana je mtu aliyeajiriwa na serikali? aongeze nini kwenye kuajiriwa kwake
 
Inaonekana mleta mada huna familia

Kwa sisi tulio na familia na watoto tena unakuta jinsia tofauti inabidi ufanye maamuzi ya kujenga ili familia ipate kwanza sehemu ya kulala. .

Kuna biashara nyingine kama ulivyosema haziwez kukua mara nyingi zina vikomo. Mfano barber shop, dereva nk

Ila mawazo yako yapo limited sana je mtu aliyeajiriwa na serikali? aongeze nini kwenye kuajiriwa kwake
Hata kama unafanya biashara kumiliki ardhi na kujenga ni muhimu sana. Wajanja wote kwenye biashara wako mstari wa mbele kumiliki ardhi na kujenga.
 
Watanzania wasipotumia hii neema tuliyo nayo ya kumiliki ardhi watakuja kujuta. Kujenga ni kuipa thamani ardhi. Kwa mfanyabiashara makini lazima ajue umuhimu wa kuwa na nyumba. Tena sio nyumba tu bali yenye furnitures na vitu vyote muhimu vya ndani. Inapunguza sana gharama za maisha. Mleta uzi ni miongoni mwa watu wajinga kabisa kuwahi kutokea kwenye historia ya binadamu. APUUZWE.
Hujamuelewa mleta uzi hatakataa kujenga ila jenga ukiwa ushazungusha hela yako mara kadhaa yaani kama una biashara tayari ushazungusha faida hata mara kumi ndo uanze kujenga ili kukuza mtaji.
 
Back
Top Bottom